Tetesi: Ubaguzi wa ajira kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

INAWEZEKANA MIMI NIKAWA MTOTO MDOGO SANA LAKINI TWENDE KWA HOJA TAFUTA KITABU CHA SHEIKH JUMBE KIITWACHO The Partner-ship: Tanganyika-Zanzibar Union 30 Turbulent Years. Kuhusu Maalim kutajwa kwenye kitabu hicho ni kweli hakutajwa lakini kwenye kadhia hiyo mwisho wa siku aliyenufaika alikuwa ni Maalim Seif na kwa bahati mbaya alipoomba nafasi ya urais, mwalimu alimwambia kuwa alikuwa badao hajaiva [kama vile alivyomwambia JK wakati wa kinyang'anyiro cha kumrithi mzee mwinyi. Tatizo la Maalim ni kwamba alikuwa na pupa mno na alifanya wajumbe wa zanzibar ambao kwa kawaida hupiga kura za 'block voting' kumkataa na kumpendelea mzee Iddris.
 
Ubaguzi ubaguzi tu. Ndio nawaambia muanze kujisafisha ili kitu ubaguzi lisiwepo kabisa.

Umeandika tetesi unaamanisha nini?

Na usipotaka kubaguliwa na wewe usiwe mbaguzi.

Weye ni mbaguzi. Na ndomana ukawa naroho ya chuki.
 

Kitabu mbona ninacho zamani sana !!!Tatizo sio maalim , tatizo Lilianza tokea 1964 pale wale waliokaribishwa na serikali iliyokuwepo na Kwa kuwasaidia ndugu zetu maisha ,wakatugeuka wakamwona Laanatullahi Nyerere ndiye MTU , wakaenda kushirikiana naye na wakaja kuuwa watu Kwa maalfu. Makosa hayohayo mnayarudiaa Kwa hizi fitna unazotumiwa hapa na hao waliokubali kuwaomba wavamizi walete majeshi kuja kupindua matakwa ya Wazanzibari Kwa kuufuta uchaguzi
 
Mtihani mwengine ukisema ujaribu upande wa sekta binafsi huko unakuta kama si mtanganyika utapata shida kupindukia .Maofisa ajira maana ndo wanatoka huko tanganyika.Basi wapemba imekua hawana option zaidi ya kuumia na hawajui wafanyeje.Ukweli GSO ipo na lengo lake mahsusi ni kuhakikisha mtu mwenye nasabu ya Pemba hatoboi wala mwenye kushabihiana na wapinzani iwe rafiki yako au jamaa yako.
Nashukuru sana leo umelisemea ila hili linahitaji nguvu kubwa sana kukemewa.Bahati mbaya sana hatuna watetezi.Ni muda sasa kueka siasa pembeni maana inaonekana inatuasithiri mno
 
Mwaka wa 1964 Maalim alikuwa wapi? nani aliyemdhamini kwenye UDSM? Jee alivyorudi masomoni alikosa kazi kwa vile yeye ni mpemba????? Kwa bahati nzuri baada ya mapinduzi marehemu Karume aliwahamasisha wapemba na waunguja kuoana na wengi walifanya hivyo sasa huo ubaguzi ulitokea wapi????? Kuhusu usaliti kwa Jumbe hiyo siyo siri na mara kadhaa yeye mwenyewe amekuwa akikana lakini ukweli unajulikana kuwa yeye ndiye aliyefanya mambo ya Ujuda wa eskariot na mwisho wa siku dhambi yake haishi kutafuna na ukweli ndiyo huo inawezekana usikubaliane name lakini mwisho wa siku utajulikana tuu.
 
Nyinyi ni katika hao wanaoitwa GSO muna chu
Na hii ndio dhihaka yenu kwa wapemba.Pemba hakuna serikali lazima ufahamu.Serikali kuu ipo Unguja na ndio wenye kuamua nani tumuajiri.Na mara nyingi watu wa unguja hawapendi kuajiriwa pemba ila kama wanataka serikali hii haijashindwa kabisa kuwapeleka kule na hakuna hata mtu mmoja atakae wazuia.Na ukweli wanaotaka wanapelekwa mbona.
 

Wewe ulikuwa ukiishi naye Maalim mwaka 1964 ???

Tizama unavyodanganya , Karume eti alihamasisha watu waoe , Hivi wewe ni muislamu au huna dini ???

Yaani watu wamekwenda kwa mzee wa kiarabu usiku wa manane na maaskari wenye bunduki na kumlazimisha mzee amtoe binti yake aolewe kwa mtutu wa bunduki ndio unaita hamasa alizohimiza Karume??? ,

Hivi wewe unajua watu walianza kuoana baina ya makabila zamani sana.

Huyo mfalme unajua ni kizazi cha nani ???

huyo karume na mke wake wa mwanzo walioana baada uvamizi ??

Usaliti wa Jumbe ni fitna hiyo , Maalim hakuwa secretary wa Jumbe , wala Jumbe asingalishindwa kusema kuwa kasalitiwa na Maalim.

Usijifanye wewe ni msemaji wa Jumbe , hao waliomwandikia hicho kitabu Partnership na ambao walikuwa hawaondoki kwa huyo Jumbe mimi nawasiliana nao mara nyingi na sijawasikia hata siku moja kusema fitna hizi unazotuletea .

Nyinyi mlioivuruga nchi na kuuwa watu bado mngali mnashirikiana na wavamizi kuvuruga demokrasia Zanzibar kwa visingizio vya Maalim,

Kama watu wanamwona Maalim ni msaliti wasingalimpa kura , au nyinyi mnaumia zaidi kuliko Maelfu ya waliompa kura zao ???

Kwa nini mnashirikiana na wavamizi wa kikatoliki kuufuta uchaguzi ???
 
Huwezi kuadhibu kwa dhambi mwengine.
 
Nimeshaeleza ubaguzi wao humu na sio mimi tu wapo wengi wamechangia. Jaribu kuperuz


Mbona sisi wengine tulioa huko Pemba hata kabla mapinduzi na hatujafanyiwa ubaguzi wowote ???

Mbona vijana wengi wameondoka kwa kubaguliwa baada ya kukoseshwa masomo kwa sababu ya kabila zao ?? Haya yametokea baada ya mavamizi.

watoto wangu waliozaliwa Pemba , ili wapate elimu ya juu imebidi tuwabadilishe vyeti , tuandike wametoka Unguja , haya ni ni hivi karibuni kwani wenzao wamekoseshwa nafasi za masomo waliokuwa na vyeti vya kuzaliwa vya pemba

Hamwoni kuwa mnafuata sera ya kanisa katoliki ???
 
Nadhani niliandika kuwa kwenye kile kitabu cha marehemu hakuwahi kumtaja Maalim ila baada ile kadhia ya Dodoma ambapo iliishia kwa marehemu Jumbe kujiuzulu, Maalim ndiye aliye kuwa mnufaika mkuu baada ya kadhia hiyo.
Pengine ungejaribu kuwauliza viongozi toka zanzibar ambao walikuwepo kwenye vikao hivyo na bado wako hai watakwambia ukweli.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huwezi kuadhibu kwa dhambi mwengine.
Lakini rais wa Zanzibar ni mwenyeji wa Pemba. Nadhani hii taarifa chanzo chake sio cha uhakika, ni tetesi tu.
Unaujua mchakato wa urais Zanzibar unakwendaje????Basi kama hujui Raisi wa Zanzibar hupatikana Dodoma na CCM wa Zanzibar hata wamkatae huku kwao ila Dodoma ndio wanaompitisha so hicho si kigezo.
 
KUMBE WEWE NI MPEMBA ATI!
SASA NIMEKUELEWA KWANI NINAFAHAMU PIGA UA MSIMAMO NI HUO. NAKUTAKIA KILA LA KHERI NA MUNGU AJAALIE MAALIM SEIF SHARRIF AWE RAIS AJAE WA ZANZIBAR KWENYE UCHAGUZI UJAO.
 



Nimuulize nani na mimi nilikuwepo tokea Mapinduzi na tumo tunateseka ???? Unataka nikawaulize hawa waliomwomba mvamizi kuleta jeshi lililomlazimisha Jecha kufuta uchaguzi ???

Hivi Wazanzibari waliomchagua Maalim ni wapumbavu na vipofu wa kujua nini kilitendeka wakati ule ???hawa vibaraka wachache wanaoiangamiza nchi ndio unawaona ndio wajuzi wa kila kitu ???
 
KUMBE WEWE NI MPEMBA ATI!
SASA NIMEKUELEWA KWANI NINAFAHAMU PIGA UA MSIMAMO NI HUO. NAKUTAKIA KILA LA KHERI NA MUNGU AJAALIE MAALIM SEIF SHARRIF AWE RAIS AJAE WA ZANZIBAR KWENYE UCHAGUZI UJAO.


Hata huyo Jumbe wako ni Mpemba , Ali karume ni mpemba , Moyo ni mpemba maana wote wameoa Pemba
 
Hata huyo Jumbe wako ni Mpemba , Ali karume ni mpemba , Moyo ni mpemba maana wote wameoa Pemba
Sasa unacholalamika ni kitu gani? Nenda kwenye archive ya TVZ utakuta video ambayo inaomuenyesha marehemu Karume akihamasisha umoja na kutaka watu wa visiwa hivyo waendelee kuoana na ukitatuta takwimu utakuta viongozi wengi wa mwanzo wa SMZ waliitikia wito huo.
Hii ni kuthibitisha kuwa baada ya mapinduzi hakukuwa na ubaguzi wa upemba na uunguja ila mbegu hii ililetwa na the 'young turks' ambao walisomeshwa na SMZ.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…