Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Thats what am talkin about!!!!!!!!!!!
Congrats sana CHADEMA kwa kufanya kweli, chama cha mafisadi taratibu kitatokomea

Ila inasikitisha kuwa wakati watanzania wa kawaida wasio na elimu huko Tarime wameamka lakini watanzania wanaojiita wamesoma na wana 'exposure' huko nje wako usingizi mzito kazi yao ni kufungua matawi ya CCM. Shame on you!!!!

Na dongo lingine liende kwa watu wa mijini hapa TZ hasa Dar, Arusha, Mwanza etc inasikitisha kuona hawa watu ndio wangeongoza kwa kuleta mabadiliko lakini cha ajabu hakuna hata mbunge mmoja wa upinzani sehemu hizo badala yake wananchi wa huko vijijini Karatu, Tarime, Mpanda, Kigoma kaskazini ndio wanaoleta mabadiliko

Mwisho kabisa ningependa kupingana na watu wanaowapigiaka kelele wapinzani eti nendeni vijijini mkajitangaze, ukweli unaonyesha kabisa watu wa vijijini ndio wana mwamko si wamjini, bananeni hapahapa mjini muwaondoe ujinga watu wanaokaa mijini kwa sababu wenyewe ndio wameshindwa kuleta mabadiliko

Wake up my brothers & sistaz
 
Sasa najiuliza! Pius Msekwa, Makamba, na utitiri wa mawaziri wote wa CCM waliokuwa kule na magari yao na helikopta mbili, na TOT na Komba mwenyewe na zile fulana na vikofia na waliofuatana nao wakakuwa wametumia pesa yetu kiasi gani? Kuna anayeweza kufanya mahesabu ya haraka hapa? Halafu tumuishe pia na gharama za kuwatibia wale walioumizwa kwenye hizi kampeni,gharama za kuweka jeshi kubwa la polisi.....na hivyo hivyo kwa Chadema, DP, na NCCR. La kujiuliza kweli tunahitaji kutumia mapesa yote haya kwa ajili ya chaguzi ndogo namna tulivyofanya. Bado hatujaweza kufikiria mishahara iliyoendelea kulipwa kwa mawaziri....ndiyo ilitakiwa siku ambazo hawafanyi kazi walizoajiriwa wasilipwe---wale wote waliokuwa Tarime walikuwa wanalipwa na vyama vyao, serikali haipasi kuwalipa kwani hawakuwa kazini....nawakilisha wanangu
 
Sasa najiuliza! Pius Msekwa, Makamba, na utitiri wa mawaziri wote wa CCM waliokuwa kule na magari ....

Walikwenda kupiga domo ili kupata kibali cha Rais kutuma Askari wa kuwatisha WanaTarime ili wapate nafasi ya kuiba kura.
 
Natamani sana kuiona sura ya Makamba leo hii,Tafadhali atakayefanikiwa kumnasa picha yake ya leo atuwekee hapa tupate burudani ya kuona sura ya mgosi wa ndima
 
Mgombea Kangoye wa CCM bado hatambui ushindi wenu.....

Tulieni kidogo. Msishangilie sana! Tunawamuulikaaaaaa!
 
Tarime mmetutoa kimasomaso! Let this be the turning point for Tz! Ushindi huu ni mtamu sana hata kama sina chama! Hongera wana JF kwa kukesha!
 
Hongereni wana Tarime

Hongereni uongozi mzima wa CHADEMA ukiongozwa na Komredi Mbowe
kwa mbinu kali mlizotumia

Wana tarime mmejiramba wale mafisadi wamemwaga fedha zao za ufisadi wakaangukia pua ooh tutawakatia laki 3 wapange matokeo lakini mkawa ngangari

Makamba utajiju kamwambie JK achague katibu mwingine

JIUZULU tu LUTENI
 
Uchaguzi huu umetufundisha mengi sana:

i) Wananchi wakiamua hakuna linaloshindikana. Huko Tarime wananchi walilishwa kila aina ya sumu, ikiwemo ghiliba na pesa nyingi lakini wameikataa CCM. Tumeshuhudia akina Makamba wakiwapa wananchi malaki na mamilioni ya shilingi. Lakini walichofanya watani zangu wa Tarime ni kukusanya hela zote walizopewa na akina Makamba na kwenda kununua pombe zote wakanywa usiku kucha. Akina Makamba kuona hivyo walikasirika mno na ndio ukawa mwanzo wa kuagiza mapolisi lundo kama tulivyoona. Walichotufundisha wana Tarime hapa ni kwamba hela ambazo CCM wanazimwaga wakati wa uchaguzi ni za kwetu ambazo wametuibia na kutunyang'anya, kwa hivyo tunaweza kuzipokea na bado hiyo isibadilishe nia yetu. Na pengine mtindo waliotumia wananchi wa Tarime ndio njia sahihi ya kukabiliana na uharamia wa CCM wa kutumia pesa katika uchaguzi.
ii) Tumefika turning point, kwa maana kwamba katika kila sehemu kuna watu wenye kutaka kuona haki inawepo. Tarime kulikuwa na majaribio mengi ya kutaka kubadilisha matokeo, lakini kuna baadhi ya watendaji ndani ya Halmashauri ya Tarime ambao walikuwa wanafanya kazi kwa niaba ya Tume walikataa kata, wakisema kuwa haki lazima itendeke. Hii ina maana kuwa kuna watendaji katika serikali hii ya ovyo ya CCM ambao kwa kweli wapo tayari kusimamia haki hata kama kufanya hivyo italeta matatizo kwenye vibarua vyao. Ni hatua ya namna hii iliyowezesha vyama vya upinzania huko Zambia, Malawi, na hata Kenya. Bila kuwa na watu wenye uchu wa haki ndani ya vyombo vya dola, itakuwa ngumu kuishinda CCM. Kwa sababu hiyo nachukua nafasi hii kuwashukuru sana watendaji mbalimbali wa Tume ya Uchaguzi huko Tarime waliohakikisha kuwa wanashinda majaribu na mashinikizo ya akina Makamba na kuhakikisha wana mtangaza mshindi kama walivyoamua wananchi.

iii) Tunawashukuru wana JF kwa changamoto na nasaha zenu, ambazo kwa kweli zimekuwa zinatusaidia sana kujifunza. Matokeo ya Tarime yametuchochea kufanya kazi ya siasa, na katika siku chache zijazo mtashuhudia viongozi wa chadema wakisambaa mikoani kwa ajili ya kazi ya kukisimika chama katika nyoyo za watanzania.

iv) Sasa hakuna shaka yeyote kuwa wenzetu NCCR wanafanya kazi ya kuisaidia CCM katika juhudi zao za kufifisha nguvu za upinzani. Mwanzo mimi binafsi nilikuwa mgumu kuamini kwamba NCCR wanafanya makusudi. Lakini sasa kwa matendo yao ya Tarime, na baada ya mimi mwenyewe kuongea na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hiki, nimekubali kabisa kwamba chama hiki hakipo kwa ajili ya kupambana na CCM. Hawa ni wachafuzi wanaofanya kazi maalumu ya kuua vuguvugu la mabadiliko katika nchi yetu. Kwa sababu hii nitakuwa mtu wa pili ndani (yupo aliyekwishanitangulia) ya chadema kupinga kwa nguvu zangu zote ushirikiano na NCCR. Kama kuna haja ya ushirikiano, basi ushirikiano huo uwe baina ya CHADEMA na CUF. Kwa maoni yangu hivi ndivyo vyama halisi vya upinzani Tanzania, ambayo vina strengths na weaknesses zake, kiasi kwamba kuungana kwao kutasaidia kupunguza weaknesses na kujiimarisha zaidi.

v) Uchaguzi huu umetukumbusha maadili halisi ya kitanzania, kwamba si utanzania kujaribu kujipatia umaarufu kupitia kwenye msiba. Sisi watanzania hutumia msiba kumaliza mitafaruku, sio kuikuuza. Wenzetu CCM, nafikiri kwa kufilisika kimawazo na kimikakati, waliamua kutumia msiba wa Wangwe kama njia ya kuimaliza CHADEMA Tarime. Wananchi, kwa kutumia common sense, sio madigrii, wamekataa ghiliba hizi. Imekuwa ni aibu kubwa. Wakajaribu kujenga propaganda kwamba Mbowe akienda Tarime atapigwa-lakini wamepigwa wao na Mbowe kapokelewa huko Tarime kuliko Malkia wa Uingereza alivyopokelewa wakati anapewa taji. Ni aibu kubwa.

Vi) Mwisho, niseme kwamba uchaguzi huu unaashiria mwisho wa siasa za ujanjaujanja. Siasa za akina Tambwe, Makamba na Akwilombe hazitawasaidia huko tuendako. Huko tuendako kinachotakiwa ni umakini, ukweli na uwezo. Blabla, longolongo na uongo unaoenezwa na akina Tambwe hauna tija. Anayeendelea kuwadanganya CCM kwamba umahiri wa kusema uongo ndio ushujaa katika siasa anawadanganya, na wajiandae kuumbuka zaidi huko tuendako. Kwa kuwasaidia, katika kujipanga upya, wawafukuze au wawape kazi nyingine akina Tambwe, Akwilombe na Makamba.
 
Tunashukuru Kitila kwa ujumbe wako uliosheheni busara. Kweli nimeamini CHADEMA ni chama makini.
 
Kama ni kweli CHADEMA mmeshinda, basi 'hongereni zenu'.

CCM tulishasema kuwa tutakubali matokeo.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Tawala
 
Silencer; this is good news; saa moto uwake mpaka 2010; hakuna kulala mpaka kieleweke ktk majimbo mengine; we expect kufikia wabunge 120 hivi toka kambi pinzani ili heshima ya matumizi ya hela walalahoi iweze kulindwa kwa heshima zaidi
 

THIS is very, very good news and the LESSON of the year for the OPPOSITION:

1. Anyone who sinks so LOW as to be used by the ruling party is finnished politically,
2. Police can be impartial and non-partisan for the good of all Tanzanians,
3. We need people who think with their heads and not hearts,
4. You can take someone bribe money and other goodies and yet vote against him,
5. Opposition makes a day for a many Tanzanians bewitched by CCM's songs of being the only part that can guard our unity and peace,
6. If we had 50 per cent opposition; and 50 per cent ruling party MPs things in Tanzania could change dramatically and the EPA's thieves will have been cornered and pay through their noses,

VIVA MULTI-PARTYISM, VIVA DEMOCRACY
 
FM ES uko wapi mkuu napenda sana hoja na changamoto zako, kulikoni umekuwa kimya sana ....
 
Kama ni kweli CHADEMA mmeshinda, basi 'hongereni zenu'.
CCM tulishasema kuwa tutakubali matokeo.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Kidumu Chama Tawala

Mkuu matokeo yameshakua rasmi kwamba Sisiem wameangukia pua....huna haja ya kupongeza huku umeweka kama.....
ALLOW ME TO SAY LOUDLY: 'HONGERENI CHADEMA...HAKIKA MLISTAHILI KUSHINDA!'
 
Thats what am talkin about!!!!!!!!!!!
Congrats sana CHADEMA kwa kufanya kweli, chama cha mafisadi taratibu kitatokomea

Ila inasikitisha kuwa wakati watanzania wa kawaida wasio na elimu huko Tarime wameamka lakini watanzania wanaojiita wamesoma na wana 'exposure' huko nje wako usingizi mzito kazi yao ni kufungua matawi ya CCM. Shame on you!!!!

Na dongo lingine liende kwa watu wa mijini hapa TZ hasa Dar, Arusha, Mwanza etc inasikitisha kuona hawa watu ndio wangeongoza kwa kuleta mabadiliko lakini cha ajabu hakuna hata mbunge mmoja wa upinzani sehemu hizo badala yake wananchi wa huko vijijini Karatu, Tarime, Mpanda, Kigoma kaskazini ndio wanaoleta mabadiliko

Mwisho kabisa ningependa kupingana na watu wanaowapigiaka kelele wapinzani eti nendeni vijijini mkajitangaze, ukweli unaonyesha kabisa watu wa vijijini ndio wana mwamko si wamjini, bananeni hapahapa mjini muwaondoe ujinga watu wanaokaa mijini kwa sababu wenyewe ndio wameshindwa kuleta mabadiliko

Wake up my brothers & sistaz
Hongerini sana wana CHADEMA ni mwanzo nzuri.

Watu wa mijini wengi ni wafanyakazi na wafanyabiashara. Tatizo tunajifanya tupo busy kupanga foleni ya kupiga kura.

Natoa wito kwa wenzangu tujiandikishe na pia kushishiriki kupiga kura. Kila mtu yupo busy. Naamini mabadiliko yatatokea tu!

Tusibaki tukilaumu tu! Rafiki yangu aliniuliza mbona wasomi mnatawaliwa na mbunge form gani sijui. Nikajua watu hawajaamua.

Ukiaangalia chama tawala kina angalia waliojiandikisha na sio kuwa na umati mkubwa kwenye mkutano halafu waliojiandikisha ni wachache.[/COLOR][/COLOR]
 
Mgombea Kangoye wa CCM bado hatambui ushindi wenu.....

Tulieni kidogo. Msishangilie sana! Tunawamuulikaaaaaa!

Mkuu Huu ushindi sio wa kubahatisha. Furaha lazima iwepo to the fullest. Yeye mwache aendelee kuhangaika tu hii sio ishu kama ya zim au Kenya.
kwamba matokeo yatabadilika.
We need to show our confidence on what we have achieved otherwise unaweza ukakandamizwa hivivi maana jamaa watasema
mura jamaa hana uhakika kama kashinda

Chadema Oyeeeeeeeeeee

Dare to Ask for Your Right. Unless you will never Get IT
Mapinduzi yanaendela
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom