Ubalozi wa Marekani watoa tahadhari kusafiri kwenda Mtwara

Ametimiza majukumu yake kadiri ya job description yake.

Je, wa kwetu ametahadharisha kukanyaga sehemu fulani fulani za US kwa sababu za ubaguzi, COVID?
 
Mbona Serikali yetu haitoi tamko kuhusu hali ilivyo huko Mtwara?.
I doesn't matter kama serikali imetoa tamko au haikutoa tamko. Balozi za nchi za nje hawatowi tahadhari kwa wananchi wao kutegemea na tamko la serikali bali ni kutegemea na namna wanavyoona wao wenyewe kutokana na hali ilivyo sehemu fulani. Ndio maana kuna tahadhari ya kuingia tanzania kwa sababu ya corona ingawa serikali ya tanzania inasema nchi haina corona.

Kuna tahadhari ya kutembelea zanzibar kwa muda mrefu sasa kwa sababu za Islamic extremism, kuna tahadhari hiyo hiyo kwa mipaka ya tanzania na mozambique. Kumbuka hizi ni tahadhari tu sio kusema kuwa hizo sehemu ni hatari, infact tahadhari zao huwa na colour code red, amber na green.
 
Umesoma hata hilo tangazo lenyewe au unabwabwaja tu? Wametahadharisha raia wao kwenda Mtwara, wewe kama unaona panakufaa nenda.
Hata akisoma hiyo lugha ataielewa mkuu?? Yeye amedandia treni kwa mbele tuu baada ya kuona heading...
 
Imeandikwa kiingereza mkuu bila tafsiri. Nawasubiri wale wa HKL waje kutafsiri ili wote tuielewe taarifa.
 
Huku alikuja makamu wa rais Dkt. Samia acha upuuzi kuna amani huku wao walisema hata dar mwaka jana nini kilitokea sasa
 
Wananchi tupo wa aina mbalimbali. Unaweza kutoa tahadhari ukasababisha taharuki ya hali ya juu ambayo italeta madhara zaidi. Kuna watu ni bora wasijue nini kinaendelea maana wanaweza kuongeza na kusambaza ambayo hayapo ikawa hatari zaidi.
 
Ukisema hivi inamaana Serikali yetu isifanye lolote kuhusu hali ya usalama huko Mtwara
Wewe nakuomba msikilize Kamanda Siro ndiyo IGP wa Tanzania,huyo Balozi wa USA hapa Tz analindwa pia na Siro, au hujuwi!!
 
Mkuu umelisoma tangazo kweli? Hajakwambia wewe Mataga, ni tahadhali kwa raia wa Marekani so wewe endelea na mishe zako
Kama kweli hao wa Marekani wako wanaona Tanzania si salama kwao,washauri wafunge na huo Ubalozi wao Kama wanajeuri hiyo!!
 
Lack of information

Maisha ni kuwa na habari na taarifa kamili kwa wakati

Kama huna taarifa kaa kimya

Kama una taarifa isiyokamili lala
Kweli watu Weusi mmelogwa na Wazungu! Yaani Mimi Mweusi mwenzio niko Mtwara nakula life,eti huniamini,unamuamini yule Balozi anae ishi pale Drive inn Msasani,ambae hata Mtwara hajawai kufika!!
 
Kwenye hili naona, magufuli kawa mzembe.
Linapokuja suala la usalama wa mtanzania, siasa zikae pembeni.

Igp sirro ni Mpuuzi tu, mshenzi
Wwe Chase amante ndiyo mpuuzi na Mjinga no moja na huo Ubalozi wako wa Marekani,wote hamna akili! Hapo ulipo unatamba hadi unapata muda wa kuandika humu inamaana Nchi iko Salamaa shukuru Mungu hata kwa hilo!!
 
Umbea usio na Maana kabisa na unaingilia utawala wa ndani
 
Zile nguvu zitumikazo kuwashughulikia wapinzani zielekezwe mtwara. Maana ni mahiri Sana kuwapiga raia wasio hata na fimbo shame kabisa. Askari aliyeiva hawezi piga mtu asiye na silaha ili kumfurahisha mtawala.
 
Kama kweli hao wa Marekani wako wanaona Tanzania si salama kwao,washauri wafunge na huo Ubalozi wao Kama wanajeuri hiyo!!
Mkuu mbona unateseka kwa mambo yasiyo kuhusu? Wafunge wasifunge ni juu yao na wewe hilo halikuhusu, wao kuona ni salama au siyo salama hawakuambii wewe, so wewe subiri taarifa ya IGP wenu. Taarifa ya ubalozi wa Marekani siyo yako. Pathetic
 
Mkuu mbona unateseka kwa mambo yasiyo kuhusu? Wafunge wasifunge ni juu yao na wewe hilo halikuhusu, wao kuona ni salama au siyo salama hawakuambii wewe, so wewe subiri taarifa ya IGP wenu. Taarifa ya ubalozi wa Marekani siyo yako. Pathetic
Sasa huo Ubalozi wako wa Marekani ndiyo unalinda mipaka yetu!? Unaacha kuwasikiliza watu tuliowapa dhamana ya Kulinda Nchi hii,wwe akisema Mzungu tu umeshakubali haraka!

Si ndiyo hao walisema wanaleta Ndege kuchukua watu wao eti Tanzania kuna Corona!? Mbona bado wako hapa wanambwelambwela tu! Wamesha sahau Mambo ya Corona Sasa wako na Mambo ya Mtwara! Waulize vp tunaweza kwenda Tanga!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…