Uchache wa Waombaji Kazi kwa Post za Assistant lecturers

Uchache wa Waombaji Kazi kwa Post za Assistant lecturers

Ahmed Saidi

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2019
Posts
1,588
Reaction score
3,487
Katika hangaika yangu ya kusaka tonge hasa katika hizi interviews za utumishi, nimegundua Kuna baadhi ya post huwa hazina waombaji wengi. Nitachukulia mfano kwa post za educational psychology, Guidance and counseling, early childhood education & special and inclusive education na fani nyengine kwa level ya Assistant lecturers na lecturers

Walioomba nafasi za assistant lecturer katika baadhi ya vyuo ni walewale tena ni wachache mno. Unakuta watu wawili au watatu tena ni walewale wameomba hiyo nafasi UDSM, UDOM, SUA, DUCE, MUCE, MUHAS, IAE, ADEM, MNMA, MZUMBE n.k tena Mara kadhaa unakuta watu hao hao wapo kwenye Educational psychology, guidance and counseling, special and inclusive education na kupelekea mtu kuchaguliwa vyuo 4 Hadi 5 katika fani zaidi ya moja ambapo muombaji akiconfirm fani au chuo kimoja, fani au vyuo vyengine vinakosa watu na hapa ndio unakuta nafasi nyingi zinakuwa re-advertized.

Wakati huo huo wanaoomba nafasi hizo kama Tutorial Assistant ni wengi sana. Hivi kwanini mamlaka husika wasijikite kuajiri sana kuanzia Tutorial Assistant?

Ukizingatia pia watoto wengi wa masikini hawawezi kumudu masomo ya postgraduate.
 
3.5? Watu hawaombi wanajua wenyew
Wengi wanapata zaidi ya hiyo, hata mimi nikiwa mmoja wao miaka yetu ya 2011 UDSM na baadhi ya study year mates na hatukuwahi kuwaza nafasi za TA sababu kubwa ni kipindi kile taasisi na NGO's mbalimbali zilikuwa zinatufuata chuoni kabla hatujamaliza. Kwasasa sijui kama hii kitu bado ipo
 
Wengi wanapata zaidi ya hiyo, hata mimi nikiwa mmoja wao miaka yetu ya 2011 UDSM na baadhi ya study year mates na hatukuwahi kuwaza nafasi za TA sababu kubwa ni kipindi kile taasisi na NGO's mbalimbali zilikuwa zinatufuata chuoni kabla hatujamaliza. Kwasasa sijui kama hii kitu bado ipo
Matabulalasa ndio wanabakia chuo
 
Sio kila chuo kinaweza fanya mchakato wa kuajir TA labda kwa sababu ya cost ya kuwasomesha badae , lakini pia policy , objective na strategies lakini pia Kuna vyuo vinatoa internship kwa TA lakini sio kuwapa ajira kabisa
Sasa ndio vinakosa watu na nafasi zinakuwa readvertised kila siku
 
Masters yaki ni added advantage ila undergraduate uwe na 3.9+ kama una less than3.9 unakosa sifa za hata shortlist hata kama masters una first class😅😅😅
Nakumbuka kipindi nikiwa idara ya uchumi UDSM hata masters ni lazima upate GPA ya 4.0+. kazi za kufundisha ni lazima ufaulu ngazi zote isipokuwa Ph.D ambayo ni pass tu.
 
Back
Top Bottom