Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

hivi karibuni nilisoma makala ya adam lusekelo, kuhusu ccm kuisaidia cuf ili wapinzani wagawane kura wao wapete, na humu jamvini nimeona hizo juhudi.
 
Hivi sasa niko mkutano wa mwisho wa kampeni wa Chadema, watu ni wengi, wengi, wengi. Helcopta imeshatua na watu nji mzima wanakimbilia ilipotua.
Wengi wa wahudhuriaji ni watoto wadogo ambao sio wapiga kura. Huku mkutano ukiendelea, wao macho yao ni kwenye helicopter mahali ilipopaki kana kwamba ni helcopter ndiyo inayoongea.

Cha ajabu, huku mkutano wa kampeni unaendelea, helcopta imewashwa inaunguruma kwa muda, ... Hiyo inapaa juu...
Inafika angani, inegeuza njia, inaruka chini chini na inapita usawa wa mkutano huu wa Chadema, watu wanashangilia...
Helicopter hiyoo inapaa juu zaidi... Hiyoo.. inaendazake...
Haa...!. Baadhi ya watu nao hao wanaanza kujiondokea zao, huku wengine wakizidi kuingia hata kama hakuna helicopter.

Nimemsikia kwa makini mgombea wa Chadema, anamwaga sera za ukombozi wa wanabusanda huku akiwakumbusha umasikini ulioletwa na CCM, miaka nenda, miaka rudi.

Safu nzima ya uongozi wa juu wa Chadema iko mbele kuanzia Mbowe, Dr. Slaa, Zitto, wabunge wao na mwanasheria wao machachari Tundu Lissu.

Kijua ni kikali ila kuna upepo unaoopooza makali ya jua, huku wengi wa wahudhuriaji, wamebeba miamvuli inayomeremeta na
inayofanana utafikiri ni sehemu ya takrima ya Chadema kwa wana Busanda kama CCM ilivyofanya kumwaga takrima ya fulana na kofia karibu kila baa, gest na masokoni.

Najipanga kuelekea mkutano wa CCM unaoendelea mahali mbali na hapa, ila ni hapa hapa Katoro.
 
Jukwaani amepanda meneja kampeni wa Chadema, anaitwa Shelembi, jamaa ni noma!. Anapiga kampeni kwa Lugha ya Kisukuma, uwanja mzima unashangilia.
Miongoni mwa anayoyazungumza ni kuwaconvince wanaBusanda
Kutofanya makosa tena kwa kuichagua CCM baada ya miaka 48 ya utumwa wa CCM, Busanda..

Kusema ukweli, matamshi ya huyu jamaa na Kisukuma cha ndani haswa kile cha Chapa Ng'ombe, inaleta burudani fulani kusikia
Yaani hata jamaa angetoa single, ingehit hata kwa wasiojua Kisukuma.
 
Niko mkutano wa CCM, nikianzia umati wa watu, ukilinganisha na Chadema, sio siri CCM cha Mtoto!.
Kama watu niliowana mkutano wa Chadema ni wapiga kura kweli, basi kwa mara ya kwanza nakiri kuwa CCM itapigwa chini mjini Busanda. Vijijini, sijajua.

Hakuna Ob yoyote ya TBC, hivyo hakuna live TBC-1 labda TBC-Taifa mlioko huko sikilizeni.

Kampeni za Mwisho za CCM mdororo!.
Tambwe Hiza kachemsha eti Rais Bush kamwalika Jk!.
Waziri Masha kagoma kupanda Jukwwaani.

Mgombea wa CCM Mama Bukwimba hana uwezo wa kujieleza.
Kama wanaBusanda wanachagua mtu na sio chama, basi Mbunge ni Magesa. Lakini kwa vile wanachagua vyama, hata mgombea wa chama awe bomu vipi, chama kitambeba.

Mhe. Magufuli amepanda jukwaani anamwaga kikabila Kisukuma mwanzo mwisho kujibu mapigo ya Shelembi. Magufuli anashangiliwa sana, sasa anamwaga sumu kali dhidi ya Chadema kwa lugha ya Kisukuma.
Anamnadi vizuri mkombea wa CCM.

Leo sijaona wazomeaji.

Kwa vile campain hizi za CCM zinaboa, sitadumu hapa kwa muda mrefu, nitaelekea kampeni za CUF na kumalizia na kampeni za UDP.
 
Pasco you are doing great job, thanks dude kwa habari kutoka mahali pa tukio.
 
kwikwi Raisi bushi kweli hiza kichwa maji,mhuu CCM oyeeee!
 
Nilipost kuhusu mkutano wa CCM, post ilienda ila hapa sijaiona
Kwa kifupi ni kweli CCM hoi bin taaban Busanda mjini. Vijijini sijui.
Polisi na FFU wenye mabomu ya machozi ni wengi. Walianticipate vurugu ila mpaka sasa hali ni shwari.

UDP mkutano hajaanza mpaka sasa na CUF wako Nyarugusu.
Kwa sasa naishia hapa, Busanda haina umeme, E90 betri imechemsha!.
 
duh! wakati wa kwenda kwenye mkutano wa cuf,betri ndo imechemsha... Haya tutayaona! ukweli haufichiki...
 
duh! wakati wa kwenda kwenye mkutano wa cuf,betri ndo imechemsha... Haya tutayaona! ukweli haufichiki...
Sorry Calipso, ni kweli betri ilichemsha, CUF wako Nyarugusu watu ambao sikuwatendea haki ni UDP maana baada kupita na kukuta mkutano bado, nilitakiwa nipite tena, kutokana kuchemsha kwa UDP, sijaweza kupita tena.
Kampeni zimeisha Mbowe anahamasisha maandamano yasiyo rasmi, watu wanatawanyika FFU wamesogeza gari lao mkao wa kula. Mwenyeji wangu kanishauri tuondoke mahali hapo kabla wakina Mbowe hawajalianzisha....maana yake FFU wenye mabomu ya machozi wanaonekana wana hamu sana kuyafyatua!.

Hatukuondoka bali tulisogea mbali ili tushuhudie timbwili la kusambaratishwa maandamano yasiyo na kibali.

Kitu cha ajabu kabisa, polisi wale badala ya kuyatawanya waliyasindikiza hadi hoteli ya command post ya Chadema!.

Kumbe kuna baadhi ya makamanda polisi wana akili!. Maandamano yale yangesambaratishwa ndio ingekuwa chanzo cha vurugu!.

Kumbe sometimes polisi wetu wanahitaji kutumia busara kidogo tuu za common sense kuepusha shari!.
 
Yoyote unayesoma na kama unaamini sema

amen n amen in jesus name

subiri miujiza ya bwana

mungu awabariki watu wa busanda awachagulie chaguo kutoka kwa mungu;kila la kheri wana busanda...huku tukilalamika wizi wa kura za ccm tujitahidi kuomba mungu awafungue watu wa busanda wenyewe kwanza waweze kujilinda na wizi huo...nje ya hapo watiba kila sehemu kasoro tarime..ila uwezekano wa kuwabana wasiibe kura na michezo yao michafu ya kuhamisha masanduku ya kura
 


Chukua tano kwa sababu ukifikiria sana hawa jamaa sio tu wanatumia nguvu za kawaida bali pia wanatumia nguvu za giza si unajua tena mambo ya albino siyo bahati mbaya ni mpango maalumu. Ghafla wameacha nani aliyewapa order ya kuacha kwa pamoja.

Hivyo kwa kuwa jamaa wanatumia mpaka nguvu za giza dawa ni kuwalipua tu
 
Amina mtumishi

labda tuwakumbushe biblia takatifu kitabu cha
isaya 59:19
kinasema
basi wataliogopa jina ka bwana toka maghariib na utukufu wake toka mawiio ya jua maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao

kwa mamlaka tuliopewa na yesu tunakwenda kuamuru nguzu zote za giza zitakazotumika zisifanikiwe na si hilo tu mungu awambue hadharani.....

Lazima tumwombe mungu awatiishe awape ufahamu ccm kwamba mungu yupo ...isaya 62:6 inasema nimeweka walinzi juu ya yerusalemu hawatnyamaza mchana wala usiku ninyi wenye kumkumbusha bwana msiwe kimya....hivyo mimi na wewe na wote tunaoitkia tanzania mapenzi mema hatuna budi kumkumbusha mungu ashushe nguvu zake kesho...na watu wasinunulike kama wanavyofanya katika chaguzi za nyuma
 
Amina mtumishi
 
Saa hizi hapa kumetulia, imebaki kutafakari yaliyojiri mchana wa leo na kusalimia watu wanaoweza kusalimilika.
Nimepitia meza aliyokaa Mzee Malecela, Mama Anne Kilango na Dr. Antony Dialo.
Kutokana na heshima ya Mzee wetu huyu na kukubalika kwa Mama Kilango, sikuthubutu kuzungumzia lolote kuhusu uchaguzi wa kesho haswa kwa kuzingatia nimeshuhudia mwenyewe jinsi CCM ilivyojeruhiwa Katoro nisije kuharibu mood ya jioni hii.

Niliwasalimia kama mtoto anavyomwamkia baba na kuwa pole za hectic za kampeni na ofcourse nikamsifia Mama anavyomwaga sera.

Kwa upande wa Dialo, nilimpongeza kwa kazi nzuri inayofanywa na TV yake ya Star TV na redio yake ya RFA katika kampeni za Busanda na kutilia msisitizo kipindi maalum cha 30 min kilichorushwa leo saa 1:00-1:30 kuibeba CCM katika muda ambao kampeni zilishamaliika rasmi tangu saa 12:00 jioni, hivyo ni kinyume cha sheria. Kama sikosei, kipindi hiki, kitarudiwa kesho asubuhi saa 1:00-1:30.

Nimepita Dr. Slaa alipokaa na kumpongeza kwa kampeni kamambe. Nikamthibitishia Chadema imekubalika na kama ni kweli na vijijini mambo ni kama nilivyoshuhudia, sio tuu CCM itapata kipigo kitakatifu, bali pia itaangukia pua na kuiweka kwenye hali ngumu zaidi Biharamulo.

Kuna habari ambazo hazijathibitishwa eti CCM wamehakikishiwa ushindi na watu wa UWT. Pia kuna taarifa isiyo rasmi ikidai kuna mamia ya wapiga kura mamluki wa CCM wanaingia usiku huu mjini Busada tayari kupiga kura za CCM hiyo kesho.

Chadema kwa kulijua hilo, imetuma timu kukesha kivukoni Busisi kuhakikisha Busanda hakufikiki.

Nadhani leo niishie hapa nitaendeleza asubuhi kuwaleteeni zoezi la upigaji kura.
 


Mkuu kama hutojali, tumwagie kidogo wamejeruhiwaje mkuu? make jana ulitwmabia TBC itakuwa live sasa majeruhi tena?

Halafu hiyo UWT kuhakikishia ushindi chama fulani badala ya kura za kwenye sanduku kuamua imekaaje mkuu? hivi bado tupo katika enzi hizo? sasa kwanini tupoteze mapesa yote hayo na muda wa watu kufanya kampeini kama UWT wanapanga washindi na kuhakikisha wanakuwa? I dont get it mkuu!

All in all asante kwa taarifa.
 

This is what makes JF unique, volunteering for the masses ! Thank you so much, your concerted efforts to inform are highly regarded. Have a wonderful evening !
 
Pia kuna taarifa isiyo rasmi ikidai kuna mamia ya wapiga kura mamluki wa CCM wanaingia usiku huu mjini Busada tayari kupiga kura za CCM hiyo kesho.

Chadema kwa kulijua hilo, imetuma timu kukesha kivukoni Busisi kuhakikisha Busanda hakufikiki.
Hapo zitatumika mbinu za visiwani... na watapenya tu, maadam upigaji kura ni kuanzia 12.00 asubuhi hadi 12.00 hakuna shaka katika hilo.
 


Asante sana na zawadi yako ni ushindi kwa CHADEMA huko Busanda. Mungu yu pamoja nasim kwani tumejenga makanisa na tunayajaza everi sundei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…