Ahmed Saidi
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 1,588
- 3,487
- Thread starter
- #101
Umeongea vizuri sana ndugu, hili liko wazi kabisa. Mimi nadhani vijana ambao wamefanya vizuri chuoni wawezeshwe ili wajiendeleze kielimu. Unakuta mtu kapata GPA ya juu kabisa, lakini haendelezwi, vyuo havitoi hata interns. Kwa kuuza nyanya na dagaa kwakweli siwezi kuafford kusoma postgraduate studies.Nakuunga mkono mkuu.
Mimi nilifanya interview (Tutorial Assistant) Mzumbe Morogoro mwezi Agosti ila sikufanikiwa kuitwa ajili ya Oral interview. Tuliokuja kwa ajili ya nafasi za Tutorial Assistants tulikuwa wengi kila kozi (20+, 100+ na wengine 200+ kwa ajili ya nafasi 2 tu). Ila waliokuja kwa ajili ya interviews za Assistant Lecturers walikuwa wachache sana (3, 5, 10, nk). Katika kozi moja ya masters, alikuja mmoja tu kufanya interview kwa ajili ya nafasi ya Assistant Lecturer - sikumbuki kama alifanikiwa kupita au la.
Hivi karibuni nimesikia kuwa Mzumbe iliwachukua wote waliokuja kwa ajili ya interview (nadhani ni Assistant Lecturers) kule kwenye campus yao ya Dar es Salaam.
Sijui kwa nini serikali haiwaruhu basi hata vyuo vyenyewe viwe na mandate ya kuajiri Tutorial Assistants (iwe ni part time au full time, iwe ni volunteering, contract au permanent, nk).
Best students tupo tu mtaani tunapambana na hali zetu. Nadhani kwa hali hii, GPA za wanafunzi zitaanza kushuka (kwani siku hizi continuing students wanatuona sisi graduates wengi tuna 3.8+ GPAs lakini hazina maana kwani ajira serikalini adimu na hata tukiitwa kutoboa ni ngumu sana). Tunapoelekea sasa tutaanza kuwa kama Nigeria (vyuo vyingi, students wengi, graduates wengi ila ajira chache sana).
Licha ya watu kufeli interviews hizi, lakini sababu kubwa ya kuwa re-advertized ni uchache wa waombaji kwa wale wenye masters na PhD. Amini maneno yangu vyuo vingi ambavyo bado havijatoa placement, vitatangaza upya nafasi Kwa masters na PhD holders.
Bado mamlaka hazijachelewa, huu ni muda wakuwaendeleza vijana waliomaliza shahda za awali na kufaulu vizuri ili kukabiliana na uhaba huu.