Uandaaji wa filamu ya Royal Tour tumepigwa lakini uzinduzi wake tunapigwa zaidi!

Kanumba angekuwepo kwenye filamu ingependeza sn na ingekuwa kali zaidi
 
Sijui viongozi wetu wanawaza nini lakini kwa kifupi ama wamepotoka au wanapotoshwa. Filamu ya aina ya Royal Tour si ya kwanza kuandaliwa duniani, ndugu zetu wa Rwanda walikwisha iandaa na imekwisha tazamwa sana. Sasa sijui kama viongozi wetu walikwisha fanya research ndogo tu kuona imeinufaishaje Rwanda. Manufaa ambayo kama Rwanda imepata basi yasingeweza kuwa siri ya ndani ya Rwanda bali pia spill over tungezipata hapa Tanzania au nchi nyingine za jirani.

Kitu cha kuzingatia ni kuwa wazo la kuandaa filamu hizi si la kwetu bali la hao wenye kumiliki uchumi lakini gharama ni za kwetu. Siyo siri katika kujenga uchumi wa nchi hakuna rafiki bali mwenye nguvu ndiye hushinda na kufaidi. Akili mu kichwa! Walio andaa wamefanikisha malengo yao bila jasho na kwa gharama nafuu.

Uzinduzi wa Royal Tour umekuwa balaa zaidi kwa hazina ya nchi! Rais wa nchi akiwa na wapambe wapatao 50 wamekaa zaidi ya wiki mbili nchini Marekani kufanya uzinduzi wa filamu hii kwa gharama za Watanzania walipa kodi. Wamarekani wamenufaika kwa kutembelewa na watalii kutoka Tanzania. Big brain amenufaika!

Kama hiyo haitoshi sasa uzinduzi utafanyika tena Tanzania kwa kodi zetu. Uzinduzi utafanyika Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam. Tena washiriki watakuwa wengi zaidi! Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma! Tumepigwa!

Tujisahihishe!
si wamesema serikali aijatoa hela bali hela zimetolewa na wafanya biashara
 
Ulitaka waseme nini baada ya kusikia kelele za wananchi wakilaani Rais wa nchi kuwa nje ya nchi yake kwa zaidi ya wiki mbili akitumbua fedha za umma bila shughuli ya maana kwa Taifa!
 
Ulitaka waseme nini baada ya kusikia kelele za wananchi wakilaani Rais wa nchi kuwa nje ya nchi yake kwa zaidi ya wiki mbili akitumbua fedha za umma!
hii noma sana inabidi wajitathimini
 
Sijui viongozi wetu wanawaza nini lakini kwa kifupi ama wamepotoka au wanapotoshwa. Filamu ya aina ya Royal Tour si ya kwanza kuandaliwa duniani, ndugu zetu wa Rwanda walikwisha iandaa na imekwisha tazamwa sana. Sasa sijui kama viongozi wetu walikwisha fanya research ndogo tu kuona imeinufaishaje Rwanda. Manufaa ambayo kama Rwanda imepata basi yasingeweza kuwa siri ya ndani ya Rwanda bali pia spill over tungezipata hapa Tanzania au nchi nyingine za jirani.

Kitu cha kuzingatia ni kuwa wazo la kuandaa filamu hizi si la kwetu bali la hao wenye kumiliki uchumi lakini gharama ni za kwetu. Siyo siri katika kujenga uchumi wa nchi hakuna rafiki bali mwenye nguvu ndiye hushinda na kufaidi. Akili mu kichwa! Walio andaa wamefanikisha malengo yao bila jasho na kwa gharama nafuu.

Uzinduzi wa Royal Tour umekuwa balaa zaidi kwa hazina ya nchi! Rais wa nchi akiwa na wapambe wapatao 50 wamekaa zaidi ya wiki mbili nchini Marekani kufanya uzinduzi wa filamu hii kwa gharama za Watanzania walipa kodi. Wamarekani wamenufaika kwa kutembelewa na watalii kutoka Tanzania. Big brain amenufaika!

Kama hiyo haitoshi sasa uzinduzi utafanyika tena Tanzania kwa kodi zetu. Uzinduzi utafanyika Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam. Tena washiriki watakuwa wengi zaidi! Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma! Tumepigwa!

Tujisahihishe!
Anaumwaga mwingi
 
Kwanza hongera sana umejitahidi kutoa ufafanuzi wako kwenye filamu ya Royal Tour, lakini niseme tu andika lako limejaa hisia sana (subjective) kuliko kuunda hoja zenye mashiko (objective) ili kubainisha uzito na ukweli wa hoja zako.

Kwanza kabisa: Hadi uamuzi wa kurusha Royal Tour kufikiwa kufanyika Amazon, watu wanatazama data, Amazon mwaka 2021 ilikuwa na Subcribers 200 milioni duniani zote, ambapo siku nne zilizopita Netflix wana watumiaji 221 milion, unaweza kuona kuona tofauti ni ndogo tu.

Hata hivyo, watu wanahama kutoka kwenye traditional media kama Televisheni kuhamia kwenye matumizi ya internet, hivyo kuiweka Amazoni ni rahisi zaidi watu kutazama kupitia simu janja kuliko National Georaphic and Animal Planet kama unavyosema.

Pili: Rais Samia ni maarufu zaidi unavyodhani, hata hivyo, Royal Tour kuja Tanzania ni kwa sababu ya Rais Samia Suluhu. Unadhani kama angekuwa Magufuli Peter Greeneberg angekuja?

Umaarufu wa Rais Samia Suluhu kwanza umeletwa na umaarufu wa Tanzania wakati wa Hayati Magufuli, dunia ilifuatilia hasa siasa za Tanzania na hata Magufuli alipofariki Tanzania ikawa maarufu zaidi na hata Rais aliyefuata akawa maarufu maradufu kwani ni mara ya kwanza, kwa Tanzania kuwa na Rais wa kwanza mwanamke.

Rais Samia Suluhu amekuwa maarufu baada ya kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa 2021. Rais Samia pia ameingia katika rekodi ya wanawake 100 wenye ushawishi Duniani 2021 katika Jariba la Forbes.

Rais Samia hakuwa na ulazima wa kushika kila taarifa, lengo la filamu ni kuonesha zaidi mandhari na uzuri wa nchi. Rais ni tour guide kwenye ile movie, na kumtumia Rais kuwa tour guide ni kichochoe tu watu wengi duniani wafuatilie, ila sio kutegemea Rais awe packed na kila taarifa ya Mbuga na mnyama, ingeboa. Ndio maana, filamu ilikuwa na shots kali mwanzo mwisho, na most of time, Peter aliingiza sauti mwenyewe.

Peter Greenberg hajaanza na Rwanda kama unavyosema, soma hapa; "He also produces and hosts a television series called The Royal Tour which airs on PBS. The series features various heads of state giving Greenberg and viewers a personal tour of their country. It has featured a number of world leaders including New Zealand's Helen Clark, Israel's Benjamin Netanyahu, Abdullah II of Jordan, Peru's Alejandro Toledo, Mexico's Felipe Calderón, Rwanda's Paul Kagame, Poland's Mateusz Morawiecki and Tanzania's Samia Suluhu Hassan. Greenberg was previously the Travel Channel's chief correspondent."

Filamu ya Royal Tour tayari kabla ya kutoka, ilishavuta watalii wengi, zaidi ya 600 kutoka Israeli, zaidi ya 200 kutoka France na nchi nyingine za Ulaya.
Ulipimaje hao watalii 600 toka France kabla haijatoka
 
MaCHADEMA again. Achaneni na Royal Tour. Tangu mwanzo mlishajitoa
 
Leo wakuu wote na magwanda yao wapo mjengoni wanacheki mchupa.
 
Hujaiona hiyo mikataba ya trl 11 ya akina rostam? Au ulitegemea uone vibabu vikiota jua seronera
Nikueleze tu hata mikataba ya Richmond mawaziri walienda Marekani kwa mbwembwe zote na kuahidi umeme kukatika itakua historia ila tukapigwa kitu kizito
 
Ah! Kumbe ni wewe, ningeshangaa kama angekuwa mtu mwenye akili timamu!

Mbona unaswaga za akina juma lokole? Akili zangu timamu ndo maana naweza kukuonesha pumba unazoandika hapa
 
Tumepigwa! Tumepigwa sisi! Tumepigwa sana!
pesa zilizolipwa kwenye bargain za wliobambakiziwa kesi za uhunumu uchumi na magufuli zimekwenda wapi mbona hazionekani hiyo ndio mada ya kuizungumza.
 
Bila shaka utafanywa wewe!
Wewe unangoja nini, wenzako tumeziona fursa na tunazitumia kweli kweli, hujamuona Rostam yuko USA na mama? Hujamuona mkurugenzi wa Bakhresa kijana mdgo kabisa, Salim Aziz yupo USA na mama wanaziwahi fursa?
 
Sijui viongozi wetu wanawaza nini lakini kwa kifupi ama wamepotoka au wanapotoshwa. Filamu ya aina ya Royal Tour si ya kwanza kuandaliwa duniani, ndugu zetu wa Rwanda walikwisha iandaa na imekwisha tazamwa sana. Sasa sijui kama viongozi wetu walikwisha fanya research ndogo tu kuona imeinufaishaje Rwanda. Manufaa ambayo kama Rwanda imepata basi yasingeweza kuwa siri ya ndani ya Rwanda bali pia spill over tungezipata hapa Tanzania au nchi nyingine za jirani.

Kitu cha kuzingatia ni kuwa wazo la kuandaa filamu hizi si la kwetu bali la hao wenye kumiliki uchumi lakini gharama ni za kwetu. Siyo siri katika kujenga uchumi wa nchi hakuna rafiki bali mwenye nguvu ndiye hushinda na kufaidi. Akili mu kichwa! Walio andaa wamefanikisha malengo yao bila jasho na kwa gharama nafuu.

Uzinduzi wa Royal Tour umekuwa balaa zaidi kwa hazina ya nchi! Rais wa nchi akiwa na wapambe wapatao 50 wamekaa zaidi ya wiki mbili nchini Marekani kufanya uzinduzi wa filamu hii kwa gharama za Watanzania walipa kodi. Wamarekani wamenufaika kwa kutembelewa na watalii kutoka Tanzania. Big brain amenufaika!

Kama hiyo haitoshi sasa uzinduzi utafanyika tena Tanzania kwa kodi zetu. Uzinduzi utafanyika Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam. Tena washiriki watakuwa wengi zaidi! Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma! Tumepigwa!

Tujisahihishe!
Sssa unataka tufanye nini kwani tumeanza kupigwa leo?nikipi kimewahi kufanyika kikaleta manufaa kwa wananchi?
 
Back
Top Bottom