Ubalozi wakanusha habari za uongo zinazodai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo

Wazungu tunawategemea ila kutwa kuwasimanga kwa kuwaita mabeberu! Kuweni na shukurani na sio kuleta kejeli na dharau huku watu wenyewe sisi ni tegemezi.

Kwa jinsi tunavyowakejeli, wazungu hawa wangekuwa na mavichwa kama yetu, hata hiyo misaada na mikopo wangeshaisitisha, ila wamegundua baadhi ya watu wetu ni wajinga na wameamua kuwapuuza ili kusaidia masikini wa hii nchi wasio na hatia.

Isitoshe kwa hapa JF, uzi uliopo unaongelea kamati na si Bunge zima.

Alafu elezeni pia mlikopeleka hela za Covid.

Sisi tunasubiri taarifa rasimi ya hilo Bunge ila mpaka sasa teyari ni aibu tosha kwani hatukwahi kuwa na status mbovu na mbaya kiasi hiki.

Awamu hii ni shida tupu!

No wonder hata JK aliwahi sema watu waache "kujimwambafai."
Mbona ndivyo mabunge yote hufanya kazi kupitia kamati za kisekta na Bunge zima kubariki kwa wabunge wachache kujadili na kuunga mkono Azimio. Hiyo ndio imetoka tena tutegemee mapendekezo makali zaidi tuendelee kufanya robbing maana na serikali kupitia embassy mbalimbali wanafanya robbing ya kupunguza ukali wa maazimio tu na si kuyazuia kwani yasemwayo yapo wazi sana na ya kishamba mmo.
 
Wapi tumesema kuna maazimio. Nenda kwenye main thread kama utakuta neno maazimio
Sasa mnakata viuno humu vya nini sasa?

Bunge linapokaa kinatoka na azimio, na azimio linatokana na maoni ya watu kama hao uliowanukuu jana hapa. Bunge likishajiridhisha ndio linaweka azimio likiona ni upuuzi linapiga kimya.

Sasa hebu niambie azimio la hilo bunge kutokana na maoni ya wale wabunge ni lipi?
 
Huu Uzi utachukiwa na watu sana kwa kuwa watu wanamalengo mabaya na Tanzania

Na hii haitikuja kutumia kamwe Tanzania ni nchi ya tofauti sana duania kama tuliwafukuza nzige na kuzuia covid Mungu wetu halali
 
Mbona ndivyo mabunge yote hufanya kazi kupitia kamati za kisekta na Bunge zima kubariki kwa wabunge wachache kujadili na kuunga mkono Azimio. Hiyo ndio imetoka tena tutegemee mapendekezo makali zaidi tuendelee kufanya robbing maana na serikali kupitia embassy mbalimbali wanafanya robbing ya kupunguza ukali wa maazimio tu na si kuyazuia kwani yasemwayo yapo wazi sana na ya kishamba mmo.
Kwahiyo bunge la ulaya limetoa azimio kwamba litainyima tz mikopo?
 
Sasa mnakata viuno humu vya nini sasa?

Bunge linapokaa kinatoka na azimio, na azimio linatokana na maoni ya watu kama hao uliowanukuu jana hapa. Bunge likishajiridhisha ndio linaweka azimio likiona ni upuuzi linapiga kimya.

Sasa hebu niambie azimio la hilo bunge kutokana na maoni ya wale wabunge ni lipi?
Unajua ufanyaji kazi wa mabunge ulivyo??? Mijadala na majadiliano ya kina yanafanyika kwenye kamati, kamati pia ndo zinaandaa maamuzi na kupeleka kwenye bunge kwa ajili ya maazimio.

Sasa kwa akili yako unafikiri hii kamati ikipeleka azimio kwenye Bunge, Bunge litapinga????

Au kwa akili zenu vilaza wa Lumumba mnafikiri bunge la EU ni sawa na bunge lenu utopolo la Ndugai????
 
Salary Slip, haina maana hatuna shukrani. Hapa kuna shida sehemu, na sio nyingine ila ni maslahi.

Kama wanataka tuwe mafala kwasababu ya kutupa misaada, mimi binafsi na wengine wenye misimamo kama yangu tutawapinga na hatuta acha kuwaita mabepali.

Kama dhambi na ushenzi waanze wao kwanza kutubu kwa dhuluma walizofanya.
 
Ubalozi wa Tanzani Ubelgiji umekanusha habari za uongo zinazoenezwa mitandaoni kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo.

Ubalozi umeeleza kuwa ni wabunge watano tu kati ya wabunge 71 wa Kamati ya Mambo ya Nje ndiyo walitoa mawazo yao na hakuna azimio lolote lililowekwa dhidi ya Tanzania na Kamati hiyo. Imeelezwa kuwa Mbunge yeyote anaweza kutoa mawazo yake binafsi na na siyo kila wazo binafsi la Mbunge ni azimio la Bunge.

Bunge lote la Ulaya lina wabunge 705 na waliotoa mawazo yao binafsi walikuwa ni wabunge watano (5) tu. S
Sikiliza clip hii

View attachment 1630332
Hongera Balozi. Hiki ulichofanya ndicho kinachotakiwa na mabalozi wetu wote.
 
Huu Uzi utachukiwa na watu sana kwa kuwa watu wanamalengo mabaya na Tanzania

Na hii haitikuja kutumia kamwe Tanzania ni nchi ya tofauti sana duania kama tuliwafukuza nzige na kuzuia covid Mungu wetu halali
mungu wenu ndo a nawaambia muue wapinzani wenu, muwabambikie kesi na mpore ushindi wao???? Subirini tu muone majibu ya Mungu aliye hai.

Na huu ni mwanzo tu, yajayo ndo makubwa zaidi, jiandaeni na ICC na nyundo takatifu kutoka kwa USA
 
Hongera Balozi. Hiki ulichofanya ndicho kinachotakiwa na mabalozi wetu wote.
Amefanya kitu gani???😂😂😂😂😂

Kwa iyo kwa wana Lumumba hapo mmeona Balozi kafanya jambo kuuubwaaaaa😂😂😂😂
 
Ubalozi wa Tanzani Ubelgiji umekanusha habari za uongo zinazoenezwa mitandaoni kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo.

Ubalozi umeeleza kuwa ni wabunge watano tu kati ya wabunge 71 wa Kamati ya Mambo ya Nje ndiyo walitoa mawazo yao na hakuna azimio lolote lililowekwa dhidi ya Tanzania na Kamati hiyo. Imeelezwa kuwa Mbunge yeyote anaweza kutoa mawazo yake binafsi na na siyo kila wazo binafsi la Mbunge ni azimio la Bunge.

Bunge lote la Ulaya lina wabunge 705 na waliotoa mawazo yao binafsi walikuwa ni wabunge watano (5) tu. S
Sikiliza clip hii

View attachment 1630332
Hali inazidi kuwa mbaya.
 
Unajua ufanyaji kazi wa mabunge ulivyo??? Mijadala na majadiliano ya kina yanafanyika kwenye kamati, kamati pia ndo zinaandaa maamuzi na kupeleka kwenye bunge kwa ajili ya maazimio.

Sasa kwa akili yako unafikiri hii kamati ikipeleka azimio kwenye Bunge, Bunge litapinga????

Au kwa akili zenu vilaza wa Lumumba mnafikiri bunge la EU ni sawa na bunge lenu utopolo la Ndugai????
Yani kamati inaandaa maamuzi na kupeleka bungeni?
Bunge linaenda kuyafanyia nini sasa hayo maamuzi kama kamati imeshaamua?

Mkuu kwanini usikubali tu kwamba yale yalikuwa ni maoni ya wabunge na si azimio la bunge?
 
Salary Slip, haina maana hatuna shukrani. Hapa kuna shida sehemu, na sio nyingine ila ni maslahi.

Kama wanataka tuwe mafala kwasababu ya kutupa misaada, mimi binafsi na wengine wenye misimamo kama yangu tutawapinga na hatuta acha kuwaita mabepali.

Kama dhambi na ushenzi waanze wao kwanza kutubu kwa dhuluma walizofanya.
Tena wenye misimamo kama yako ndio walimuangusha Lisu baada ya kuona anataka kutawala nchi wakiwa na Amsterdam
 
Yani kamati inaandaa maamuzi na kupeleka bungeni?
Bunge linaenda kuyafanyia nini sasa hayo maamuzi kama kamati imeshaamua?

Mkuu kwanini usikubali tu kwamba yale yalikuwa ni maoni ya wabunge na si azimio la bunge?
Kwa iyo kwa akili yako unafikiri walijadili ili iweje??? Hujui kuwa kamati zinapelekaga mapendekezo bungeni kwa ajili ya bunge kufanya maazimio????

Una elimu gani we mtu??? Au unashabikia tu siasa na hujui mifumo ya kisiasa inavyofanya kazi???
 
CHADEMA hamtaamini kitakacho tokea mwisho wa hili sakata, lazima jpm awa prove wrong eu na wote wanaoiwazia mabaya nchi yetu. Nchi hii ina Mungu ndugu zangu tofauti na tunavyo dhani, tumekwepa mengi sana yaliyokua yanafikiliwa km yangetuvuruga kabisa lakini tumevuka na chadema mkiwa mashahidi lakini bado hamjifunzi kuweka akiba ya maneno
 
MARA YA MWISHO UBALOZI WA BELGIUM KUPOST TWITTER NI TAREHE 16 OFFICIAL ISSUES ZOTE LAZIMA WAPOST TWITTER
PILI BUNGE LA ULAYA WABUNGE 705 SIYO 71
TATU UBALOZI WA UBELGIJI HAUWEZI KUTOA TAARIFA KUHUSU EU PARLIAMENT HATA KAMA MAKAO MAKUU YAPO BRUSSELS KUNA
OFISI YA EU HAPA TANZANIA WAO NDIYO WANATAKIWA KUTOA TAARIFA KWANZA KILICHOPO WAO(WAKO KIKAANGONI WAELEZE ILKUWAJE WAKATOA HIZO BILIONI 63

Why are using your time Kuwa jibu Hawa watu walioficha akili zao?
 
Mbona huyo balozi anajichanganya anakana kuwa umoja wa Ulaya huwa inatupa pesa at the same time anakataa kuwa pesa Hamna pesa zozote zilizozuiliwa na umoja wa Ulaya.
 
Back
Top Bottom