Uchaguzi 2025, huyu mzee anazidi kumtia makamu tumbo joto

Msihamishe magoli,bandari zetu bandari zetu bandari zetuuuuuuuuuuu
Bandari mbona wanaopigania matumbo yao, wakwepa ushuru na kodi bandarini, wapitisha madawa ya kulevya, vishoka na wauza vifaa vya magari yaliopo bandarini washaanza kusalenda baada ya amiri jeshi mkuu kuwashtukia na kuwapuuza kitambo.

Labda mmebaki nyinyi mliolaghaiwa ili mpambane kwa ajili yao na familia zao. Kwa kisingizio cha uzalendo uchwara unaowafaidisha wao tu, huku wewe ukiwa huna unachofaidika nacho kupitia bandari.
 
Muhimu kwanza ni bandari mkuu mengine yoote ni baadae. Bandari ikienda tumepigwa mande hamtaamini.
Bandari.. 100% ya watanzania tumezaliwa na kuona au kusoma katika vitabu tu kuwa nchi yetu ina bandari kubwa Afrika Mashariki.

Lakini kiukweli bandari hiyo inanufaisha 1% tu, ya wajanja wanaopiga kelele mitandaoni kuhusu bandari. 99% ya watanzania waliobaki ikiwemo mimi na wewe hatujawahi kufaidika na chochote kinachoingia wala kutoka bandarini.

Kwa sisi ambao tushafika bandarini mara nyingi tunajua ni kwanini kuna kundi dogo la wakwepa kodi na ushuru linapiga kelele, tunajua ni kwanini kuna wapitisha madawa ya kulevya bandarini na wezi wa vifaa vya magari bandarini linapiga kelele, tunajua ni kwanini wahujumu uchumi pale bandarini wamegawa pesa kwa baadhi ya watu wenye ushawishi na uwezo wa kudanganya nyumbu wamehongwa ili kusaidia wahujumu hao kupiga kelele.

Pengine wewe umeunga tela tu bila kupewa hata senti tano kwa kigezo cha uzalendo uchwara huku wenzako wakinufaika na mfumo mbovu uliyopo bandarini sasa hivi.

Unafika bandarini unakuta mtu ana tumbo kama fuko la dagaa, ana majumba yasiokuwa na idadi afu wewe unaetaka bandari iendelee kubaki katika mikono yao kwa kigezo cha uzalendo unashindwa kupata hata hela ya kulipa chumba unachopanga.

Nonsense.
 
Kubwabwaja kwao kusikuhadae ukaendelea kutumiwa kama daraja kwa faida zao na familia zao. Shtuka ndugu.
Wewe ninakufahamu kwa 'utaahira' siku nyingi humu JF; kwa hiyo kujibishana nawe ni luxury tu ya kupotezea muda!
Hebu kwa mfano angalia haya uliyoandika hapa chini. Ni kama mtu ambaye hana kichwa kabisa chenye ubongo ndani yake.
Samia kwa sasa hivi ashukuru tu kama atamudu kufika hiyo 2025 na kuutua mzigomkubwa sana unaomuelemea mgongoni mwake.
 
Kama iliwezekana kwa mamvi basi hakuna kinachoshindikana
 
Endelea kuota siku ukishtuka utajikuta umeshachelewa miaka 100.

Nilitegemea utanipa ushahidi wa kile Lisu alikifanya jimboni kwake kama mbunge kwa miaka 15.

Au alichofanya Slaa ili tuone uwezekano wa wao kumtoa Samia kupitia yale waliyofanya kwa wananchi. Kumbe wewe ubora wao unaupima kupitia kubwabwaja kwao.

Kama kubwabwaja kwa mwanasiasa ndio kigezo cha kupewa uraisi basi watanzania bado tuna safari ndefu kupitia wajinga kama nyie nchini.
 
Kwanza Lissu hanaga moto wa urais au uongozi sawa unavyotaka kutuamisha.

Lissu anapenda sana ubunge na aliwahi kukiri kwa kinywa chake.

Pili Lissu na Slaa ni marafiki wakubwa sana.

Slaa alipoondoka chamani na Lowassa kupewa nafasi Lissu aliingiwa na ukimya mkubwa sana.
 
Sina muda wa kupoteza hapa.

sijaona mfano wowote wa alichofanya Samia kabla, na hata sasa akiwa rais. Labda hilo lingekuongezea sifa kidogo za kuonyesha unao uwezo wa kufikiri na siyo kupayuka tu.

Hakuna lolote jipya ninaloweza kulipata toka kwenye akili kama yako.
 
Wewe umefika bandarin Mimi nafanya biashara ya inahusisha bandari Zaid ya miaka 25 sasa. Nimesafir nchi nyingi kwenye bandar nyingi coz of My business. Ila nachotaka kusema ni kuwa kuitoa bandari kwa mkataba ule ni big no ni punguani tu anaweza kufanya hayo madudu. Hakuna mtu anakataa wawekezaji shida ni mkataba Mzee. Bro nchi haiwez kugawa hela mpaka useme wewe unanufaika na nini. Ni jukum lako kuziona fursa na kupambana mtoto wa kiume acha kulegea. Eti bandari inanufaishaje nchi so hao wanaopaswa kuisimamia ili tuone manufaa yake kama wameshindwa si waachie ngaz waje wanaoweza? Yaan tumekupa mamlaka yote unashindwa kuyatumia unaenda kumpa mtu mgen simpo coz umeshindwa bure kabisa. Hawa watu bora wazee wao wangevaa condom tu wangetusaidia sana. Hiv unajua Singapore imeendelea kwasababu ya bandari tu.
 
Kama ulijua fika kuwa usiku utalala kwa kula ugali na mboga za maboga, hivi ni kwa nini sasa umejilipuwa kwa mataputapu na gongo!? Ona sasa madhara yake!
 
Kwahiyo 2020 aligombea ubunge au uraisi?
Wakati Lisu na Slaa wanatupiana maneno ya kashfa na kuchafuana wewe ulikuwa bado haujafika mjini?

Fungua picha hizo uone madongo
 

Attachments

  • Screenshot_20230704-092837.jpg
    87.5 KB · Views: 3
  • Screenshot_20230704-093429.jpg
    55.9 KB · Views: 3
Maneno mengi lkn hayana uwezo wa kumfanya mtu mwenye akili timamu kama mimi ayaamini. Kwa aina hii ya uandishi ni wazi kabisa kwamba hata bandari yenyewe haujui iko wapi achilia mbali porojo za kujifanya msafiri.

Mtu aliesafiri nchi mbali mbali hawezi kuambiwa kwamba mkataba au kitu fulan hakifai bila kuoneshwa kwa macho kile kisichofaa ili ajiridhishe kuwa kile alichoambiwa ni kweli.

Anyway mimi sio mtu wa kushikiwa akili au kufanywa spika la propaganda za wakwepa kodi wa bandarini. Maana mwisho wa siku utajikuta unatumiwa afu wanufaika na watoto wao wanakuona wewe poyoyo lao.

Ili nikubaliane na kile ulichoandika hapa naomba uniwekee mkataba hapa ili nione ubaya na kasoro zake. Ila kama ni bla bla za kuandika maneno mengi utafikiri gazeti. Ndugu yangu utakuwa unapoteza muda wako bure maana mimi sio type ya watu wanaoambiwa na wakwepa kodi, wachumia tumbo au wanasiasa fulani, afu eti na mimi nianze kukurupuka bila kuwa na uhakika kupitia macho yangu mwenyewe.

Never.
 
Unasema gazeti halafu umelirudia kuandika. Umesema huwez kutumiwa lakin ushatumika tayar. Naona ushachagua upande tusipoteze muda hatuwez kutumia muda mwingi kumuelewesha mjinga mmoja aliyegoma kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…