Ubalozi wa Marekani wamkumbuka Mwl. Nyerere. Wasema "maendeleo ni watu sio vitu"

Ukweli wa kauli ya Nyerere ni huu sio tafsiri mnazo taka nyinyi

Hapo Nyerere anasema kuwa maendeleo yanatakiwa kuambatana na uhuru pamoja na democrasia.Tanzania huo uhuru pamoja na democrasia havipo kwa sababu:

1.Zimetungwa sheria kadha wa kadha wakati huu wa Magufuli kukandamiza vyombo vya habari(Kila mtu analijua hili)

2.Zimetungwa sheria kadhaa kugandamiza uhuru wa social media.Watu kadhaa wameshtakiwa na kufungwa kisa kumkosoa Magufuli kwenye social media

3.Zimetungwa sheria kandamizi hadi kwenye kutumia line za simu(Ni mambo ya aibu)

4.Zimetungwa sheria kandamizi dhidi ya upinzani ikiwa ni pamoja na sheria za kuzuia wapinzani kuungana

5.Vyombo vya dola pamoja na tume vinaegemea wazi wazi upande wa CCM wakati huu wa uchaguzi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa

6.Zimetungwa sheria kandamizi na za ajabu kuwa rais,speaker,waziri mkuu hawaruhusiwi kushtakiwa wakifanya maovu

Ndiyo maana tunasema kuwa utawala wa Magufuli unahangaika na maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu kwa hiyo Magufuli anatakiwa kukaa pembeni apishe wanaojua kuongoza nchi kwa sababu yeye amekosa kibali cha wananchi.
 
Mambo kunoga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The first key point ni kwamba maendeleo yawe people centred in the context kwamba barabara n.k yaweze ku endeleza maendeleo vya watu iwe flyover, interchange, hospital, dispensary, shule n.k.
Yaani yamuwezeshe mtu kufanya biashara vizuri zaidi, kusafiri vizuri zaidi, huduma ya afya iwe bora zaidi ili aweze ukizalishe zaidi na kuishi Maisha marefu zaidi, elimu imsaidie kufanya shughuli za kimaisha na kiuchumi kwa ufanisi zaidi n.k n.k
Ukitoka hapo ndio unaenda kwenye uhuru wa watu, ambao tunao na la mwisho ndio kazungumzia demokrasia iwe ya chama kimoja sawa iwe Vyama vingi sawa?
Na aka pose kwa kusema kwamba Zaire au DRC one Vyama 140 , sasa hajui kama ndio demokrasia au sio ni juu yako kufanya hiyo analysis
 
Nimekuwekea msululu wa sheria za ajabu na aibu zilizotungwa chini ya utawala wa Magufuli kwa lengo la kugandamiza na kuua uhuru wa watu pamoja na democrasia na bado unasema kuwa uhuru tunao!Unajua kusoma?Umesoma nilichoandika?!
 
Fake mbona kwenye twitter account yao haipo! Naona mnahangaika kweli. Wakati Mbelgiji Lissu alitukana Baba wa Taifa Nyerere wakati wa Bunge la Katiba msifikiri tumesahau!
 
Nimekuwekea msululu wa sheria za ajabu na aibu zilizotungwa chini ya utawala wa Magufuli kwa lengo la kugandamiza na kuua uhuru wa watu pamoja na democrasia na bado unasema uhuru tunao!Unajua kusoma?Umesoma nilichoandika?!
Sheria za ajabu kwa nini wakati zimepitishwa na Wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi? Pia kumbuka uhuru wako unakoma pale uhuru wa mwenzako unapoanzia! Pia kumbuka uhuru na wajibu hakuna uhuru usio na mipaka. Ndiyo maana hata huko kwenu Chadema mmekubaliana kuwa Mbowe awe Mwenyekiti wa Maisha, pia ACT Wazalendo kuwa Kiongozi Mkuu wa Chama ni Zitto pekee ambaye ni mkuu kuliko Mwenyekiti Maalim Self.
 
Kuna hekima aliiyoa kiongozi Fulani kwamba; " Ukiona Nchi Maskini, jua Wananchi wake ndio maskini. Na ukiona Nchi tajiri, juwa wananchi wake ni tajiri."
Huu ndio ukweli, nchi tajiri kama U. S sio kwamba hakuna mafukara kule, bali namba ya matajiri ni kubwa kuliko maskini. Hata kwenye nchi maskini Sana,kuna watu matajiri wa kutupa ila huwa wachache. Tanzania nakupenda.
 
Na kwa vile leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali
 
Nimekuwekea msululu wa sheria za ajabu na aibu zilizotungwa chini ya utawala wa Magufuli kwa lengo la kugandamiza na kuua uhuru wa watu pamoja na democrasia na bado unasema kuwa uhuru tunao!Unajua kusoma?Umesoma nilichoandika?!
Sasa wewe na akili zako umeona needs zetu ni za wizara moja tu ya sheria? Ambayo unaweza kusema ni % ya huna needs may be 10% , hutaki kuongelea ya wizara ujenzi, uchukuzi,afya, biashara, ardhi, afya, elimu n.k , wewe umengangana na hiyo 10% ambayo ukiidadavua utabaki na 2% , wakati shida zako nyingi za kila siku zipo kwenye hii 90% iliyobaki
 
Kweli mimi ninamuenzi Nyerere kwa vitendo hivyo tarehe 28/10/2020 nitampa kura yangu Magufuli pia nakubaliana na wewe kuwa Rais Magufuli tumpe awamu mbili za miaka 10/10 Hivyo Rais Magufuli ataendelea mpaka mwaka 2035.
 
"Kila nilipokuwa nikitaka kung'atuka walikuwa wakiniambia: 'Mwalimu endelea tu, hii nchi ni changa na umeitoa mbali. Nchi hii haitaendelea bila wewe'. Nami niliendelea hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa waliyoiongelea ni familia zao."
Mwl. Julius Kambarage Nyerere
 
Unateka watu,unawaua watu,unawadhulumu watu haki zao ili kujenga miundo mbinu hayo ni upumbavu mtupu.
Hata ununue ndege 1000 flyover 50,000 ukaua watu 5,000 hayo si maendeleo
 
Wapi nimezungumzia wizara ya sheria?!Mimi sijazungumzia wizara ya sheria.Nimezungumzia jinsi uhuru pamoja na demokrasia zinavyobanwa chini ya uongozi dhalimu wa Magufuli kupitia sheria za hovyo na za aibu alizosimamia zitungwe.

Wewe ndiye ambae umenipa video ya Nyerere akizungumzia maana ya maendeleo ya watu.Nyerere kwenye video hiyo anasema maendeleo ya watu ni yale yanayoambatana na uhuru pamoja na democrasia ya watu.Sasa unakana tena video ambayo wewe mwenyewe ndiyo umenitumia?
 
Maendeleo yasikamue na kuleta udhia kwa wananchi,yalete auheni kwa watu.
 
Lakini mwalimu hakuwahi kuwadhulumu watumishi walio kazini na wastafu kwa kuwa alikuwa anajenga reli au kununua ndege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…