Uchaguzi: Hii ndio Dira ya Mh. Samuel J. Sitta Kama mwenyekiti Bunge la Katiba

Uchaguzi: Hii ndio Dira ya Mh. Samuel J. Sitta Kama mwenyekiti Bunge la Katiba

Unavyofikiri wewe samweli sita atafanikiwa kuletea katiba mpya kama atakuwa ndiyo amechaguliwa kuliongoza bunge la katiba? Maana wananchi wengi tunataka serikali tatu ila viongozi wa ccm wanataka mbili pia sita aliwahi sema serikali tatu ni ulafi. Tujadili bila chuki binafsi.
 
wanasema ya kaisali na apewe kaisali na ya mungu apewe mungu
1779356_692432247487427_1207154164_n.jpg

Mh Samuel J.Sitta a.k.a CHUMA CHA PUA,Yupo imala kabisa kama unavyomuona hapo ktk harakati za kurudisha fomu za kugombea uenyekiti wa KUDUMU bunge maalumu la KATIBA​

Mzee Samweli Sitta hakika anastahili kuongoza hili bunge kwani uwezo wa kushawishi na kusimamia haki anaweza kwa kiwango kikubwa. Hata wakati wake wa uspika Ufisadi mwingi uligundulika kwa kuruhusu mijadala ya wazi ambayo watu fulani fulani walionekana kumpinga na kumtisha kumnyang'a kadi ya chama. Na huo uzushi unaondelea mtaani Tuna uamuru kushindwa katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo. Mungu ampe afya njema na uzima wa kuitumiki nchi yake Ameni
 
Uamuzi sio wa Sitta au Bunge la Katiba. Wananchi ndio watakaoamua kwa kura, kuikubali au kuikataa hiyo Katiba!
 
Uamuzi sio wa Sitta au Bunge la Katiba. Wananchi ndio watakaoamua kwa kura, kuikubali au kuikataa hiyo Katiba!
Ni mwananchi yup kama tulio wachagua wamefika huko tuache walivyo zuzuka na posho na bahasha. Huja sikia kua wanasiasa na vyama vyao wanavyo pigania kataba ya watz igeuke kua ya vyama vyao mpk rasimu feki zimepenya. Na wajumbe ambao sio mlego wao wanabaniwa kusema. Huja msikia Mtikila na Mkosa mali?.
 
Mi namkubali si sana ila ninawasiwasi kama hatajenga ofisi nyingine Tabora!
 
Aminiki sana ila sasa kuliko chenge au likijani jengine yeye anakiunafuu
 
nadhani kitu cha kwanza ambacho hukijui ni kwamba KATIBA YA NCHI sio pekee muundo wa serikali iwe moja,mbili au tatu..na pia hoja yako imekaa "destructive" kwa kuwa unaonekana umeitoa kwa misingi ya chama chako...SITTA anafahamika kwa VIWANGO VYA UBORA WAKE KATIKA KUONGOZA SHUGHULI ZA BUNGE..na pia akiwa mwenyekiti sio yeye anayepitisha maoni yake na kuipitisha katiba..yeye kazi yake ni kuliongoza hilo bunge maalum tu na sio kuamua serikali mbili au tatu

pili..usiwasemee wananchi kuwa wengi wanataka serikali taut..hayo ni maoni yako binafsi tu kuwa wewe ndie unaetaka serikali tatu ivo usiwasingizie wananchi.

Unavyofikiri wewe samweli sita atafanikiwa kuletea katiba mpya kama atakuwa ndiyo amechaguliwa kuliongoza bunge la katiba? Maana wananchi wengi tunataka serikali tatu ila viongozi wa ccm wanataka mbili pia sita aliwahi sema serikali tatu ni ulafi. Tujadili bila chuki binafsi.
 
Ni mwananchi yup kama tulio wachagua wamefika huko tuache walivyo zuzuka na posho na bahasha. Huja sikia kua wanasiasa na vyama vyao wanavyo pigania kataba ya watz igeuke kua ya vyama vyao mpk rasimu feki zimepenya. Na wajumbe ambao sio mlego wao wanabaniwa kusema. Huja msikia Mtikila na Mkosa mali?.
Ndiyo maana nimesema wananchi ndiyo watakao chambua mchele na chunya kwa kura zetu! Kama ni Katiba Murua, tutapiga kuikubali na kama ni fake tutaikataa! Au unasemaje!
 
Unavyofikiri wewe samweli sita atafanikiwa kuletea katiba mpya kama atakuwa ndiyo amechaguliwa kuliongoza bunge la katiba? Maana wananchi wengi tunataka serikali tatu ila viongozi wa ccm wanataka mbili pia sita aliwahi sema serikali tatu ni ulafi. Tujadili bila chuki binafsi.

Kwanza nianze na hapo uliposema wananchi weng wanataka Serikali 3, ni ukweli ulio wazi kuwa wananchi wengi wanataka huduma bora za kijamii kama Afya, elimu na nyinginezo na ni wanasiasa ndio wanaopigana na ishu za muungano uwe wa namna gani Ukija kwenye issue ya Sitta kama anafaa au hafai siyo siri Sitta Tangu atoswe uspika wa Bunge la Jamhuri amekuwa ni mtu ambaye ni mnafiki na haeleweki.
 
Kama kuna mwanasiasa mwenye bahati kati ya wanaotajwa kuwania urais kupitia Ccm ni Sitta. Mpaka anapata nafasi ya kuongoza bunge la katiba, alikuwa ametimuliwa vumbi kwa mbali sana na wale wanaoutaka urais hasa Lowassa, Membe hata Makamba. Na naamini hata yeye mwenyewe alishaanza kukata tamaa na kuanza kupiga hatua za kurudi nyuma. Lakini baada ya kupata nafasi hii ni kama ametupiwa kamba ya kumtoa shimoni na ukweli nimjuavyo ataitumia inavyotakiwa ukizingatia rekodi yake katika bunge la tisa.

Hata hivyo kuna maswali mengi kuliko majibu ambayo tunaweza kujiuliza na kujadiliana:

  • Sitta atakuwa kama Warioba kukubali maoni ya watanzania yapite katika katiba inayopendekezwa?
  • Au atakisikiliza chama chake ambacho kwa maoni ya wengi kinakwenda kinyume na maoni ya watanzania?
  • Sitta ana ubavu kama aliyokuwa nao bunge la tisa mpaka akatishiwa kunyang'anywa kadi na chama chake?
  • Mpaka wanaelewana kumuachia nafasi ya mgombea pekee, hakuna mashariti aliyopewa yenye masrahi kwa chama chake?
  • Uswaiba wa ghafla na mafisadi mpaka wanakubaliana kuachiana nafasi hiyo umetoka wapi?
  • Upinzani haukuweka wagombea (hasa Chadema na CUF), je wanamwamini au yale makubaliano ya kabla ya 2010 yanaendelea?
Akiitumia nafasi hii ya miezi mitatu tu, anaweza kurudisha matumaini yake na hasa kama akiruhusu maoni ya watanzania yapite hatakuwa na wasi wasi maana hata chama chake kikimtupa anaweza kupitia upinzani na kupewa kura za shukrani na watanzania.
 
Kwanza nianze na hapo uliposema wananchi weng wanataka Serikali 3, ni ukweli ulio wazi kuwa wananchi wengi wanataka huduma bora za kijamii kama Afya, elimu na nyinginezo na ni wanasiasa ndio wanaopigana na ishu za muungano uwe wa namna gani Ukija kwenye issue ya Sitta kama anafaa au hafai siyo siri Sitta Tangu atoswe uspika wa Bunge la Jamhuri amekuwa ni mtu ambaye ni mnafiki na haeleweki.

Nani kakudanganya kuwa wananchi hawahitaji serikali3? Pamoja na kuhitaji huduma hizo za msingi ambazo umezitaja, lakini ukweli ni kuwa wananchi wanahitaji serikali3, siyo tume ya Warioba au Kisanga, maoni yamejirudia, sasa hiyo unayoisema wewe labda kama uko ulaya. Panda boti leo ukifika Zanzibar hata kwenye Grocery halafu sema hizo serikali 1 au 2 usikie moto wake?! 1 hawataki kwa kuwa watamezwa, mbili ndo kabisa wanaona ni ulaghai.
 
Kweli mkuu,anatakiwa awaoneshe watanzania kuwa anafaa.[/QUOTE

He will make it for sure, who else? He cannot afford to make mistakes and he knows that the people's support has an important meaning than that from his party!
 
kuna meseji kuwa ameanguka alipokuwa anakwenda kupeleka fomu je ni kweli?
 
Hakika huu ni wakati pekee kwa Sitta ama kujenga jina au kuliharibu. Akikumbuka suala la Njelu Kasaka na Mzee Aboud Jumbe hakika hatayumbishwa, ila akiamua kuambatana na mawazo ya kijambazi ya viongozi wa nchi hii na watoto wa wa kujitengenezea himaya ya utawala wa milele, hakika tutamsahau milele na kama tutamkumbuka basi itakuwa ni kwa mabaya u!
 
inaweza kuwa kweli mkuu kwani hawa jamaa kwa ndumba ni kiboko
 
Back
Top Bottom