Kwa bunge hili hata angekuwa nani mbele ya safari atalaumiwa sana" pengine hata mzee Sitta asipokuwa makini atakuja jiharibia sifa zake"
Kuna uzi humu ulikuwa nadhani unauliza KULIKONI SITA NA LOWASA kwenye Bunge la katiba?......... kwani walikuwa wanajadiliana jambo kila wanapokuwa pamoja.............Nchi hii MAMASTER MIND AND MAKER wapo wengi kila kitu munaloobu.........HATARI SANA...........naendelea kuangalia kwa karibu sana Trend and Track............
Leo saa 10,Bunge la katiba litamchagua mwenyekiti wa kudumu wa bunge la KATIBA,Wadau mnaombwa kuzingatia uzoefu,uadilifu,ujasiri na DIRA ya mgombea husika.
Wana JF, mimi kidogo dhamira yangu inanipa hofu saana juu ya huyu jamaa. Pongezi zangu naziweka hadi hapo nitakapoona katupatia Katiba mpyaa inayotokana na RASIMU YA PILI YA KATIBA na sio Katiba inayotokana na matakwa yao kama wajumbe wa bunge la katiba. Tusisahau Mzee Samweli Sita Hajaacha hata siku moja kuwa mwanachama mwaminifu kwa CCM, na mwana CCM. Hata siku moja usile naye yamini na Mwana CCM atakugeuka tu. Kumbukeni JK alivyowageuka vyama vya upinzani katika maamuzi yote aliyoyafanya toka atangaze kuanza kwa mchakato wa kupata katiba mpyaa hadi alipotangaza majina ya wajumbe wa baraza hili la katiba. Kifupi nasema TUSUBIRI MASIKIO YATASIKIA na MACHO YATAONA NINI KITATOKEA BAADA YA SIKU 70 au 90 za bunge hili.
Hii ndiyo risasi ya mwisho iliyobakia kwenye bunduki yako Mh.Sitta, ama itumie kumuua adui yako au jiue wewe mwenyewe ili usikamatwe mateka! Watanganyika wengi hatuna uanachama wa vyama vya siasa ila tu ni mashabiki hivyo ukifanya kosa ukaegemea upande wa chama chochote basi umaarufu wako wa SS ndio kwaheri!
Mimi Pia ninaimani nae sana wasiwasi wangu chama kubwa huwa hawanaga imani nae sana kwani chama ukiwa karibu na watu wewe ni adui yao wanataka uwe karibu na chama ilo ndilo linanitia wasi wasije wakamtosa nakumbuka kinyanganyiro cha uspika walivyomtendaga labda mzimu wa Richmond uwe umetoka bungeni.
Huyu bwana amungunyi maneno yeye ni muwazi na kdg mkweli tuombe mungu anaweza wakampa hyo mama kwa maslahi ya chama yote yawezekana maana pale kiti jina ila kuna mtu nje ndio anaendesha kile kiti kwa hiyo anatakiwa mtu laini kdg waweze kum drive.
kiukweli ni mtu ambaye anaweza akasimamia maslahi ya wananchi tukapata katiba inayotakiwa na wananchi,ila naomba kutoa angalizo,Nina mashaka na jinsi ccm walivyompitisha kiurahisi na wakati wanamjua kwamba huyu mtu uwa anasimamia ukweli,tukumbuke kwamba sita ni ccm na huenda ccm ilimpitisha kwakuwa walikubaliana kuwa atatetea maslahi ya chama chake,for me this may be a trap kwakuwa wanaona kwamba sita anakubalika sana ata na vyama pinzani.Haya ni mawazo yangu tu.