Ubungo mataa: Trafiki agongwa na pikipiki akikimbilia kusimamisha lori

Hawa watu ni shida sana, wanatakiwa kujirekebisha mana wameshaweka uadui kati yao na watu wanaomiliki vitu vya moto
Boda boda wana bifu mpaka na watoto wa shule.sembuse traffic!!!

Angegongwa na semi,labda ungeeleweka.
 
Kumbuka huyo askari ana mke na watoto, hatujafika huko kuombeana mabaya, Yesu alitupenda kama jinsi tulivyo, Mungu angeangalia maovu Yetu hakika hamna ambaye Angepona, tuombeana badala ya kuchukiana
Kwa kawaida ukiona mtu anafurahia mabaya yamkute mwingine,ana ushetani mwingi sana chini ya moyo wake umejaa.

Binaadam msafi wa moyo haijalishi kaumizwaje,ila mbaya wake yakimfika ya kuliza naye hulia pia.
 
Reactions: Cyb
Hapendwi kila mtu anafurahi kilichompata
Then kesho yake anakuja traffic mwingine hapo,kazi inaendelea.

Umasikini unaharibu akili,hata ukijikwa utahisi jiwe linakusababishia njaa,wakati hauko makini kutembea.
 
Hukuvuka taa nyekundu na ukabambikiwa kesi,mara ngapi hili limekupata mpaka useme hutasamehe traffic yeyote??

Maana kama ni mara moja,bahati mbaya ungesamehe,mara kwa mara basi una gundu.kwanini wewe tu!!
 
Halafu jamaa alipaa na ndege au[emoji16][emoji16][emoji16]

Kuna hasira hasara,halafu hasira za mkizi.
 
Then kesho yake anakuja traffic mwingine hapo,kazi inaendelea.

Umasikini unaharibu akili,hata ukijikwa utahisi jiwe linakusababishia njaa,wakati hauko makini kutembea.
Hakuna watu wanaojiona wamefanikiwa mno kama wale ambao wanaokaa kwenye daladala seat ya mbele.

Bilashaka mkuu utakua ni mpanda daladala tena unapendaga kukaa Ile seat pale.

Hizi comment zako zinaonesha wewe ni wakupanda daladala, sometimes Bora ukae kimya tu Maana kidogo nitoe tusi.

Ungekua karibu hapa ningekupa konzi la utosi.
 
Jamaa wanapiga mkono hadi kwenye hiyo highway ya Kimara <> Kibaha...
πŸ€” Hyaani hata Mimi nawashangaa Sana Hawa traffic, ile ni high way lakini wamo tu, na hakuna wa kuwakemea ,πŸ™„
 
Pole sana Trafiki, Mungu atakuponya haraka urejee kwenye majukumu yako ya kila siku.
 
πŸ€” Hyaani hata Mimi nawashangaa Sana Hawa traffic, ile ni high way lakini wamo tu, na hakuna wa kuwakemea ,πŸ™„

Nani wa kuwakemea mkuu wakati wametumwa hesabu
 

Maisha mafupi mno mkuu,acha mtu afurahie kile anaweza kukifanya.

Wewe utanunua subaru ufunge muffler ya makelele,ndani ina mziki mkubwaa.lakini kwa wengi huu ni upuuzi,na hawezi mtu kukwambia,japo unadhani unakuwa umetisha ile mbaya.

Dala dala napanda sana mkuu,mpaka zingine najitambulisha kama staff.
 
Reactions: Cyb
Ni tukio la Kusikitisha ila linachekesha sana na nimejikuta ninacheka mno hasa uliposema baada ya Kugongwa huko na Pikipiki akaamka na kusimamisha Lori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…