Katika sehemu ya mashariki ya mji wa Detroit nchini Marekani, kupitia picha za satelaiti, tunaweza kuona ukuta unaotoka kaskazini hadi kusini na kupitia mitaa minne, ambapo umetenganisha sehemu ya watu weupe na sehemu ya watu weusi. Katika nchi hii ambayo siku zote inadai kutetea haki na usawa, kuna dunia mbili tofauti, dunia tajiri ya Wamarekani weupe, na dunia maskini ya Wamarekani Weusi. Wachambuzi wa Marekani wanasema chanzo cha umaskini wa Wamarekani wenye asili ya Afrika ndio ubaguzi wa rangi.Ripoti ya kila mwaka kuhusu hali ya haki za binadamu ya Wamarekani wenye asili ya Afrika iliyotolewa hivi karibuni na Shirikisho la Miji la Marekani ilieleza kwamba, Wamarekani wenye asili ya Afrika wana “asilimia 73.9 tu ya fursa za wazungu”, na hawana haki sawa na watu weupe katika kupata utajiri, afya, elimu na mambo ya kisiasa. Data za uchunguzi kuhusu hali ya kifedha ya wateja nchini Marekani zinaonyesha kuwa, wastani wa mali za familia ya Wamarekani weupe ni mara nane kuliko familia ya Wamarekani weusi. Wastani wa mali za familia ya watu weupe ni dola 983,400 za kimarekani, huku wastani wa mali za familia ya watu weusi ukiwa dola 142,500 tu za kimarekani.
Suala la ardhi ni chanzo kingine muhimu cha umaskini wa Wamarekani wenye asili ya Afrika. Ripoti iliyotolewa tarehe 3 Mei na Shirika la Habari la Uingereza Reuters inasema, wakulima wenye asili ya Afrika nchini Marekani walipoteza takriban ardhi zenye thamani ya dola bilioni 326 za kimarekani katika karne ya 20 kutokana na sera za ubaguzi wa rangi. Kuanzia mwaka 1922 hadi 1997, mashamba ya kilimo ya wakulima weusi katika majimbo 17 nchini Marekani yalipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na “vitendo vya kimabavu vilivyoungwa mkono na serikali”, pamoja na sera ya ubaguzi wa rangi ya mikopo na hatua ya kuwalazimisha watu weusi kuuza mashamba yao.
Takwimu za Sensa iliyofanywa na Wizara ya Kilimo ya Marekani zinaonesha kuwa, mwaka 1910, wakulima wenye asili ya Afrika nchini humo walikuwa wanamiliki mashamba zaidi ya ekari milioni 16, ikiwa ni asilimia 14 ya mashamba yote ya kilimo nchini Marekani. Lakini hadi kufikia mwaka 2017, wakulima weusi walikuwa wanamiliki mashamba ekari milioni 4.7 tu. Hivi leo ni asilimia 1 tu ya watu weusi wanaomiliki mashamba nchini Marekani, ambao wanamiliki asilimia 0.1 tu ya mashamba ya kilimo ya nchi hiyo.
Ubaguzi wa rangi ulioendelea kwa miaka mingi nchini Marekani umesababisha ukosefu wa haki katika nyanja mbalimbali na kuchangia umaskini wa Wamarekani wenye asili ya Afrika. Marekani siku zote inajidai ni mlinzi wa usawa na haki duniani, lakini kama haiwezi kuondoa ubaguzi wa rangi kwenye nchi yake yenyewe, haitaaminiwa na jumuiya ya kimataifa.