Uchache wa Waombaji Kazi kwa Post za Assistant lecturers

Umeongea vizuri sana ndugu, hili liko wazi kabisa. Mimi nadhani vijana ambao wamefanya vizuri chuoni wawezeshwe ili wajiendeleze kielimu. Unakuta mtu kapata GPA ya juu kabisa, lakini haendelezwi, vyuo havitoi hata interns. Kwa kuuza nyanya na dagaa kwakweli siwezi kuafford kusoma postgraduate studies.

Licha ya watu kufeli interviews hizi, lakini sababu kubwa ya kuwa re-advertized ni uchache wa waombaji kwa wale wenye masters na PhD. Amini maneno yangu vyuo vingi ambavyo bado havijatoa placement, vitatangaza upya nafasi Kwa masters na PhD holders.

Bado mamlaka hazijachelewa, huu ni muda wakuwaendeleza vijana waliomaliza shahda za awali na kufaulu vizuri ili kukabiliana na uhaba huu.
 
Hao IFM na wenzake sio vyuo vikuu.
 
Basi hali ni mbaya sana.

Kuna tangazo moja la usaili la UDSM niliona jina la mtu mmoja limejirudia (yuko peke yake) kwa nafasi za assistant lecturer wa kada ya micro economics, fisheries economics pamoja na energy economics.

Kwahiyo kabla hata interview haijaanza maana yake nafasi mbili kati ya hizo tatu imeshakosa mtu na itakua re-advertised.

Kuna uhaba wa watu wa aina hii kwa kweli kama ulivyosema
 
Unajua kipindi cha nyuma, hii miaka mitano iliyopita msukumo wa watu kusoma postgraduate ulikuwa ni mdogo sana ukizingatia ajira zilikuwa chache sana.

Si rahisi mtu kusoma masomo hayo wakati uhakika wa ajira hakuna. Kwaiyo sasahivi nafasi zimekuwa nyingi lakini waombaji hamna.

Labda kama wakimua kuanza kuajiri watu wenye bachelor's degree
 
Ilikuwa ngumu kweli maana ukasome wakati hata bachelor hujaona ilipokupeleka popote na nafasi hazikuwa zikitoka
 
Ilikuwa ngumu kweli maana ukasome wakati hata bachelor hujaona ilipokupeleka popote na nafasi hazikuwa zikitoka
Yeah, Mimi nimejiunga zamani ajira portal lakini ndio Kwanza mwaka huu nmeona nafasi ktk field yangu
 
Miaka ya nyuma ilikuwa inakatisha sana tamaa aseeh
Aliesoma Hadi master na aliefeli darasa la 7 wote sawa. Kama recruitment itafanyika hivi miaka yote, naamini hali itatengemaa miaka michache mbeleni
 
Aliesoma Hadi master na aliefeli darasa la 7 wote sawa. Kama recruitment itafanyika hivi miaka yote, naamini hali itatengemaa miaka michache mbeleni
Yes inatakiwa waendelee hivi kwa miaka kama 7 hivi ndo hali itanormalize
 
Kweli, limekuja kuwa tatizo hili. Wangeendelea na ule utaratibu wa zamani wa kuwajengea uwezo wale wanaohitimu wakiwa vema na wanaipenda fani. Wakimaliza wafanyiwe usahili, waendelee kutumikia nafasi ya TA baadae wajiendeleze. Hili tatizo lisingalikuwepo.
Saiv Bachelor degrees ni nyingi mno kuliko levels zingine.
 
Na zinaendelea kuwa nyingi kila siku
 
BS mnajitetea mkasome masters huko mpate qualifications. Kuna kazi hata huwa sizishobokei ni Pamoja na kufundisha. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…