Uchaguzi 2020 Ubunge Arusha sasa upo wazi kwa Godbless Lema

Uchaguzi 2020 Ubunge Arusha sasa upo wazi kwa Godbless Lema

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

Mbio za ubunge katika jiji letu la Arusha sasa zipo wazi kabisa kiasi kwamba hata kipofu ni rahisi kujua na kufahamu nani atashinda ubunge.

Mara baada ya Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo kupitishwa na kamati kuu kugombea ubunge Arusha Mjini kulikuwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wanaCCM kindakindaki. Wengi walijiuliza kulikoni kamati kuu kupitisha jina la mgombea ambae tayari alishasemwa hadhani na mheshimiwa Rais na hata Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr Bashiru.

WanaCCM wengi walikubaliana pengine kamati Kuu iliangalia nani mwenye uwezo wa kushinda nafasi ya ubunge na kuviweka vigezo vingine kando ikiwemo tuhuma za rushwa, uchonganishi (kiwanja cha Msikiti Mkuu Bondeni), kukwamisha ujenzi wa stand mpya, kuhujumu ujenzi wa shule mbali mbali kwa kisingizio cha udogo wa viwanja na nk.

CCM iliamini na kujiaminisha kwamba Mrisho Mashaka Gambo angewavusha salama katika uchaguzi mkuu, hapakuwemo mgombea mwingine wa kumzidi yeye.

Katika hali ya kushangaza sana kama si kusikitisha Mrisho Gambo Mashaka amepwaya kweli kweli, zile amri zake za ukuu wa Mkoa hazifui dafu katika kuomba kura. Mrisho bila ngoma,mdundiko na wacheza show hawezi kufanya mkutano,Mrisho bila kukusanya watu toka kata mbali mbali za wilaya ya Arusha Mjini,Arumeru hawezi kufanya mkutano, Mrisho Gambo bila usaidizi wa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa hawezi kufanya mkutano. Mrisho Gambo yuko hoi bin taaban kisiasa na kiuchumi. Matajiri wengi wamejiweka kando na kampeni zake hawataki kutoa fedha tena wanamwangalia kama gari bovu.

Zipo tuhuma sijui zimetoka wapi, sijui nani kazianzisha zimesambaa kwa kasi ya ajabu juu ya kuungua soko la Samunge loooh hata kuandika naogopa soko la Samunge ni kaa la moto si mtaji tena wa Mrisho.

Update leo 17/09/2020.

Sasa ni dhahiri mpasuko mkubwa ndani ya CCM yapo makundi matatu makuu.

Kundi la Gambo ambalo linaungwa mkono na Mwenyekiti wa UWT na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kamanda Msatahafu Zelote Steven.Kundi hili lilihakikisha jina la Gambo linarudi pamoja na kugubikwa na tuhuma nyingi za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo kuwaweka mfukoni aliyekuwakuwa Mkuu wa TAKUKURU na RPC.Wakuu hawa wa vyombo vya dola walikuwa wakisimamia kwa karibu harakati zote za ushindi za Gambo.

Kundi la pili linaongozwa na Monaban,Kundi hili liliumizwa sana na Gambo wakati akiwa RC ikiwemo kuporwa biashara zake za nafaka (National Milling) kwa kisingizio alikuwa mtu wa E N Lowassa.Kwa hakika hapa ndipo kwenye mzizi mkubwa wa fitina.Monaban ana kundi kubwa sana nyuma yake.Huyu hakubali ahadi za kitoto anataka Gambo atupiliwe mbali.

Kundi la tatu ni Msando huyu alijaribu kujitutumua akajikuta anaangukia kukaa sero masaa kadhaa kwa makosa ya kugawa barakoa.Msando mwanasheria ni kundi lililoingia chamani kuunga juhudi za Mheshimiwa sana.Alipewa kazi ya kuhakiki mali za chama kazi ambayo ilikuja kumwingiza Dr Bashiru katika nafasi ya Katibu Mkuu.Ilitegemea baada ya kazi nzuri basi nafasi ya ubunge ilikuwa halali yake.

Kikao cha Mwisho cha Waziri Mkuu mstaafu Mizengo bado hakijaleta muunganiko chamani.

Naomba kuwasilisha.

Ngongo safarini Bukoba kwasasa nipo Katerero sokoni.
 
Umeandika yaani Mtu akisoma anasema Mrisho kaisha kweli. Hahahaha mwisho wa siku Mrisho anaibuka Kidedea kama ilivyokuwa kura za Wajumbe. Kishindo tu. Mrisho ndio Mbunge makini atakuwa
Unaota labda hujui siasa za Arusha na sisi ndo wananchi wa Arusha, Mrisho gambo asahau kabisa ubunge Arusha.
 
Wala usiogope , kuhusu soko la Samunge kuna tuhuma kwamba lilihujumiwa na Gambo ili apate nafasi ya kuchangia mabati kwa lengo la kupata kiki (ni kweli alitoa bati ) japo hakununua yeye bali yeye ndiye aliyejulikana katoa, hata hivyo hali imekuwa ngumu kiasi ambacho yasemekana anafikiria kujitoa
 
Wala usiogope , kuhusu soko la Samunge kuna tuhuma kwamba lilihujumiwa na Gambo ili apate nafasi ya kuchangia mabati kwa lengo la kupata kiki ( ni kweli alitoa bati ) japo hakununua yeye bali yeye ndiye aliyejulikana katoa , hata hivyo hali imekuwa ngumu kiasi ambacho yasemekana anafikiria kujitoa

Ni kweli Gambo anafikiria kujiondoa hasa baada ya wagombea wenzake ndani ya CCM kumsusa katika kampeni zake.Chama kimemkatalia kata kata lazima apambane mpaka mwisho kama kagundua kashindwa basi apambane kura za Rais.
 
Nipo Arusha, Mrisho Gambo anashinda saa 2 asubuhi, Lema anaulizwa alichofanya Arusha amekosa jibu, alishindwa hata kuwapa pole wana Samunge waliounguliwa na soko, kwa aibu ametunga uongo wa soko kuchomwa, Lema ana hali ngumu sana, safari hii anaondoka.
 
Ni kweli Gambo anafikiria kujiondoa hasa baada ya wagombea wenzake ndani ya CCM kumsusa katika kampeni zake. Chama kimemkatalia kata kata lazima apambane mpaka mwisho kama kagundua kashindwa basi apambane kura za Rais.
Kibaya kupita vyote inafahamika kwamba Gambo ndiye aliyetumika na jiwe kumkomoa Lema na kumsweka jela kwa miezi minne, wananchi wanaona kama Gambo ni gaidi.
 
Duniani hasa mataifa ya afrika kinapokaribia kipindi cha chaguzi mbalimbali kwenye haya mataifa, baadhi ya makundi huingiza pesa haramu kufadhili vyama ,au makundi mbalimbali ili yaunde serikali kwa makubaliano flaniflani yenye lengo la kuweka watu wao ambao watakua -remoted.

Fedha hizo huingizwa nchini si kwa ajili ya kufanyia kampeni ,bali hutumika kuandaa vikundi mbalimbali vya kihalifu kwa lengo la kufanya hujuma na mashinikizo flani yenye maslahi ya wachache na si kwa nchi husika .

Niipongeze serikali hasa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuliona hilo mapema sana .

Ifahamike vyama hasa vikubwa vya upinzani nchi kwa mujibu wa sheria vinapokea ruzuku kila mwezi, na pia huchangishana ,kazi ya fedha hizo ni pamoja na kuzitunza kwa ajili ya chaguzi mbalimbali ukiwemo na uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Inasikitisha kuona mgombea anatoka hadharani kulalamika ya kwamba pesa imezuiliwa kuingia nchini ,ooh! wafanyabiashara tuliokuwa tunawategemea wamehama nchi ,ni kina nani hao waliohama nchini ?na wanapodhamini uchaguzi nini matarajio yao kama si ukwepaji wa kodi?,

Suala la kujiuliza kwanini pesa hizo zije kipindi hiki cha uchaguzi ?,nani mfadhili wa hizo pesa ?anatarajia nini kwa anaowafadhili?,imani yangu kuna nia ovu dhidi ya taifa.

Uchaguzi ni mchakato wa muda mrefu wenye maandalizi ya kina yalioratibiwa kwa ustadi makini sana.

Namalizia kwa kusema wote ambao mnagombea dhamira zenu ni kujinufaisha binafsi na si taifa mtashindwa kwa aibu sana.
 
Back
Top Bottom