Sasa mmeshindwa nini kupeleka waandishi huko majuu wakaripoti nyie si matajiri ?Sisi tunatakiwa nasi tuwe na waandishi wa habari mahiri na vyombo vya habari mahiri kutangaza masuala yao huko wako.
Ulaya wapo ombaomba, kuna food bank wazifahamu hizi?
Idadi ya waso na kazi ni kubwa na sasa COVID -19 yawala wao kisawasawa, hivyo nao wana matatizo mengi tu wakae kimya kila mtu ashughulike na lwake.
Sie twapeta tu.
Sasa kama twataka usawa wa propaganda basi twaanzia hapo.
Halafu, uzuri mimi nimeishi huko Ulaya na Marekani hivyo nafahamu ninacho kiongea.
Kumbuka, hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hakumwambia bwana Sir Edward Twinning kwamba ataka uhuru halafu baadae arudishe uhuru huo kwa wazungu kwa njia ya kujikombakomba.
Pili wasema ulaya unemployment rate iko juu sababu ya covid je unafikiri hata kama waso na ajira ni wengi utaweza kulinganisha na bongo!? Ulaya matatizo yapo ila hayawezi kufikia matatizo ya bongo
Ndio uone hata hiyo misaada ya chakula na food banks wenzetu wanazo je bongo wapi mnatoa walau chakula bure wakati tunasikia mabillioni yanachotwa na watu wanadunda mtaani tu kama kawaida ! Huku masikini akibaki masikini na tajiri akiendelea kuwa tajiri