Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Tumekua tukisikia kwamba mkuu wa nchi ni mbaguzi hasa linapo kuja swala la mitazamo ya kisiasa kitu ambacho si kuzuri na hakifai kwa mkuu wa nchi.

Tofauti na viongozi wenyine hata marais waliopita, Mh hapa amefeli na inaonyesha anafanya makusidi.

Jana akiwa msoga diwani wa hilo eneo aliitwa atoe kero, Mh akadhani ni diwani toka chama cha chadema kwa sababu hakuvaa sare ya ccm, akaamuru anyang'anywe mic na maneno makali juu lakini baada ya kuuliza chama gani akaambiwa ni wa ccm, mara moja akaamuru arudishiwe mic na aendelee kuongea.

Leo tarehe 29 June 2020 akiwa kilosa akaanza kumponda mbunge wa eneo na kusema wananchi wa eneo hilo wanachagua kwa jazba akiamini mbunge wa eneo hilo ni qa chadema. Anaongeza kwa kusema yeye angekua mbunge wa eneo hilo angekua amemaliza changamoto zote ila kwa sababu wananchi wanachagua kwa jazba na wanachagua wabunge sio ndio maana bado changamoto zipo.

Baadae akauliza mbunge wa hapo anaitwa nani na wa chama gani? Wananchi wakamtaja na kumwambia anatoka chama chamapinduzi.. Bila hata aibu akaanza kumsifia na kuahidi kuzimaliza changamoto hizo akisadiwa na waziri husika.

Wananchi wa Tanzania sio watoto wanajua na wanaelewa vizuri, wao wanapendana bola kujali vyama, dini wala kabila lakini bado kuna viongozi karne hii wanasimamia ubaguzi.

Naamini mh Rais ana nia njema na Tanzania, lakini bado ana nafasi ya kuondoa hurka hii ya ubaguzi hata kama chadema walimpa wakati mgumu 2015.

Rais ndio kiungo pekee cha kuwaunganisha watanzania .

Sio sababu ya yeye kuendelea kubagua vyama vya upinzani hali kazi zake alizo zifanya zinaonekana.

Haya mambo madogodogo yanamuondolea kitu fulani kama kiongozi.

Tuungane kuuoinga ubaguzi.



Prof Jay
Rais Magufuli hana nia njema na Tanzania ila ana nia njema na barabara tu
 
Kosa la Magufuli ni kufanya hata Yale ambayo watu wangali wakifikiri kuwa Kwa hilii!!! Hatoweza kulifanya

Ikitokea amelifanya, watu wa Aina hiyo, hulazimika humtafutizia makosa ya kulazimisha, ili tu naye angalau aonekane anafanya makosa!

Kwa kuwa naye ni Binadamu! Hawezi kuishi bila kukosea, hiyo ni huluka yetu binadamu, na hata mleta mada naye hukosea!!

Lakini Kwa ujumla wake, Makosa ya Magufuli ni kazi zake na si vinginevyo
Anafanya ubaguzi kwa makusudi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
hiyo ya kunyang’anyana mic waliodhaniwa wapinzani mbona iko wazi tu wakati huu wa kuelekea uchaguzi si kitu kizuri kuwapa wapinzani nafasi ya kupata kiki kupitia kuongea katika mikutano ya Rais.

Mkulu yuko sahihi asilimia mia mbili huu ni wakati wa kusherehekea na kutangaza ahadi zilizotekelezwa si kuuliza uliza maswali ya kuudhi!!
Huna akili
 
Mie naona upumbavu na utoto tu unaendelea. Kwa nini viongozi wanakuwa wanaongea utafikiri viranja wa shule ya msingi?
 
Ila hapo aliponyang'anywa mic si kwasababu alimuadentify kama ni diwani wa chama gani bali ni kwasababu huyo mzee anazunguka sana kujielezea.....

Raisi amekuja kwa ziara ya kushtukiza yeye anaanza kutoa salamu kwa ndugu na jamaa badala ya kwenda straight kwenye point iliyomleta anazunguka na kuleta mambo ya chama cha mapinduzi.....

Nyoosha maelezo, NASHUKURU MHESHIMIWA AND RAIS. CHANGAMOTO ZA WANANCHI ENEO LETU NI MOJA MBILI TATU, SISI KAMA VIONGOZI TUMEFANYA MOJA MBILI TATU KUKABIRIANA NA CHANGAMOTO HIZO NA TUMEKWAMIA HAPA.....


Sasa yeye anaanza, magufuri hoyeeeeeee kwann asishushuriwe....
Kwahiyo rais ni mshushuaji .?
 
Hii ndio unaiba nguo usiku kwenye kamba ,kuja ndani unakuta ulizo iba ni nguo zako na sio za jirani.
Kweli mkuu mimi huwa sipendi kufatilia siasa lakini ulichokizungumza ni kweli leo TBC aliaanza kumponda sana mbunge wa hapo akijua ni wachama cha upinzani. Baada ya kuambiwa anatokea ccm ikabidi aanze kumsifia bila hata aibu
 
Na leo eti anasema anasmhukuru lijuakali yupo, japo wakati wabunge wa ccm wanaongea wananchi walikua kimya.. ila aliposimama mbunge wa mikumi bwana haule toka chadema hadi wananchi wamesimama kumchangilia na akaongea point tupu.
Upinzani kuna vichwa huwezi linganisha na utopolo wa ccm! Yeye mwenyewe kajionea!
 
Kila kona ya nchi Dkt Magufuli anahitajika akahutubie, kila anapopita watu nyomi

Watu nyomi ni jambo nadra nchi hii? Kama watu wanaweza kusimama na kuangalia bulldozer likichimba barabara, tena wakiwa wamejazana, ndio itakuwa kwenye ziara ya rais ambazo kuna vikundi vya burudani kabisa? Hujawahi kuona watu wamejazana wakiangalia show za promotion za bidhaa mbalimbali? Sasa kipi kinakushangaza watu kujazana kwenye hafla zenye burudani, tena huko mikoani?
 
Back
Top Bottom