Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi


========
Habari nilizo nazo ni kuwa CCM wanawalaumu akina Rostam kwa kukwamisha kampeni zao huko Busanda. Magazeti yao (Mtanzania na Rai) yamekaririwa wiki hii yakichambua udhaifu wa CCM badala ya kuwatia moyo. Rai limeenda mbali na kusema timu ya CCM huko Busanda haina mbinu za kisasa.

Ukweli huu unadhihirishwa na kuondoka kwa Makamba huko ambaye akina Rostam wanamtetea kuwa anaonewa na kuchongewa kwa Mwenyekiti. Kitendo cha Kampeni za Busanda kuongozwa na Mkuchika (Hasimu namba moja wa Lowassa) hakiwezi kuruhusu Rostam aende Busanda. Kimsingi, akina Rostam wanasubiri jimbo liende ili wapate cha kusema ndani ya KAMATI KUU. Mzee Malecela anapigana kufa na kupona, si kuwashinda Chadema, bali kuwaonyesha akina Rostam kuwa bila anaowaita "mafisadi", ushindi unawezekana. Nao wanaoitwa "Mafisadi" wanataka kusema, bila wao, CCM inayumba.

Muungwana kaenda USA na kuwaacha wamalizane wenyewe.
 
.............halisikii dawa!
CCM has never before stooped so low!

Nakumbuka lile sakata la ufisadi wa jengo la UVCCM ambapo Kikwete aliamua kuunda tume ya watu watatu kuchunguza tuhuma za ufisadi ule na kumpa wenyekiti wa tume ile fisadi Chenge na hadi hii leo hatujasikia chochote kuhusu ripoti ya tume iliyoundwa. Hivyo CCM wanavyotapatapa sasa hivi wanaweza kabisa kuwapeleka hao mapapa mafisadi ili wakamwage vijisenti maana fulana zao na matandiko waliyowahonga wapiga kura inaelekea hayajakonga nyoyo za wapiga kura wa Busanda.
 

Kwa msimamo wa CCM sasa hivi, wengi tunajiuliza kuwa hivi kinasimamia nini kiitikadi.Lazima wanachama waelewe wanachagua nini hasa.
 
Kwa msimamo wa CCM sasa hivi, wengi tunajiuliza kuwa hivi kinasimamia nini kiitikadi.Lazima wanachama waelewe wanachagua nini hasa.

Itikadi ziko mbili tu:
1. Tetea ufisadi na mafisadi kwa manufaa ya chama hata kama ikibidi kufa au kuua au kusababisha hali ngumu ya maisha.
2. Kumbuka namba 1 hapo juu
 
Zikiwa zimebaki siku sita tu wananchi wa jimbo la Busanda kupiga kura kumchagua mbunge wao, huku CCM ikiwa imekabwa kisawasawa na upinzani kutokana na tuhuma za ufisadi. Zipo tetesi kuwa CCM inapanga kuwatuma makda wake mahiri Mhe Rosatam Aziz na Mhe Andrew Chenge kwenda kufanya ka,peni kuokoa jahazi la chama hicho.

Kwa mujibu wa watu walio karibu na viongozi waandamizi wa CCM, baada ya mafanikio makubwa aliypoyapata Mhe Anne Kilango katika kampeni hizo kwa wananchi kumheshimu kwa kutomzomea hata kidogo. Viongozi mbali mbali wanataka makada hao ambao kwa kiwango kikubwa ndio wanaongozaakuipaka matope CCM wajitolee kwenda Busanda ili kukutana na joto la wananchi na sio kujificha kwenye luninga na redio.

Sababu ingine inayofanya viongozi wa CCM kutaka RA na AC wapelekwe Busanda ni kutokana na wao kuwa vinara wakusambaza siasa za chuki kikanda kuwa sasa hivi ni zamu ya kanda ya ziwa. Ikiwa Mama Kilango kutoka kanda ya kaskazini kulimudu joto la Busanda iweje makada mahiri kama RA na Ac wapige chenga kwenda kufanya kampeni kwenye kanda yao.

Wana JF mnasemaje? Je tunawaunga mkono wanaotaka RA na AC waende Busanda? au hatuungi mkono
 
Hii habari imekaa kama ijuma ijumaa vile?!!!!
Hivi sisiemu makini inaweza kweli kupeleka hawa jamaa kule kweli??? naona unatania mkuu

na kama ni kweli basi ujue mtu mzima uzeee unamtatiza
 
haiwezekani watu hao kupelekwa huko kwani ni kwenda kujiangamiza kwa ccm, so wapo clever pia si kuwa wanafanyaga everything kinyume.
 
Hapendwi mtu huko ni pochi tuu. Nafikiri watapeleka vijisent na mapesa
 
mjomba zile nyimbo za papa na nyangumi ziliimbwa vizuri sana, nasikia watu wako walizifurahia sana hasa kile kiitikio cha joel bendera,lakini kutishia kujamba wakati unaharisha ni ujinga. Siku hizi wamepata mbinu mpya mjomba, tena ilikujipatia umaarufu wanalazimisha kuweka jina la rostam kwenye kila tundiko, nadhani wanajua wanachokifanya tena wameadhimia kutupoteza na vita vya mafisadi vishindwe, lakini unajua dalili zao mjomba?nikipata vocha nitakupigia mjomba...
 
Itikadi ziko mbili tu:
1. Tetea ufisadi na mafisadi kwa manufaa ya chama hata kama ikibidi kufa au kuua au kusababisha hali ngumu ya maisha.
2. Kumbuka namba 1 hapo juu

Tehetehetehetehetehetehe, nimecheka kweli. Lakini kiukweli ndo hivyo wanavyofanya hawa jamaa. Nakumbuka Kingunge alivyowakemea wabunge wa CCM wanaokemea ufisadi kwa maslahi ya taifa. Yeye anasema maslahi ya chama kwanza. Na tumeona series ya uuaji wao e.g kwa akina Kolimba, Dk Ali Juma, Balali n.k na Maregesi kanusurika sijui ana hali gani sasa.
 
Unaweza kuwa beberu la kutupwa lakini katika hatari, lazima ufikirie. Japo Mafisadi ccm, wanatembea kifua mbele, lakini wanaelewa hasira za wananchi. Lakini kifo kiko palepale, hawatoki Busanda. Wana Busanda tupeni raha kwa kuonyesha People's power! Japo kuna kibaraka wa ccm (lipumba) anajaribu kuvuruga kwa kuwaambia wananchi wasiichague chadema (kwa mujibu wa magazeti), msitoe kura kwa ccm. Mwenye ccm yake alishakufa, waliobakia wamebadilika na kuwa chui katika ngozi ya chui!!!
 
hahahahaha
kibwagizo swaaafi sana hiki.
ukitoa albam nitakuwa wa kwanza kuipaireti.
hahaha
 
Jamani ikibidi tuwatie moyo kwa jinsi yoyote wawapeleke RA na mzee wa VIJISENTI ili idadi ya wabunge wa upinzani iongezeke bungeni.
 
RA aliingia kimya kimya Busanda na kumwanga fedha kufanikisha ushindi wa Bibie ambaye wengi wanasema ilipata ushindi wa kura za maoni kwa kupitia mngongo wa Katibu mkuu na kuwashinda Bwana Donald Max na yule kibaraka wa Dialo huku wengi wakitegemea Max ashinde akambulia nafasi ya pili.
RA ikabidi atumwe kwenda kumkatia Max ambaye tayari alishaweka makundi hivyo kuhatarisha ushindi wa CCM kama kipande hiki kinavyothibitisha

"Kutokana na makubaliano hayo CCM kiliagizwa kusaka fedha za kumrudishia Max ambazo zililetwa na mbunge mmoja wa Kanda ya Magharibi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ambaye imeelezwa aliingia Geita kimya kimya na kufanya mazungumzo naye."

Hata hivyo RA alikuwa analalamika kuwa kuna baadhi ya viongozi wamemtenga sijajua kwanini (papa)?

news baadhi ndio hizo
 
He kumbe haikuwa porojo.
Haya tuone kama atagawana umaskini na wanachi wa busanda kwa kuwahonga viongozi wao.....
 

Mh.... Mkuu utanisamehe, nimeshindwa kukuelewa sijui ni kwamba dots zako sizioni au vipi
 
Busanda ni CCM hata bila ya RA. Hii ni kutokana na kugawana kura kati ya Chadema na CUF. Kwa wapenda demokrasia ya kweli, watapenda kuona Busanda inatwaliwa na upinzani ili kupanua wigo wa demokrasia ndani ya Bunge kwa kuongeza uwiano wa upinzani Bungeni haswa ukizingatia wingi wa CCM Bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…