Ubinafsi wa wazanzibar ulitokea wapi baada ya muungano wa Tanzania?

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
Kwa mujibu wa hotuba ya mh. Pius Msekwa katibu wa bunge kipindi cha kusaini hati ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar amedai kwamba baada tu ya muungano huo rais wa Zanzibar Mzee Karume alijihudhuru cheo chake cha urais na kuwa Makamo wa rais wa Kwanza wa JMT chini ya rais Mwl. JK Nyerere.

Utaratibu huu ulipaswa kuendelea hivyo hivyo hadi leo lakini sijui ilitokea wapi au kushindwa wapi kusimamia hati hiyo, leo hii Zanzibar wana rais wao, makamo wawili wa urais, nyimbo ya utaifa, bendera ya utaifa na mambo mengi ambayo ni manufaa kwa wazanzibar huku Tanganyika kutokujulikana ilipotelea wapi!

Katika maadhimisho ya muungano hakuna aliyegusia juu ya kero za muungano zinazowakumba watanganyika japo kuwa tuna watanganyika ambao wakishapewa madaraka wanajifanya hawaoni kero za muungano hasa kwa taifa la Tanganyika katika kudumisha muungano. Embu cheki hizi baadhi ya kero ambazo zinaelekea kuielemea Tanganyika;

1. Kupoteza utambulisho wa kitaifa wa nchi Tanganyika huku wenzetu wakiitukuza nchi yao ya Zanzibar popote walipo

2. Serikali ya Tanganyika kutumia rasilimali zake muhimu kulinda usalama wa Zanzibar sijui hapa wanatulipa kitu gani

3. Wananchi wa zanzibar kulipwa mishahara mara mbili, mfano Tanganyika inapolipa wabunge kutoka zanzibar huku hakuna Mtanganyika anaeshiriki bunge la Zanzibar.

4. Ajira za Tanganyika zinafunguliwa kwa watanganyika na wazanzibar wote ziwe za ualimu, afya n.k wakati ajira za wazanzibar ni kwa ajili ya wazanzibar pekee.

5. Ardhi ya watanganyika huko mtwara, kigoma, Pwani na sehemu yoyote ile ni mali ya wazanzibari 100 pasee kununua na kufanya makazi hata kurithisha wajukuu na vitukuu vyao, lakini mtanganyika zanzibar unakaribishwa kama muwekezaji means unamiliki ardhi kwa muda then uondoke uwaachie ardhi yao.

6. Leo hii Mama Samia anatawala ardhi ya Tanganyika kama rais lakini Mtanganyika huwezi kupeleka huko kwao kichwa chako eti kuwa rais wa Zanzibar, hii ni hatar kama nchi.

Watanganyika tupo zaidi ya million 55 tunashindwa kweli kupambana kuitafuta TANGANYIKA yetu au kushinikiza Kupata Tanzania yenye muunganikano wenye usawa?

Serikali tatu ni muhimu sana kama tunaitaji muungano huu uendelee pasipo malalamiko, yaani kila serikali ya Tanganyika iwe na makamo wake wa rais, huku Zanzibar pia ikiwa na makamo wake wa rais ambao wote wanakuwa chini ya Rais mmoja wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania apo tutaenda sawa.

Kusiwepo na vikwazo vya umiliki wa ardhi na biashara kwa wananchi wa pande mbili Tanganyika na Zanzibar ieleweke sio kwamba watanganyika hatutaki muungano bali tunataka usawa ambao sasa tunaona unaelemea kwa Wazanzibar. Watanganyika wenzetu mliopo madarakani msitusahau Wala kuisahau Tanganyika kiasi hicho.
 
Rejea:
"... hatuwezi kuiacha Zanzibar ijitawale sababu Waislsmu wa itikadi kali wataweka makazi yao huko na kutuletea shida... " by William Lukuvi akiwa kanisani.
Vumilia yote ili azma hiyo ititimie.
Mbona tumeweza kuishi na majirani wakorofi kama Kenya, Rwanda lakini kila mmoja anaheshimu mipaka ya mwenzake
 
Mkuu 'Thailand', hapa kuna kila sababu ya kuwalaumu viongozi wote walioongoza serikali ya Tanzania tokea Mwinyi hadi sasa kwa Samia.

Na hasa hasa, lawama zielekezwe kwa chama cha CCM, ambao wao rushwa ndiyo wanadhani ni suluhisho la matatizo yanayowakabili.

Zanzibar imefikia hapo ilipofikia kwa kupewa rushwa wasiendelee kupiga kelele, hasa kile kikundi kinachojisogeza zaidi na kujitambulisha na uarabu wao.
CCM walidhani kwamba wakitoa rushwa kelele za kutaka madaraka kamili kwa Zanzibar zitakwisha.

Huu muungano ulitakiwa kufikia wakati huu uwe na serikali moja tu, serikali inayotambulika kuwa ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, lakini kwa sababu ya udhaifu wa viongozi hao, tokea Mwinyi hadi kwa Samia, wameruhusu Zanzibar ndiyo iwe na madaraka zaidi juu ya Tanzania.

Lakini, pamoja na udhaifu huu, jambo moja litabaki kuwa ndilo ukweli: Zanzibar, kwa aina yoyote ile haitaweza tena kuondoka katika muungano huu.
 
Naunga Mkono kurekebisha Kero za Muungano lakini siungi Mkono Kuvunjika Kwa Muungano.

Siungi Mkono Serikali Tatu, Hii itawapa uhalali kabisa Zanzibar kuwa Nchi inayojitegemea na Muungano hautakua na Maana yoyote.

Katiba inapaswa kuwa Moja, Raisi Mmoja, Baraza la Mawaziri Moja na Wimbo mmoja wa Taifa. Ardhi yote iliyopo Tanzania iwe chini ya Wa Tanzania wotee Bila Kujali Eneo la Kijiografia, hoja ya Kusema Zanzibar ni ndogo Ardhi ibaki Kwa wazanzibar ni hoja mfu isiyo na Mashiko yoyote.

Hata wachina Leo Hii wanahangaika kuileta HongKong na Taiwan kuwa sehemu Moja na sio Ile One Country two Systems, Huu ni Uhuni. Huwezi ukasema Una nchi halafu watu wake wamegawanyika na wanaviongozi tofauti. Itakuaje Siku Raisi wa Zanzibar akiamua kusaliti na Kupewa Nguvu na Mataifa Dhalimu maana hata Askari japo wako chini ya Jeshi Moja lakini tayari wako katika Nchi inayojitegemea kbisa kikatiba na Raisi.
 
Zanzibar hawajawahi kuutaka huu Muungano. Na ndio mana hadi hii leo hawautaki. Ila watanganyika ndio wanaoutaka na kuung'ang'ania. Kwahiyo acheni kulalamika kinafik
 
Lakini, pamoja na udhaifu huu, jambo moja litabaki kuwa ndilo ukweli: Zanzibar, kwa aina yoyote ile haitaweza tena kuondoka katika muungano huu.

Naunga Mkono kurekebisha Kero za Muungano lakini siungi Mkono Kuvunjika Kwa Muungano.

Siungi Mkono Serikali Tatu, Hii itawapa uhalali kabisa Zanzibar kuwa Nchi inayojitegemea na Muungano hautakua na Maana yoyote.

Katiba inapaswa kuwa Moja, Raisi Mmoja, Baraza la Mawaziri Moja na Wimbo mmoja wa Taifa. Ardhi yote iliyopo Tanzania iwe chini ya Wa Tanzania wotee Bila Kujali Eneo la Kijiografia, hoja ya Kusema Zanzibar ni ndogo Ardhi ibaki Kwa wazanzibar ni hoja mfu isiyo na Mashiko yoyote.

Hata wachina Leo Hii wanahangaika kuileta HongKong na Taiwan kuwa sehemu Moja na sio Ile One Country two Systems, Huu ni Uhuni. Huwezi ukasema Una nchi halafu watu wake wamegawanyika na wanaviongozi tofauti. Itakuaje Siku Raisi wa Zanzibar akiamua kusaliti na Kupewa Nguvu na Mataifa Dhalimu maana hata Askari japo wako chini ya Jeshi Moja lakini tayari wako katika Nchi inayojitegemea kbisa kikatiba na Raisi.

Thailand

Umeona watanganyika wenzako hao? Wapo tayari kwa lolote ila si kwa kuvunjika Muungano. Kwahiyo kama Mumeamua kuung'ang'ania muungano itabidi mukubali kuvumilia tu mana hakuna namna.
 
Unaweka 'spin' zisizokuwepo. "...kukubali kuvumilia..." kitu gani?
 
Naunga Mkono kurekebisha Kero za Muungano lakini siungi Mkono Kuvunjika Kwa Muungano.

Siungi Mkono Serikali Tatu, Hii itawapa uhalali kabisa Zanzibar kuwa Nchi inayojitegemea na Muungano hautakua na Maana yoyote.

Katiba inapaswa kuwa Moja, Raisi Mmoja, Baraza la Mawaziri Moja na Wimbo mmoja wa Taifa. Ardhi yote iliyopo Tanzania iwe chini ya Wa Tanzania wotee Bila Kujali Eneo la Kijiografia, hoja ya Kusema Zanzibar ni ndogo Ardhi ibaki Kwa wazanzibar ni hoja mfu isiyo na Mashiko yoyote.

Hata wachina Leo Hii wanahangaika kuileta HongKong na Taiwan kuwa sehemu Moja na sio Ile One Country two Systems, Huu ni Uhuni. Huwezi ukasema Una nchi halafu watu wake wamegawanyika na wanaviongozi tofauti. Itakuaje Siku Raisi wa Zanzibar akiamua kusaliti na Kupewa Nguvu na Mataifa Dhalimu maana hata Askari japo wako chini ya Jeshi Moja lakini tayari wako katika Nchi inayojitegemea kbisa kikatiba na Raisi.
Sasa tufanyeje ili kufikia kuwa na serikali moja huku nguvu zote anapewa zanzibar?
 
Rejea:
"... hatuwezi kuiacha Zanzibar ijitawale sababu Waislsmu wa itikadi kali wataweka makazi yao huko na kutuletea shida... " by William Lukuvi akiwa kanisani.
Vumilia yote ili azma hiyo ititimie.
Hapa pakiunganishwa na maslahi ya mabeberu yaan Roma,Anglikana na Uingereza ndo msingi wa muungano
 
Leo hii kila mtanganyika haoni umuhimu wa huu Muungano. Watanganyika wanafaidika nini?

Kama ni suala la ulinzi na usalama mbona Cuba na Usa zipo jirani lakini vyombo vyao vya usalama vinawalinda.

Wazanzimbar wapo tu kunufaika na rasilimali za Tanganyika huku watanganyika wakinyonywa.

Muungano ufe kabla ya 2025
 
Kusema ulinzi na usalama ni uoga na kutojiamini tu. Si afadhali tungeungana na kenya na Uganda tu ambazo ni kubwa sana.
 
Nyerere kuna mambo alifanya Kwa "agenda"...
Bahati mbaya hizo agenda zake hawezi ziweka wazi..
Ndo mana hata kina Warioba walikuwa hawamuelewi...

Muungano...
Kung'oa reli mikoa ya kusini
Kuzuia kilimo cha pamba mikoa ya kusini..
Ku sapoti waasi Nigeria kinyume na maazimio ya OAU...
Na mengineyo mengi sana
 
Mkuu the boss naona unafukua makaburi dhahiri kabisa,ila hili la kuwapa Msaada waasi wa Nigeria uku kukiwa na msisitizo wa kuunganisha bara la Afrika ulikuwa uamuzi wa ajabu sana na sijui kwanini aliamua kufanya vile
 
Mkuu the boss naona unafukua makaburi dhahiri kabisa,ila hili la kuwa Msaada waasi wa Nigeria uku kukiwa na msisitizo wa kuunganisha bara la Afrika ulikuwa uamuzi wa ajabu sana na sijui kwanini aliamua kufanya vile
We unaona Hilo la ajabu .
Je kung'oa reli mikoa ya kusini??
 
Mimi siku zote huwa najiuliza kwani muungano ni lazima hata kama hauna manufaa? Nchi ya Tanganyika irudishwe haraka alafu ndio tuongee sasa kama kuna haja ya kuungana
 
Kwa mujibu wa hotuba ya mh. Pius Msekwa katibu wa bunge kipindi cha kusaini hati ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar amedai kwamba baada tu ya muungano huo rais wa Zanzibar Mzee Karume alijihudhuru cheo chake cha urais na kuwa Makamo wa rais wa Kwanza wa JMT chini ya rais Mwl. JK Nyerere.

Utaratibu huu ulipaswa kuendelea hivyo hivyo hadi leo lakini sijui ilitokea wapi au kushindwa wapi kusimamia hati hiyo, leo hii Zanzibar wana rais wao, makamo wawili wa urais, nyimbo ya utaifa, bendera ya utaifa na mambo mengi ambayo ni manufaa kwa wazanzibar huku Tanganyika kutokujulikana ilipotelea wapi!

Katika maadhimisho ya muungano hakuna aliyegusia juu ya kero za muungano zinazowakumba watanganyika japo kuwa tuna watanganyika ambao wakishapewa madaraka wanajifanya hawaoni kero za muungano hasa kwa taifa la Tanganyika katika kudumisha muungano. Embu cheki hizi baadhi ya kero ambazo zinaelekea kuielemea Tanganyika;

1. Kupoteza utambulisho wa kitaifa wa nchi Tanganyika huku wenzetu wakiitukuza nchi yao ya Zanzibar popote walipo

2. Serikali ya Tanganyika kutumia rasilimali zake muhimu kulinda usalama wa Zanzibar sijui hapa wanatulipa kitu gani

3. Wananchi wa zanzibar kulipwa mishahara mara mbili, mfano Tanganyika inapolipa wabunge kutoka zanzibar huku hakuna Mtanganyika anaeshiriki bunge la Zanzibar.

4. Ajira za Tanganyika zinafunguliwa kwa watanganyika na wazanzibar wote ziwe za ualimu, afya n.k wakati ajira za wazanzibar ni kwa ajili ya wazanzibar pekee.

5. Ardhi ya watanganyika huko mtwara, kigoma, Pwani na sehemu yoyote ile ni mali ya wazanzibari 100 pasee kununua na kufanya makazi hata kurithisha wajukuu na vitukuu vyao, lakini mtanganyika zanzibar unakaribishwa kama muwekezaji means unamiliki ardhi kwa muda then uondoke uwaachie ardhi yao.

6. Leo hii Mama Samia anatawala ardhi ya Tanganyika kama rais lakini Mtanganyika huwezi kupeleka huko kwao kichwa chako eti kuwa rais wa Zanzibar, hii ni hatar kama nchi.

Watanganyika tupo zaidi ya million 55 tunashindwa kweli kupambana kuitafuta TANGANYIKA yetu au kushinikiza Kupata Tanzania yenye muunganikano wenye usawa?

Serikali tatu ni muhimu sana kama tunaitaji muungano huu uendelee pasipo malalamiko, yaani kila serikali ya Tanganyika iwe na makamo wake wa rais, huku Zanzibar pia ikiwa na makamo wake wa rais ambao wote wanakuwa chini ya Rais mmoja wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania apo tutaenda sawa.

Kusiwepo na vikwazo vya umiliki wa ardhi na biashara kwa wananchi wa pande mbili Tanganyika na Zanzibar ieleweke sio kwamba watanganyika hatutaki muungano bali tunataka usawa ambao sasa tunaona unaelemea kwa Wazanzibar. Watanganyika wenzetu mliopo madarakani msitusahau Wala kuisahau Tanganyika kiasi hicho.
Mleta mada alikuwa on point kisawasawa.
Unabaki unajiuliza maswali magumu, zaidi ya maswali yake yenye hoja nzito.
I am wondering, hivi ni nini hasa kilichotupeleka tuwe na Muungano huu?kitu gani hasa ambacho kinaendelea na kutukosesha raha Watanganyika over and over , kila linapotokea jambo au sakata kama hili la Bandari among other issues?
 
Back
Top Bottom