Wakuu, nimekuwa na mjadala mkali na jamaa wawili, watatu na wengine wana 'ukigogo' kiasi fulani ndani ya CCM. Dondoo zilizozua mjadala huo naziweka hapa chini kama maswali.

Sote tunaelewa na kufahamu kuwa Katibu Mwenezi CCM - Nape Nnauye alikuwa Igunga kwa ajili ya kuhamasisha na kuandaa taratibu za ufunguzi wa kampeni, kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga. Haikuwa siri, kwani picha na taarifa zipo, na hata Nape mwenyewe binafsi amethibitisha hilo.

Pia tunakumbuka kuwa katika kikao cha Kamati Kuu kilichopita, mojawapo ya maazimio ya kikao hicho ni kutoa tamko rasmi lililowazuia Nape na Chiligati kwenda Igunga na/au kushiriki shughuli za uchaguzi Igunga.

Hakuna kikao kingine cha Kamati Kuu kilichokaa na kutengua uamuzi huo, au kutoa tamko linalotengua tamko hilo la awali.

Mjadala unakuja.

Je, Nape kwa kwenda Igunga, amekaidi na kupuuza maamuzi ya Kamati Kuu?

Na kama anafanya alivyoagizwa na makao makuu (kwani sidhani kama Nape anaweza kuondoka mwenyewe tu kwenda hadi Igunga kivyake-vyake), je, ni mtendaji gani aliyeamua/aliyekaidi hivyo nje ya vikao halali vya Kamati Kuu ambavyo vilitoa uamuzi wa kumzuia Nape na Chiligati kwenda Igunga, na haijakaa tena kubadili uamuzi huo?