UCHAGUZI BAVICHA: John Pambalu aibuka kidedea Uenyekiti. Nusrat Shaaban Hanje ateuliwa kuwa Katibu Mkuu

UCHAGUZI BAVICHA: John Pambalu aibuka kidedea Uenyekiti. Nusrat Shaaban Hanje ateuliwa kuwa Katibu Mkuu

Wanawake mabinti wanaweza Sina shaka.Wana sababu kubwa ya mafanikio ya kisiasa ukizingatia Tanzania si kisiwa kilicho mbali na maendeleo ya dunia .Wanawake wengi wanafahamu changamoto Za kijamii na ni rahisi kuzitatua
 
Chadema bhana ni ya wachaga na wakurya,wasukuma wanachukuliwa kama bosheni kutafuta popularity,kulijua hili inahitaji uwaze nje ya box
Baraza la vijana (Bavicha) la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) linaendelea na uchaguzi wake leo kwa ngazi ya kitaifa.

Muda mfupi uliopita katika ukumbi wa Mlimani City limewapata viongozi wake wakuu ambapo Diwani wa Butimba jijini Mwanza, Bwana John Pambalu ameshinda Uenyekiti kwa kupata kura 150.

Pambalu amefuatiwa na Diwani mwenzake wa kata ya Ari wilayani Babati mkoani Manyara, Bwana Mathayo Gekul aliyepata kura 74.

Katibu wa Chadema jimbo la Kawe jijini DSM, Bi Dorcas Francis amemaliza wa tatu kwa kupata kura 58.

Kwa Makamu Mwenyekiti Tanganyika, Mwanaharakati Bi Moza Ally kashinda kwa kura 136 dhidi ya 72 za Diwani wa Nyansurura huko Serengeti Mkoani Mara, Bwana Francis Garatwa.

Kwa upande wa Zanzibar, Makamu Mwenyekiti ni Bwana Omary Nassor aliyepata kura 110 na kumzidi mpinzani wake, Bi Rukia Mohammed aliyepata kura 94.

Mwanadada Nusrat Shaaban Hanje kutoka Kigamboni DSM amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza hilo.

Bi Nusrat Hanje atasaidiwa na Kaunya Yohana kutoka Bunda Mkoani Mara kama Naibu wake, upande wa Tanganyika.

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ni Haji Abeid Haji.

Katibu Mwenezi amechaguliwa Kamanda Twaha Salim Mwaipaya.

Nafasi ya Mhasibu ni hapo baadae.

Hongereni sana Bavicha.

#IamTheFutureIwant#.NoHateNoFear.UchaguziChadema2019.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana Bavicha mko.vizuri kuliko.li chadema lenyewe.Bavicha mna sura ya kitaifa.Mwenyekiti katoka Tanzania Bara na makamu katoka Zanzibar.

Lichama lenyewe linazidwa akili na vitoto vya Bavicha sababu chadema wagombea uenyekiti wanatoka Tanzania Bara na Makamu mwenyekiti Ni Tundu Lisu toka Tanzania Bara hopeless kabisa.

Lichama pumbafu linazidwa akili na vitoto vya Bavicha

Hongereni na pongezi kwenu viongozi wote wa Bavicha mlioshinda
Hahaaa! Nilizani makamu katokea somalia kumbe singida? Wonders shall never end

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera zake!! Sio musukuma ila amekaa na kukulia mwanza( mkuyuni). Kabila lake ni MUFIPA TOKA SUMBAWANGA
 
Back
Top Bottom