Ubalozi wakanusha habari za uongo zinazodai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo

Sasa mmeshindwa nini kupeleka waandishi huko majuu wakaripoti nyie si matajiri ?

Pili wasema ulaya unemployment rate iko juu sababu ya covid je unafikiri hata kama waso na ajira ni wengi utaweza kulinganisha na bongo!? Ulaya matatizo yapo ila hayawezi kufikia matatizo ya bongo

Ndio uone hata hiyo misaada ya chakula na food banks wenzetu wanazo je bongo wapi mnatoa walau chakula bure wakati tunasikia mabillioni yanachotwa na watu wanadunda mtaani tu kama kawaida ! Huku masikini akibaki masikini na tajiri akiendelea kuwa tajiri
 
Wanakurupuka Tu, wakipewa fedha wanawaita nchi rafiki, Wakiambiwa wafuate democrasia wanawaita mabeberu/ mashoga. Nchi ya waliochanganyikiwa.
Tamaa ya madaraka na ufisadi ndiyo maana wanataka kutawala milele! Taifa kwa ujumla likipata shida, wao marupurupu yao yapo pale pale.
 
Hongera Mhe. Balozi! Pia mwenye nyaraka za hili sakata atusaidie. Hivi mkopo mkubwa hivyo unatoka bila mkataba???

Queen Esther
 
Mkuu weka basi azimio lasimi la bunge la ulaya
Kikao ni hatua ya kwanza. hawa wanafuata utaratibu na utaratibu mjadala huanza mengine yanafuata. Mbona mna haraka...vuteni subira tusiandikie mate.
 
Kwani wewe ndie unaeamua kuweka au kutoweka hivyo vikwazo?
 
Nimemsikiliza Balozi Jestas Nyamanga akitolea ufafanuzi wa kile alichokiita upotoshaji kuhusu mjadala unaoendelea katika bunge la Ulaya kuhusu Tanzania.

Anadai kilichoketi ni kamati sio bunge zima. Na kwenye kamati waliozungumza ni wabunge watano tu. Hivyo anahitimisha kuwa maoni ya wabunge watano hayawezi kuhesabiwa kuwa ya bunge zima.

Kitu ambacho Balozi hajataka kusema ni kwamba mjadala wa kuhusu Tanzania ni lazima uanzie kamati. Ukitoka kwenye kamati ndipo utaenda kwenye bunge zima. Kwahiyo balozi kusema ni kamati tu imejadili, ni kama anataka kusema mjadala utaishia hapohapo kwenye kamati. Si kweli.

Taarifa ya kamati itapelekwa bungeni ili kuwa na mjadala wa bunge zima. Hata Tanzania tunafanya hivyo. Skendo zote kubwa za Richmond, EPA, Escrow etc mjadala wake ulianzia kwenye kamati na baada ya kamati ndipo bunge zima likajadili. Kwahiyo Balozi angejipa muda ili mjadala utakapohamia kwenye bunge zima asikose cha kuwaambia watu.

Balozi anadai hata kwenye kamati walioongea ni wajumbe watano tu. Na anataka kuitumia idadi hiyo kupuuza maoni ya kamati. Hii si sahihi. Kwanza kitendo cha Mwenyekiti wa kamati hiyo David McAllister kuongea, huo ndio msimamo wa kamati, hata wengine wasipoongea.

Nimkumbushe Balozi kwamba wakati wa skendo ya Richmond, Kamati teule ilikua na wajumbe 11, lakini walioongea public ni watatu tu ambao ni Stella Manyanya, Lucas Selelii na Mwenyekiti wao Harrison Mwakyembe. Je yale mapendekezo yalipuuzwa kwa sababu waliongea wajumbe watatu?

Jambo la muhimu kujiuliza ni je, tuhuma dhidi ya Tanzania ni za kweli au uzushi? Kamati imesema Uchaguzi ulivurugwa. Vyombo vya dola vilitumika kukandamiza upinzani na kukipendelea chama tawala. Baadhi ya watu waliuawa na wengine kuwekwa jela. Je tuhuma hizo ni kweli au uzushi? Hizi ndio hoja za McAllister na kamati yake. Kwahiyo Balozi ajibu hizo hoja sio kusema walioongea kwenye kamati walikua watano tu. 🤣

Halafu Balozi amekwepa kusema ukweli kwamba ni Kamati hiyohiyo iliyotaka maelezo ndani ya saa 48 kwanini Tanzania ilipokea zaidi ya TZS Bilioni 75 za kupambana na athari za corona. Kwanini Balozi hakuishauri serikali igome kutoa maelezo kwa sababu wanaotaka maelezo ni wajumbe watano tu wa kamati? Paradox.!

Wakati akijaribu kujieleza Balozi amejikuta akijikanusha mwenyewe. Amesema Tanzania hatupewi €626M kutoka EU. Halafu hapohapo akasema pesa hizo hazijazuiwa, tumekuwa tukipewa na tutaendelea kupewa kwa sababu zinasaidia miradi ya maendeleo. Sasa kama amekanusha kuwa hatupewi pesa na EU hizo zinazotusaidia kwenye miradi ya maendeleo ni za EU ipi? Liars must have a good memory.

Halafu tuache hii tabia ya kuamini kwamba kila taarifa anayoitoa kiongozi ni ya kweli. Mnakumbuka SACP Zombe alipoua wale wafanyabiashara na kusema ni majambazi, nchi nzima ilimuamini. Kama sio Kikwete kuingilia kati na kuunda kamati, tungeendelea kuamini waliouawa ni majambazi.

Mmesahau kuwa ndege yetu ilipozuiwa Afrika kusini, Bwana Kabudi alijitokeza na kukanusha vikali. Akasema ndege haijazuiwa na wanaoeneza taarifa hiyo ni waongo na wazushi? What happened later?

Tusubiri kamati ya mambo ya nje ya EU imalize vikao vyake ipeleke mapendekezo kwenye bunge zima. Lakini tuache kuhusisha nchi yetu tukufu na "uhuni" wa viongozi wachache. Tanzania yetu ni kubwa kuliko viongozi. Hawa viongozi watapita lakini Tanzania itadumu. Kiongozi akiamua kufanya uhuni, tunapaswa tumlaumu yeye, si kulaumu wanaotaka kutuwekea vikwazo kwa sababu ya uhuni wa viongozi wetu.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Mpumbavu hutizama alipoangukia na kulaumu bali mwerevu huchunguza alipojikwaa na kujisahihisha" Tuangalie tumejikwaa wapi. Kuwatukana mabeberu ni kutizama tulipoangukia. Tuangalie kilichofanya hao mabeberu wakatugeukia ghafla. Mimba haifichwi kwa kuvaa nguo kubwa.!
 
yaliyotolewa sio maazimio ya kamati ni wabunge binafsi kuchangia kwenye kamati
ni kikao cha kamati. Nadhani sote tunaelewa maana ya kamati. Ieleweke kwamba kama ni kamati bila shaka ni wawakilishi wa wabunge waliobiki. Otherwise utueleze kwa nini inaitwa kamati?
 
Sio propaganda.

Abiy ananyang'anya ardhi ili awape makabaila wa kizungu.

Sasa wananchi wa Ethiopia wamekuwa wakimbizi na wengine twawakamata huko Morogoro.

Ndo mlitaka Tundu Lissu afuate sera hizo kuweka rehani rasilimali za nchi.
Acha uongo we jamaa...

Tuwekee chanzo cha hi taarifa yako.
 
hivi hii nchi imekosa msemaji wa serikali yaani ishu nyeti kama hii anajibu balozi anyway naona bado kuna teuzi tusishangae tumbili ,haraka haraka,msibani,mayela,na wasaka tonge wengi wakiijibia serikali naomba katiba iheshimiwe mambo ya serikali yajibiwe na mhusika baloz mwenyewe kujieleza hajui anaonekana kabisa anajikomba ,serikali ni taasisi kubwa
 
Huu Uzi utachukiwa na watu sana kwa kuwa watu wanamalengo mabaya na Tanzania

Na hii haitikuja kutumia kamwe Tanzania ni nchi ya tofauti sana duania kama tuliwafukuza nzige na kuzuia covid Mungu wetu halali
Yaani mlitegemea mfanye mliyofanya halafu dunia inyamaze?
 
Tena wenye misimamo kama yako ndio walimuangusha Lisu baada ya kuona anataka kutawala nchi wakiwa na Amsterdam
Hakuna aliemuangusha Lissu, bali kuna waliotuangusha watanzania. unataka kuwajuwa waliotuangusha watanzania wengi kwa kumfurahisha mtu mmoja?
Baadhi yao ni Ma DED, RC's, Polisi, Jeshi la Tanzania, TISS na wengine waliotumika ama kwa manufaa yao au kwa kuogopa vibarua vyao. Hao wote hawakujali maslahi ya taifa kwa ujumla na wakaamua kututumbukiza sote na kutuweka katika dimbwi hili leo!
Sasa yanayoendelea na yatakayoendelea kutokea yatamhusu kila mmoja wetu na si Lissu pekee!
 

kwani sisi hatujui lugha😂
 
Huyo Balozi ni mjinga mno maoni ni maoni hata yangetolewa na mtu mmoja tu
 
Hapana kuonyeshwa kuchukizwa na kuingiliwa mambo yetu wafukuzwe haraka na sisi tuondoe mabalozi huko kwao unaonaje hiyo?
Kuwabambikia kesi kesi uonevu kuwapiga risasi wapinzani ni kuingiliwa mambo yenu? Kuiba kutafuna pesa za corona kienyeji kifisadi ni mambo yenu mnaingiliwa siyo? Kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi ni mambo yenu hutaki yaingiliwe? Kama hamtaki mambo yenu yaingiliwe acheni kufanya vitu haramu vya kishamba na kishetani
 
Mbona hizo 27million Euros ni ndogo sana. Kama hata hao wachangiaji hawafahamu kama kweli walitoa hiyo pesa, ujinga mtupu. Tanzania sasa naona wapo pazuri lazima wale sahani moja na hawa wapumbavu.
Upumbavu ni kula pesa za corona kienyeji kifisadi siyo kumlaumu aliyetoa pesa ambaye anasaka ukweli juu ya matumizi yake
 
Mbona Amsterdam na Tundu "Quinsling" Lissu leo wako kimya, mipango imebuma au?
Robert Amsterdam"Final review of our ICC submission. Filing early next week".
List ya majina yatakayotumwa ICC inatisha...hajaachwa mtu maweee...sisi wanyonge tunamuita BOB...Lissu ni Patriot mtamuita majina yote na bado ”ndoo” za Ulaya mtazijaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…