Ndugu yetu huyu amekuja na tamko la kumkosoa Gwajima juu ya masikitiko yake na ushauri alioutoa kwa serikali kuhusu utekaji unaoendelea.
Pasco ni mwanasheria, mtu ambaye anapaswa kuheshimu katiba na sheria. Kwa uanasheria wake tulitegemea amuunge mkono Gwajima kwa sababu licha tu ya kutumia haki ya kikatiba na kisheria kutoa maoni yake na kushauri serikali bali pia Gwajima ameonyesha masikitiko yake juu ya Haki ya Kuishi ambayo ni haki ya kikatiba na haki ya binadamu. Yaani mwanasheria anampinga mtu anayetetea haki ya kuishi?! Inasikitisha sana.
Pasco pia ni mwanahabari, mtu ambaye ulitegemea apaze sauti zetu na sauti ya Gwajima na kuhoji, lakini ndio kwaaanza.
Unajiuliza uanasheria wake una msaada gani kwa jamii?
Kuna makala mpya imewekwa humu kuwa wote wanaowalaumu au kuwasakizia wenzao wapiganie haki zao wakati wenyewe wamo humu kwa ID fake niii..... hao tunaowasema wapo humu kwa majina halisi na walishapitia mambo magumu kutokana na kujifanya watetezi wetu.
Je walipoingia kwenye shida tuliwasaidia nini?
Mimi naamini huyo Gwajima kwenye dhamiri yake moyoni kabisa wala hapiganii maslahi au kuwatetea hao anaowataja bali kama walivyowanasiasa wote Duniani wao ni Opotunist wanaangalia upepo unavumaje wakati huo na wao wanapita mulemule lakini lengo ni maslahi yao wenyewe.
Kwa sababu hayo anayoyashutumu mbona hakuyashutumu awamu iliyopita? Au pale yalipooanza tuu?? Why nyakati hizi wakati wanaelekea kwenye michujo ya wagombea????
Inamaana tayari ashazidiwa huko jimboni kwake lazima kuna mtu kamzidi kete anataka kumtoa jimboni na ameona wazi hakuna msaada kutoka juu kama aliopata mwaka 2020 live kabisa against waliomshinda kura za maoni na against Halima Mdee.
Mfuatilieni muda ni hakimu, mambo yasipoenda kama anavyotarajia yawe atapiga uturn mpaka mtashangaa na mtaanza kumtukana matusi yote mnayoyajua.
Ulimwengu huu hakuna wa kukupigania haki yako zaidi yako wewe mwenyewe. Pigania haki yako kwa akili nyingi bila kuathiri uhai wako ambayo ni zawadi ya thamani kubwa kuliyopewa na Mungu, Kabla ya chochote tazama familia yako na wote wanaokupenda au kukutegemea halafu pima kipi cha thamani kwako???
Je unachokipigania kwa njia unayoitumia je una hakika utafanikiwa???? If not change strategies tumia njia ya maarifa na akili nyingi, ukishindwa pigania familia yako pekee ile, isome na kukidhi mahitaji muhimu.
Ukiona kwote kugumu join them strategically ukiwa na malengo ya kuwa nao mpaka ufikie level fulani ambayo itakupa nguvu ya kutimiza unayoyataka au kupata fursa ya kuwa sehemu ya maamuzi au ushauri au kujenga mazingira rafiki na wafanya maamuzi ili uweze kuwa influence katika maamuzi yao kulingana na mtazamo au interest zako(robbing).
Ukishindwa na hilo basi we dili na fursa tuu unazoweza kuzipata kupitia mfumo huo huo usioupenda. Be opportunist always. Dunia ngumu hii na inawenyewe haigusiki kwa namna yeyote(kamuulize Putin).
Sasa wewe huna nguvu, rasilimali, ulinzi, mtaji, ushawishi wala plan b eti ulichonacho ni mdomo tuu wa kuongea ongea ovyo dhidi ya wenye nguvu litakalokupata hata ukifa huwezi hata kuiona mbingu zaidi ya kwenda motoni maana utaoneka huna akili kabisa, ulichezea zawadi ya uhai uliopewa bila kutumia akili.
Labda mwenyezi Mungu alikupangia jambo tofauti kabisa katika maisha yako halafu wewe ukajiingiza kwenye Bwawa la Mamba eti unapambana nao na huu mwili wa nyama bile silaha wala protective gear.
Wapo maelfu ya watu ambao hawakubaliani na mambo ya watawala but they are very very smart and carefully when they deal with situation na wanafanikiwa.
Ukitaka kuleta mabadiriko ya kweli jichanganye nao, tafuta opportunity unayotaka, au ingia kwenye decision chain then utafanya kiurahisi sana. Sio haraka haraka wasije wakakushtukia bali hatua kwa hatua.
Hata mazuri tuliyonayo sasa yawe machache au mengi yamefanywa na watu walioamua kupambana wakiwa ndani na si nje.