Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
Hapo Nyerere anasema kuwa maendeleo yanatakiwa kuambatana na uhuru pamoja na democrasia.Tanzania huo uhuru pamoja na democrasia havipo kwa sababu:Ukweli wa kauli ya Nyerere ni huu sio tafsiri mnazo taka nyinyi
1.Zimetungwa sheria kadha wa kadha wakati huu wa Magufuli kukandamiza vyombo vya habari(Kila mtu analijua hili)
2.Zimetungwa sheria kadhaa kugandamiza uhuru wa social media.Watu kadhaa wameshtakiwa na kufungwa kisa kumkosoa Magufuli kwenye social media
3.Zimetungwa sheria kandamizi hadi kwenye kutumia line za simu(Ni mambo ya aibu)
4.Zimetungwa sheria kandamizi dhidi ya upinzani ikiwa ni pamoja na sheria za kuzuia wapinzani kuungana
5.Vyombo vya dola pamoja na tume vinaegemea wazi wazi upande wa CCM wakati huu wa uchaguzi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa
6.Zimetungwa sheria kandamizi na za ajabu kuwa rais,speaker,waziri mkuu hawaruhusiwi kushtakiwa wakifanya maovu
Ndiyo maana tunasema kuwa utawala wa Magufuli unahangaika na maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu kwa hiyo Magufuli anatakiwa kukaa pembeni apishe wanaojua kuongoza nchi kwa sababu yeye amekosa kibali cha wananchi.