Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzangu,
Inasemekana ndoto za makamu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zinazidi kuyayuka kama chumvi ndani ya maji baada ya kuanza kusoma alama za nyakati, na kusikia tetesi kutoka kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya chama chake, wakidai kwamba kuna mpango unasukwa na genge la aliekuwa katibu mkuu wa chama hicho na ambae aliwahi kuwa balozi wa Tanzania huko ukubwani, ili aweze kurudi katika chama hicho na hatimae aweze kupeperusha bendera ya mgombea uraisi wa chama hicho ifikapo mwaka 2025.
Inasemekana genge hilo linalojiita "chadomo asili" limekuwa likifanya maongezi ya siri na boss wa chama hicho ili amruhusu mzee huyo kurudi chamani, na hatimae kugombea uraisi. Ikumbukwe kuwa boss wa chama hicho na makamu wake wanaishi kwa kutoaminiana muda mrefu, ndio maana hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, mgombea uraisi wa chama hicho ambae ndio huyo makamu wa chama alinusurika kutupwa nje ya kinyang'anyiro na boss wake, ili ampitishe mgombea aliemtaka yeye ambae alikuwa akijulikana kwa jina Lazara Nyalanda.
Ila kelele za baadhi ya watu, haswa wanachama wa mitandaoni ndio zilizomfanya boss huyo abadili muelekeo wa maamuzi yake, na hatimae kumpitisha ndugu makamu kwa shingo upande.
Sasa safari hii kuna uwezekano mkubwa wa kumchinjia mbali makamu, ukizingatia ataempitisha safari hii atakuwa na baraka zote za chama kutokana na historia kubwa aliyonayo chamani na pia mzee huyo ndio anaeaminika kuwa ni raisi wa mioyo yao.
Hizi kelele zote zinazojitokeza sasa hivi kutoka kwa mzee huyo, ni mpango mahususi uliopangwa na boss ili kuwaandaa wanachama wao kusaikolojia. Kwani ataporudi chamani itakuwa ngumu kumpinga kutokana aina ya mapambano yake katika siasa.
2025 mzee huyo atapitishwa na makamu atarudi ubeberuni kwa mabeberu kwa hasira na aibu.
Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja.