Uchaguzi 2020 Ubunge Arusha sasa upo wazi kwa Godbless Lema

Mzee wetu Waziri Mkuu mstaafu bado yuko Jijini Arusha akijaribu kuokoa Jahazi lisizame,lakini mpaka sasa hakuna matumaini wala hauweni.
 
acha kujidanganya, Makongoro alishinda kwa nguvu ya Lyatonga Mrema kipindi kile, Lema janashinda kwa nguvu ya CHADEMA kupendwa na wachaga, sasa hivi wana arusha wamebadilika, wanataka maendeleo, mbinu za Lema zimejulikana, ungemsikia Lema anavyolia lia kwenye mikutao utacheka, sasa ivi wamasai, waarusha, waislam t wote wanamsapoti gambo, lema hatoboi

..arusha hawana mambo ya ukabila.

..pale wanachagua watu machachari, watu wa amsha-amsha.

..nimekupa mfano wa Makongoro Nyerere, na Godbless Lema.

..Arusha wanapenda watu wenye haiba kama za hao hapo juu.

..mrisho gambo amepooza sana, ana aibu, hawezi siasa za majukwaani.
 
gambo alikaribisha madiwani 10 ccm kutoka chadema! huu mwaka cdm is loosing vyama vingine vinagain wanachama,
Unazungumzia wale walioenda kuunga mkono juhudi kwa ushawishi wa pesa? Sikujua kama kuna daydreamer, acheni hizo buku tano za Lumumba zinawafanya muonekane vituko
 
Gambo Ni aina ya wabunge wanaokwenda kusema ndio bungeni na kudhalilisha bunge tulirudi Yale ya ndugai, tupeleke watu matured bungeni
 
Heshima sana wanajamvi,

Mbio za ubunge katika jiji letu la Arusha sasa zipo wazi kabisa kiasi kwamba hata kipofu ni rahisi kujua na kufahamu nani atashinda ubunge.

Mara baada ya Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo kupitishwa na kamati kuu kugombea ubunge Arusha Mjini kulikuwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wanaCCM kindakindaki. Wengi walijiuliza kulikoni kamati kuu kupitisha jina la mgombea ambae tayari alishasemwa hadhani na mheshimiwa Rais na hata Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr Bashiru.

WanaCCM wengi walikubaliana pengine kamati Kuu iliangalia nani mwenye uwezo wa kushinda nafasi ya ubunge na kuviweka vigezo vingine kando ikiwemo tuhuma za rushwa, uchonganishi (kiwanja cha Msikiti Mkuu Bondeni), kukwamisha ujenzi wa stand mpya, kuhujumu ujenzi wa shule mbali mbali kwa kisingizio cha udogo wa viwanja na nk.

CCM iliamini na kujiaminisha kwamba Mrisho Mashaka Gambo angewavusha salama katika uchaguzi mkuu, hapakuwemo mgombea mwingine wa kumzidi yeye.

Katika hali ya kushangaza sana kama si kusikitisha Mrisho Gambo Mashaka amepwaya kweli kweli, zile amri zake za ukuu wa Mkoa hazifui dafu katika kuomba kura. Mrisho bila ngoma,mdundiko na wacheza show hawezi kufanya mkutano,Mrisho bila kukusanya watu toka kata mbali mbali za wilaya ya Arusha Mjini,Arumeru hawezi kufanya mkutano, Mrisho Gambo bila usaidizi wa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa hawezi kufanya mkutano. Mrisho Gambo yuko hoi bin taaban kisiasa na kiuchumi. Matajiri wengi wamejiweka kando na kampeni zake hawataki kutoa fedha tena wanamwangalia kama gari bovu.

Zipo tuhuma sijui zimetoka wapi, sijui nani kazianzisha zimesambaa kwa kasi ya ajabu juu ya kuungua soko la Samunge loooh hata kuandika naogopa soko la Samunge ni kaa la moto si mtaji tena wa Mrisho.

Naomba kuwasilisha.

Ngongo safarini Bukoba kwasasa nipo Katerero sokoni.
Pole sana kwa kuwa na misconstrued and misguided mawazo juu ya hiki kinyang'anyiro cha ubunge Jimbo la Arusha Mjini. Wewe subiri uone 28/10/2020. Mawazo na nadharia hasa hasa humu JF hayasaidii chochote.
 
Ile hospitali ya wanawake na watoto ambaye Lema alitaka kuanzisha kisha kufanyiwa figisu iliishia wapi?!

Yani ilisikitisha watu wengi maana watu toka mikoa mingine na nchi jirani wangekuja Arusha kupata huduma !

Yani swala lile liliwagusa watu wengi sana jamani !
 
Heshima sana wanajamvi,

Mbio za ubunge katika jiji letu la Arusha sasa zipo wazi kabisa kiasi kwamba hata kipofu ni rahisi kujua na kufahamu nani atashinda ubunge.

Mara baada ya Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo kupitishwa na kamati kuu kugombea ubunge Arusha Mjini kulikuwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wanaCCM kindakindaki. Wengi walijiuliza kulikoni kamati kuu kupitisha jina la mgombea ambae tayari alishasemwa hadhani na mheshimiwa Rais na hata Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr Bashiru.

WanaCCM wengi walikubaliana pengine kamati Kuu iliangalia nani mwenye uwezo wa kushinda nafasi ya ubunge na kuviweka vigezo vingine kando ikiwemo tuhuma za rushwa, uchonganishi (kiwanja cha Msikiti Mkuu Bondeni), kukwamisha ujenzi wa stand mpya, kuhujumu ujenzi wa shule mbali mbali kwa kisingizio cha udogo wa viwanja na nk.

CCM iliamini na kujiaminisha kwamba Mrisho Mashaka Gambo angewavusha salama katika uchaguzi mkuu, hapakuwemo mgombea mwingine wa kumzidi yeye.

Katika hali ya kushangaza sana kama si kusikitisha Mrisho Gambo Mashaka amepwaya kweli kweli, zile amri zake za ukuu wa Mkoa hazifui dafu katika kuomba kura. Mrisho bila ngoma,mdundiko na wacheza show hawezi kufanya mkutano,Mrisho bila kukusanya watu toka kata mbali mbali za wilaya ya Arusha Mjini,Arumeru hawezi kufanya mkutano, Mrisho Gambo bila usaidizi wa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa hawezi kufanya mkutano. Mrisho Gambo yuko hoi bin taaban kisiasa na kiuchumi. Matajiri wengi wamejiweka kando na kampeni zake hawataki kutoa fedha tena wanamwangalia kama gari bovu.

Zipo tuhuma sijui zimetoka wapi, sijui nani kazianzisha zimesambaa kwa kasi ya ajabu juu ya kuungua soko la Samunge loooh hata kuandika naogopa soko la Samunge ni kaa la moto si mtaji tena wa Mrisho.

Naomba kuwasilisha.

Ngongo safarini Bukoba kwasasa nipo Katerero sokoni.
Asante mkubwa kwa taarifa ya kuizika rasmi ccm kwa mara nyingine tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika yaani Mtu akisoma anasema Mrisho kaisha kweli. Hahahaha mwisho wa siku Mrisho anaibuka Kidedea kama ilivyokuwa kura za Wajumbe. Kishindo tu. Mrisho ndio Mbunge makini atakuwa.
Labda atakuwa mbunge kupitia jimbo la magogoni, siyo Arusha maana ccm ilishafutika kitambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ww upo arusha... Huyo mleta uzi mwenyewe hayupo arusha. Endeleeni kujifurahisha na kushangilia ushindi... Jana lema alikuwa na mkutano sinoni muulize alikuwa na watu wangapi....
I was born in Arusha na im still dwelling pia hali mnayoamibishana sivyo ilivyo
Wana Arusha hawawezi kuruhusu huu upuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaomuunga mkono gambo ni baadhi ya wafanya biashara wanaotaka kulindwa kwenye mambo yao ya gizani na baadhi ya wakazi wa uko chini muriet.Tena hao wakazi wenyewe wanahisi labda akiwa mbunge atasaidia yale maeneo kwabaadhi ya mambo ila kwakifupi Hakubaliki ata kidogo.
 
Arusha
IMG_20200918_140650.jpg
IMG_20200918_140710.jpg
 
Mkuu ww upo arusha... Huyo mleta uzi mwenyewe hayupo arusha. Endeleeni kujifurahisha na kushangilia ushindi... Jana lema alikuwa na mkutano sinoni muulize alikuwa na watu wangapi....
I was born in Arusha na im still dwelling pia hali mnayoamibishana sivyo ilivyo
Naona unaota wewe siyo bure, ccm Arusha ilishakufa kitambo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom