Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Hauelewi unachoongea.Kote duniani mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa hufanyika tu miezi michache kuelekea uchaguzi mkuu. Hata huko Ubelgiji, Ujerumani, EU na USA ndivyo mambo yanavyokuwaga. Baada ya hapo the winner takes it all na upinzani huhamia bungeni.
Ndiyo maana ya demokrasia: the majority (washindi) rules and the minority (wapinzani) are allowed to talk in parliament and may be listened. Ukiona wananchi wanaandamana kipindi ambacho si cha uchaguzi, ujue ni kwa ajili ya kudai vitu kama kupunguziwa bei ya chakula ambacho kwao ni mkate lakini kwetu ni mchele, sembe na maharage. Au kuongezewa mshahara, kupunguziwa bei ya umeme, maji, dawa, usafiri etc
Sasa sisi ni nani kutaka kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa anytime every time? Tunataka the minority and the loosens of the election to be our rulers!!
1. Marekani ni mtu ndie anayegombea na sio chama.
2 Ukimzuia mtu ( au taasisi yeyote) yeyote kuongea kwa vyovyote vile kutapingana na First Amendment ya Katiba yao ambayo inatoa haki ya kuzungumza kwa uhuru na uwazi bila kuingiliwa kwa namna yeyote na serikali.
3. Kutokana na First Amendment vyombo vya habari, watu binafsi, vyama vya siasa, asisi tofauti n.k. zinauwezo wa kuikosoa na kuipinga serikali wakati wowote na bila uoga. Ndio maana mpaka sasa hivi kuna watu wanasema wazi kuwa hawamtambui Biden kama Rais wao. Wakati wa Trump watu kama De Niro, Spike Lee, Snoop walikuwa wanamtukana Trump matusi ya nguoni bila kujificha.
4. Trump toka ameshindwa amekuwa akifanya mikutano ya siasa na hivi karibuni ametangaza nia ya kugombea na ataendelea na mikutano ya hadhara ambapo ataiponda serikali iliyopo na kujisifia kuwa yeye ni bora zaidi.
5. Stacey Abrams aliposhindwa kwa mara ya kwanza aliendelea kuorganize watu kwa ajilu ya uchaguzi wa mwaka huu.
6. Marekani mikutano ya hadhara ni njia moja tu ya kutangaza sera zako. Nyingine ni TV, radio, social media, town hall meetings n.k. ambazo anasiasa wanazitumia zaidi kwa sababu zina uwezo wa kufikia wapiga kura wengi. Unapokaribia uchaguzi ndio mikutano ya hadhara, simu, flyers na kugonga milango kunashamiri. Kinachowafanya wanasiasa wasifanye siasa za namna hii muda wote ni gharama. Wakati kama huu wanategemea zaidi interviews kwenye TV, na juhudi za taasisi zinazowaunga mkono.
Sisi nyumbani sio tu watu hawaruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara bali hata hizo njia mbadala ni shida.
Kwa kifupi katika nchi ulizotaja hakuna nchi inayozuia raia wake kufanya mikutano ya kisiasa popote pale.
Amandla...