Thailand
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 275
- 795
Kwa mujibu wa hotuba ya mh. Pius Msekwa katibu wa bunge kipindi cha kusaini hati ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar amedai kwamba baada tu ya muungano huo rais wa Zanzibar Mzee Karume alijihudhuru cheo chake cha urais na kuwa Makamo wa rais wa Kwanza wa JMT chini ya rais Mwl. JK Nyerere.
Utaratibu huu ulipaswa kuendelea hivyo hivyo hadi leo lakini sijui ilitokea wapi au kushindwa wapi kusimamia hati hiyo, leo hii Zanzibar wana rais wao, makamo wawili wa urais, nyimbo ya utaifa, bendera ya utaifa na mambo mengi ambayo ni manufaa kwa wazanzibar huku Tanganyika kutokujulikana ilipotelea wapi!
Katika maadhimisho ya muungano hakuna aliyegusia juu ya kero za muungano zinazowakumba watanganyika japo kuwa tuna watanganyika ambao wakishapewa madaraka wanajifanya hawaoni kero za muungano hasa kwa taifa la Tanganyika katika kudumisha muungano. Embu cheki hizi baadhi ya kero ambazo zinaelekea kuielemea Tanganyika;
1. Kupoteza utambulisho wa kitaifa wa nchi Tanganyika huku wenzetu wakiitukuza nchi yao ya Zanzibar popote walipo
2. Serikali ya Tanganyika kutumia rasilimali zake muhimu kulinda usalama wa Zanzibar sijui hapa wanatulipa kitu gani
3. Wananchi wa zanzibar kulipwa mishahara mara mbili, mfano Tanganyika inapolipa wabunge kutoka zanzibar huku hakuna Mtanganyika anaeshiriki bunge la Zanzibar.
4. Ajira za Tanganyika zinafunguliwa kwa watanganyika na wazanzibar wote ziwe za ualimu, afya n.k wakati ajira za wazanzibar ni kwa ajili ya wazanzibar pekee.
5. Ardhi ya watanganyika huko mtwara, kigoma, Pwani na sehemu yoyote ile ni mali ya wazanzibari 100 pasee kununua na kufanya makazi hata kurithisha wajukuu na vitukuu vyao, lakini mtanganyika zanzibar unakaribishwa kama muwekezaji means unamiliki ardhi kwa muda then uondoke uwaachie ardhi yao.
6. Leo hii Mama Samia anatawala ardhi ya Tanganyika kama rais lakini Mtanganyika huwezi kupeleka huko kwao kichwa chako eti kuwa rais wa Zanzibar, hii ni hatar kama nchi.
Watanganyika tupo zaidi ya million 55 tunashindwa kweli kupambana kuitafuta TANGANYIKA yetu au kushinikiza Kupata Tanzania yenye muunganikano wenye usawa?
Serikali tatu ni muhimu sana kama tunaitaji muungano huu uendelee pasipo malalamiko, yaani kila serikali ya Tanganyika iwe na makamo wake wa rais, huku Zanzibar pia ikiwa na makamo wake wa rais ambao wote wanakuwa chini ya Rais mmoja wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania apo tutaenda sawa.
Kusiwepo na vikwazo vya umiliki wa ardhi na biashara kwa wananchi wa pande mbili Tanganyika na Zanzibar ieleweke sio kwamba watanganyika hatutaki muungano bali tunataka usawa ambao sasa tunaona unaelemea kwa Wazanzibar. Watanganyika wenzetu mliopo madarakani msitusahau Wala kuisahau Tanganyika kiasi hicho.