Uchaguzi 2025, huyu mzee anazidi kumtia makamu tumbo joto

Habari zenu wana JF wenzangu,

Inasemekana ndoto za makamu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zinazidi kuyayuka kama chumvi ndani ya maji baada ya kuanza kusoma alama za nyakati, na kusikia tetesi kutoka kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya chama chake, wakidai kwamba kuna mpango unasukwa na genge la aliekuwa katibu mkuu wa chama hicho na ambae aliwahi kuwa balozi wa Tanzania huko ukubwani, ili aweze kurudi katika chama hicho na hatimae aweze kupeperusha bendera ya mgombea uraisi wa chama hicho ifikapo mwaka 2025.

Inasemekana genge hilo linalojiita "chadomo asili" limekuwa likifanya maongezi ya siri na boss wa chama hicho ili amruhusu mzee huyo kurudi chamani, na hatimae kugombea uraisi. Ikumbukwe kuwa boss wa chama hicho na makamu wake wanaishi kwa kutoaminiana muda mrefu, ndio maana hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, mgombea uraisi wa chama hicho ambae ndio huyo makamu wa chama alinusurika kutupwa nje ya kinyang'anyiro na boss wake, ili ampitishe mgombea aliemtaka yeye ambae alikuwa akijulikana kwa jina Lazara Nyalanda.

Ila kelele za baadhi ya watu, haswa wanachama wa mitandaoni ndio zilizomfanya boss huyo abadili muelekeo wa maamuzi yake, na hatimae kumpitisha ndugu makamu kwa shingo upande.

Sasa safari hii kuna uwezekano mkubwa wa kumchinjia mbali makamu, ukizingatia ataempitisha safari hii atakuwa na baraka zote za chama kutokana na historia kubwa aliyonayo chamani na pia mzee huyo ndio anaeaminika kuwa ni raisi wa mioyo yao.

Hizi kelele zote zinazojitokeza sasa hivi kutoka kwa mzee huyo, ni mpango mahususi uliopangwa na boss ili kuwaandaa wanachama wao kusaikolojia. Kwani ataporudi chamani itakuwa ngumu kumpinga kutokana aina ya mapambano yake katika siasa.

2025 mzee huyo atapitishwa na makamu atarudi ubeberuni kwa mabeberu kwa hasira na aibu.

Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja.
Hoja hapa Bandari yetu hatutaki iuzwe. Period
 
MKUU HII SIO JAMII FORUM NINAYOIJUA MIMI.

kutoka Great thinkers Hadi kuwa Hivi mbona ni aibu sana!!!!!!!!

Unajisikiaje kuandika jambo la Kipuuzi na kijinga kama hili???????????

ANDIKA KITU AMBACHO KITAWASAIDIA WATANZANIA KUJIEPUSHA NA UMASIKINI , UJINGA MARADHI NA UKOSEFU WA AJIRA.

JITAFAKARI.
Mkuu yaani Wapumbavu wanazidi kuongezeka., bora hata zamani tulikuwa na wajinga na siyo hawa wapumbavu.
 
CHADEMA sio ACT hii ni CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO KWAKIFUPI CHADEMA
Haya mkuu tusiandikie mate na wino upo. Hata 2015 kuna watu walipinga na wengine kuweka dau la nyumba zao kwamba chadema hakiwezi kufanya kosa la kumkaribisha fisadi chamani.

Lakini mwisho wa siku watu walipewa mpunga wakampokea na kumpitisha fasta fasta bila hata kutumia mchujo.
 
Obviously Dr Slaa ndo chaguo la Pengo pale Chadema since wamefanya kazi pamoja Slaa alipokuwa katibu Baraza la maaskofu...

But chaguo halisi la Pengo ni Philip Mpango....ndo maana Philip Mpango kakaa kimyaa kuhusu Bandari Kwa maagizo ya Pengo...Slaa atatumika Tu kuwatisha Ccm ..mradi ikiwezekana wamchague Philip Mpango...hapo Slaa atamuachia Lissu..agombee huku anasubiri teuzi Kwa Ccm
🤣🤣🤣🤣
 
Hoja hapa Bandari yetu hatutaki iuzwe. Period
Hoja ya bandari kwa sasa haina maana kwa sababu mods wameamua kuziunganisha thread zote zinazohusu bandari pamoja, kutokana na walalamikaje wengi kutokuwa na uwezo wa kuandika hoja zinazoeleweka, na mbaya zaidi ni kutumiwa na wajanja wachache wanaonufaika na mfumo mbovu wa bandari sasa hivi, kama vile wazee wa kukwepa kulipa ushuru wa bandarini, wezi wa vifaa mbali mbali pale bandarini, wapitisha madawa ya kulevya na vishoka wao.
 
Habari zenu wana JF wenzangu,

Inasemekana ndoto za makamu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zinazidi kuyayuka kama chumvi ndani ya maji baada ya kuanza kusoma alama za nyakati, na kusikia tetesi kutoka kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya chama chake, wakidai kwamba kuna mpango unasukwa na genge la aliekuwa katibu mkuu wa chama hicho na ambae aliwahi kuwa balozi wa Tanzania huko ukubwani, ili aweze kurudi katika chama hicho na hatimae aweze kupeperusha bendera ya mgombea uraisi wa chama hicho ifikapo mwaka 2025.

Inasemekana genge hilo linalojiita "chadomo asili" limekuwa likifanya maongezi ya siri na boss wa chama hicho ili amruhusu mzee huyo kurudi chamani, na hatimae kugombea uraisi. Ikumbukwe kuwa boss wa chama hicho na makamu wake wanaishi kwa kutoaminiana muda mrefu, ndio maana hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, mgombea uraisi wa chama hicho ambae ndio huyo makamu wa chama alinusurika kutupwa nje ya kinyang'anyiro na boss wake, ili ampitishe mgombea aliemtaka yeye ambae alikuwa akijulikana kwa jina Lazara Nyalanda.

Ila kelele za baadhi ya watu, haswa wanachama wa mitandaoni ndio zilizomfanya boss huyo abadili muelekeo wa maamuzi yake, na hatimae kumpitisha ndugu makamu kwa shingo upande.

Sasa safari hii kuna uwezekano mkubwa wa kumchinjia mbali makamu, ukizingatia ataempitisha safari hii atakuwa na baraka zote za chama kutokana na historia kubwa aliyonayo chamani na pia mzee huyo ndio anaeaminika kuwa ni raisi wa mioyo yao.

Hizi kelele zote zinazojitokeza sasa hivi kutoka kwa mzee huyo, ni mpango mahususi uliopangwa na boss ili kuwaandaa wanachama wao kusaikolojia. Kwani ataporudi chamani itakuwa ngumu kumpinga kutokana aina ya mapambano yake katika siasa.

2025 mzee huyo atapitishwa na makamu atarudi ubeberuni kwa mabeberu kwa hasira na aibu.

Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja.
Uharo
 
Mkuu yaani Wapumbavu wanazidi kuongezeka., bora hata zamani tulikuwa na wajinga na siyo hawa wapumbavu.
Vipi mlioambiwa Lowasa fisadi na bado 2015 mkampigia deki na kumpa kura awe raisi?
Wapumbavu au wajinga?
 
Obviously Dr Slaa ndo chaguo la Pengo pale Chadema since wamefanya kazi pamoja Slaa alipokuwa katibu Baraza la maaskofu...

But chaguo halisi la Pengo ni Philip Mpango....ndo maana Philip Mpango kakaa kimyaa kuhusu Bandari Kwa maagizo ya Pengo...Slaa atatumika Tu kuwatisha Ccm ..mradi ikiwezekana wamchague Philip Mpango...hapo Slaa atamuachia Lissu..agombee huku anasubiri teuzi Kwa Ccm
Pengo ana nguvu kuliko chama chenu?
 
Back
Top Bottom