Ubalozi wakanusha habari za uongo zinazodai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo

Anayetakiwa kukanusha ni aliyetamka kauli, sasa huyu si mtetea ugali tu mama tulivyo sisi.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya vikao vya kamati ya Bunge na kikao cha Bunge la EU.

Ubalozi wa EU upo pale Umoja House tafuteni ukweli.
Ndugu, pengine hujui namna mchakato wa public policy making unavyokuwa. Ndio Tanzania (soma madudu ya Tanzania) umeingia mainstream ya EU policy-making. Ukweli ndio huo!
 
huyo balozi hana akili,badala ya kujibu hoja zilizowekwa yeye anajadili idadi ya watoa maamuzi
 
mkuu aliyejibu ni balozi wa Tz yaani mteule wa Magufuli huko Ubelgiji,sio mzunge
 
BALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI NA HUMPREY POLEPOLE WA CCM SIKILIZENI

HOJA hapa sio kukanusha kwamba; hizi sio habari za kweli kama Balozi anavyokanusha hapa online. Hoja za msingi hapa ni hizi hapa chini;-

Je, ni kweli Kamati ya Bunge la Ulaya imekutana kutujadili sisi Tanzania? Jibu ni kweli, imekutana kutujadili.

Je, Kamati hiyo imekutana kutujadili sisi Tanzania kuhusiana na masula gani? Jibu ni kuhusiana na mambo yafuatayo;-

Fedha za corona tulizochukua wakati Serikali ilitangaza hadharani kwamba; Tanzania hatuna corona tumeifukuza kwa maombi ya siku tatu.

Aidha, Kamati hiyo imetujadili kuhusiana na mazingira ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2020 maana EU imekuwa ikifadhiri fedha za kuboresha demokrasia na utawala bora hapa nchini.

Je, nini hatma ya mjadala huo uliofanyika jana?

Wajumbe zaidi ya 70 wa Kamati ya Bunge la Ulaya waliazimia kupeleka mapendekezo ya Kamati yao kwenye Bunge la Ulaya kuhusu mambo yafuatayo;-

Tanzania inyimwe misaada na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na nchi zote ambazo ni washirika wa umoja wa ulaya.


Serikali ya Tanzania ikiri kwa maandishi kwamba; itaratibu chaguzi zilizo za huru na haki sambamba na kuilinda Demokrasia iliyoporomoka kwa kiwango kikubwa sana.

Sisi watanzania tunasubiria kwa hamu sana vikao vya Bunge zima la Ulaya vianze ili Kamati ikawasilishe maazimio/mapendekezo yake mbele ya Bunge zima ili tupime ukweli ni upi.

Francis M. Garatwa,
Kada Mtiifu wa Chadema.
20 Novemba, 2020. Tanzania
 
Kwani huwa tunahitaji misaada ya bebereu?
 
mkuu aliyejibu ni balozi wa Tz yaani mteule wa Magufuli huko Ubelgiji,sio mzunge
walivyosema jana nilijua ni mzungu ila anavyoongea balozi wa TZ huko Brussels ni kama vile hatukuona livestream,napata shida sana na viongozi wetu kwa kweli...dah
 
Mimi nilijua nakuja kukanusha kwamba hata kamati haijakaa na kwamba CDM wametengeneza ili clip. kumbwe kweli wameongelea ujinga uliofanyika kwenye uchaguzuzi. no bora angekaa kimya
 
He's lovely young diplomat at the very important place.

Afaa sana huyu.

Mwenzako alipeleka "letters of credentials" Brussels na akapokewa.
una sound kama unafurahia recognition ya mabeberu ya brussels?kupokelewa letter yake ila katudharau huyo diplomat kutuafafanulia kilichoongelewa sababu tuliona livestream an kiingereza tunakijua
 
Mimi nilijua nakuja kukanusha kwamba hata kamati haijakaa na kwamba CDM wametengeneza ili clip. kumbwe kweli wameongelea ujinga uliofanyika kwenye uchaguzuzi. no bora angekaa kimya
mkuu tunaongozwa na bogus. wazungu watakuwa wanajiuliza kama huyu kaja kuwawakilisha huku,je aliowaacha kule wanafananaje
 
mkuu tunaongozwa na bogus. wazungu watakuwa wanajiuliza kama huyu kaja kuwawakilisha huku,je aliowaacha kule wanafananaje
JANA MATAGA walisema mkubwa wao kakanusha,nikajiuliza mkubwa wa kina Mc allister aliyekanusha ni nani?kumbe balozi wa Tz huko ubelgiji, duh
 
Hawa Dona kantri wanalilia misaada ya mashoga?.
 
Hawa Dona kantri wanalilia misaada ya mashoga?.
Halafu hii issue ya ushoga, ni propaganda nyingine ambapo Makonda alikwenda kinyume na katiba ya nchi kwa kutangaza kuwakamata mashoga wa Dar. Sasa hapo mabeberu wamemlazimisha nani kuwa shoga?😀🤦🏾‍♂️
 
Ninafikiri Bunge la Umoja wa Ulaya ndo waliopaswa kukanusha. Kama suala ni mawazo ya baadhi ya wabunge wa bunge la Ulaya, balozi wetu amepata wapi uhakika kwamba mawazo ya hao baadhi ya wabunge yamekubaliwa au yamekataliwa? Sasa balozi wetu anajua kuwa lolote kama bunge hilo limehitimisha mjadala huo ama bado?
 
Halafu hii issue ya ushoga, ni propaganda nyingine ambapo Makonda alikwenda kinyume na katiba ya nchi kwa kutangaza kuwakamata mashoga wa Dar. Sasa hapo mabeberu wamemlazimisha nani kuwa shoga?😀🤦🏾‍♂️
Wanakurupuka Tu, wakipewa fedha wanawaita nchi rafiki, Wakiambiwa wafuate democrasia wanawaita mabeberu/ mashoga. Nchi ya waliochanganyikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…