Watanzania asilimia kubwa kwa umbea, majungu na roho mbaya ndio kwao!! Miaka mitatu ya nyuma nilifanikiwa kuanzisha mradi fulani ambao ulinilazimu kuanza na watumishi kama ishirini, kati ya hao, tisa walikuwa wana elimu ya chuo kikuu,pamoja na kujitahidi kuingia gharama kubwa za kutengeneza mazingira mazuri ya kazi ili kuleta ufanisi wa kazi,naweza kusema sikujua kama nimefanya kosa kubwa!!
Kazi zilikuwa hazifanyiki ni uvivu, majungu, wizi, kukosa heshima kwa wateja, kudharau wateja na kujifanya wakubwa, matumizi mabaya ya rasilimali za ofisi!! Kiukweli kichwa kiliniuma Sana, nilikuwa simalizi masaa mawili bila kupokea simu za wafanyakazi!!wanakupigia kushitakiana tu, wengine wanakusalimia tu hana la maana, wengine kujifanya wema kumbe majizi!!
Mama yangu mdogo alinipeleka kwa rafiki yake ambae ni muhindi ana mradi kama wangu, kwa lengo la kujifunza!! Niligundua kuwa ili mradi wako ufanikiwe usicheke na kima!! Uwe na roho ngumu hasa!! Toka kipindi icho nilibadilika nilifukuza wafanyakazi wengi, nikaleta vijana saba tu kutoka Uganda!! Hakika hapo ndio nilianza kuona utendaji ulio nyooka,mauzo yakapanda kwa kiwango kizuri, simu za usumbufu za wafanyakazi zikaisha!! Waganda wanapiga kazi uwezi kukuta wanabishana asubuhi masuala ya mipira na uzinzi!! Mtanzania anataka alipwe pesa nyingi wakati anacho deliver ni zero!!! Yaani ili afanye kazi vizuri mpaka uweke sheria kali kama za jela!! Kwangu simlaumu MO, maana hata mimi niliona bila kuwa mafia wabongo wanakufilisi uku unajiona na wanabaki wakikucheka!!!