Uchache wa Waombaji Kazi kwa Post za Assistant lecturers

Uchache wa Waombaji Kazi kwa Post za Assistant lecturers

Ni kweli kabisa. Ila sijiskii amani kufanya hiyo kazi ya ulecturer. Amani ipo kwenye biashara zaidi na siasa.
Nimepewa tender ya kusupply unga wa muhogo non food grade tani 300 na price ni 700,000/= per tone price at factory gate.

Tuchangamkie au wewe unataka biashara gani?
 
Kwa mliosomea fani za educational psychology, educational guidance and counseling, special and inclusive education, early childhood education Hadi masters level hizo nafasi Bado zinakosa wajazaji wa nafasi
 
Screenshot_20221110-175404~2.jpg
hizi nafasi zitakuwa re-advertized sana tu
 
Katika hangaika yangu ya kusaka tonge hasa katika hizi interviews za utumishi, nimegundua Kuna baadhi ya post huwa hazina waombaji wengi. Nitachukulia mfano kwa post za educational psychology, Guidance and counseling, early childhood education & special and inclusive education na fani nyengine kwa level ya Assistant lecturers

Walioomba nafasi za assistant lecturer katika baadhi ya vyuo ni walewale tena ni wachache mno. Unakuta watu wawili au watatu tena ni walewale wameomba hiyo nafasi UDSM, UDOM, SUA, DUCE, MUCE, MUHAS, IAE, ADEM n.k tena Mara kadhaa unakuta watu hao hao wapo kwenye Educational psychology, guidance and counseling, special and inclusive education na kupelekea mtu kuchaguliwa vyuo 4 Hadi 5 katika fani zaidi ya moja ambapo muombaji akiconfirm fani au chuo kimoja, fani au vyuo vyengine vinakosa watu na hapa ndio unakuta nafasi nyingi zinakuwa re-advertized.

Wakati huo huo wanaoomba nafasi hizo kama Tutorial Assistant ni wengi sana. Hivi kwanini mamlaka husika wasijikite kuajiri sana kuanzia Tutorial Assistant?

Ukizingatia pia watoto wengi wa masikini hawawezi kumudu masomo ya postgraduate.
Nakuunga mkono mkuu.

Mimi nilifanya interview (Tutorial Assistant) Mzumbe Morogoro mwezi Agosti ila sikufanikiwa kuitwa ajili ya Oral interview. Tuliokuja kwa ajili ya nafasi za Tutorial Assistants tulikuwa wengi kila kozi (20+, 100+ na wengine 200+ kwa ajili ya nafasi 2 tu). Ila waliokuja kwa ajili ya interviews za Assistant Lecturers walikuwa wachache sana (3, 5, 10, nk). Katika kozi moja ya masters, alikuja mmoja tu kufanya interview kwa ajili ya nafasi ya Assistant Lecturer - sikumbuki kama alifanikiwa kupita au la.
Hivi karibuni nimesikia kuwa Mzumbe iliwachukua wote waliokuja kwa ajili ya interview (nadhani ni Assistant Lecturers) kule kwenye campus yao ya Dar es Salaam.

Sijui kwa nini serikali haiwaruhu basi hata vyuo vyenyewe viwe na mandate ya kuajiri Tutorial Assistants (iwe ni part time au full time, iwe ni volunteering, contract au permanent, nk).
Best students tupo tu mtaani tunapambana na hali zetu. Nadhani kwa hali hii, GPA za wanafunzi zitaanza kushuka (kwani siku hizi continuing students wanatuona sisi graduates wengi tuna 3.8+ GPAs lakini hazina maana kwani ajira serikalini adimu na hata tukiitwa kutoboa ni ngumu sana). Tunapoelekea sasa tutaanza kuwa kama Nigeria (vyuo vyingi, students wengi, graduates wengi ila ajira chache sana).
 
Vijana mjiajiri, mkumbuke hata hivyo vyuo ni mali za watu
Dada ungefaa sana uwe Assistant Lecturer chuoni. Haiwezekani nafasi zinakuwa re-advertised hadi mara 3 halafu watu kama nyie hamna mpango kabisa hata kuja ku'apply huko mbeleni. Endelea kufanya biashara zako na kuwaajiri watu ila nafasi za chuoni zikitokea sio vibaya ku'apply.
Vyuo ni mali za watu lakini watu hao hawafanyi jitihada zozote kubadilisha sera na mifumo iliyopo sasa. Watu kama nyie mkiingia huko mnaweza mkafanyika chachu ya kuleta mabadiliko halisi ndani ya miaka michache.

Vijana tunawahitaji, mkumbuke hata hivyo baadhi ya watoto wenu au wa ndugu zenu wanategemea kupata ajira vyuoni.
 
Back
Top Bottom