Ubalozi wa Marekani: Mbowe ameshambuliwa kikatili, wakumbushia pia shambulio la Tundu Lissu huku kukiwa hakuna hatua zilizochukuliwa

Ubalozi wa Marekani: Mbowe ameshambuliwa kikatili, wakumbushia pia shambulio la Tundu Lissu huku kukiwa hakuna hatua zilizochukuliwa

Sifurahishwi na mtu yeyote kuvamiwa au kuvamia mwenzake, ila haijathibika kuwa ikiwa ni kweli kavamiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe si umeamua kumuamini yule mgonjwa aliyesema Mbowe alikua amelewa chakari, sisi wengine tumeamua kuamini taarifa za kuvamiwa kwake na wahuni wa chama cha mashetani (CCM).
 
Wasalaam wanabodi,

Nimeona twit ya UBALOZI WA MAREKANI wakilaani au KUSIKITISHWA na kuvamiwa na kuumizwa kwa mbunge na kiongozi wa upinzani bungeni Mh Freeman Aikael Mbowe.

Kitu ambacho kimenishangaza ni kuwa UBALOZI huo umesema moja kwa moja kuwa mh Mbowe kashambuliwa ilhali taarifa za uchunguzi bado hazija toka na swala lenyewe bado lipo katika uchunguzi.

Je, wao wamepata wapi uhakika kuwa mh Mbowe kavamiwa? Je ni sawa kwao kutoa taarifa kabla vyombo vinavyohusika kutoa taarifa?

Kwa kuwa kumekuwa na conspiracy nyingi tu juu ya tukio hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
taarifa ya kushutiwa Tundu Lissu haijatoka hadi leo ndiyo maana!
 
Mpaka kesho bado tunasubiri ripoti dhidi ya shambulizi la lissu, halafu nyumbu mmoja anakuja kuwaonya ubalozi wa USA wasiseme chochote mpaka polisi watoe ripoti
 
But don't trust so easily, unahakika gani ni CCM wamefanya hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uhakika unatokana na ukweli kua CCM ndio yule abilisi anayetajwa kwenye Biblia kwamba kazi yake ni kuua, kuiba na kuharibu hivyo uuaji wowote kama ilivyotokea kwa Alphonce mawazo, uizi wowote kama ilivyotokea kwenye Escrow account na uharibifu wowote kama ilivyotokea kwenye kuharibu mipango ya kutengeneza bandari yenye hadhi ya kimataifa kule Bagamayo, mhusika lazima awe shetani ambaye hapa kwetu ni CCM!
 
Nami nimeshangaa pia.Wanafanya mambo kiajabu ajabu tu.
21st century Americans ni spoiled generation tu. True Americans washapita.Eti make America great again! Ndo imetoka hiyo!
 
Uhakika unatokana na ukweli kua CCM ndio yule abilisi anayetajwa kwenye Biblia kwamba kazi yake ni kuua, kuiba na kuharibu hivyo uuaji wowote kama ilivyotokea kwa Alphonce mawazo, uizi wowote kama ilivyotokea kwenye Escrow account na uharibifu wowote kama ilivyotokea kwenye kuharibu mipango ya kutengeneza bandari yenye hadhi ya kimataifa kule Bagamayo, mhusika lazima awe shetani ambaye hapa kwetu ni CCM!
Duu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee mie nimeshangazwa tu na yule mbowe wa huko kwao vile walimkandamiza mpaka akadanja,Hilo la mbowe wa huku halijanistua kabisa.
 
Nimeona ya UK na EU pia wametoa. Why ya Marekani pekee ikushangaze?
 
Back
Top Bottom