From the best of my knowledge
Maaskofu wa katoliki wanateuliwa na papa baada ya mchakato mrefu.
Pia, hawana hicho cheo cha Askofu mkuu. Badala yake kila askofu ana mamlaka kamili kwenye jimbo lake. Anawaongoza maparoko, mapadri na watawa wengine ndani ya jimbo lake tu. Ni kama wabunge.
Kuhusu uchaguzi, upo wakati wa kuchagua viongozi wa Baraza lao la maaskofu (TEC). Lakini viongozi hao wa TEC hawana ukuu juu ya maaskofu wengine. Ni kama viongozi wa kamati za bunge.
Pia kuna baadhi ya maaskofu wana cheo cha ukadinali, mfano Pengo na Rugambwa. Hawa wanawajibika Vatican na sio viongozi wa maaskofu wengine. Ni kama mawaziri miongoni mwa wabunge.