Uchaguzi KKKT: Askofu Malasusa achaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa KKKT kuchukua nafasi ya Dkt. Fredrick Shoo

Uchaguzi KKKT: Askofu Malasusa achaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa KKKT kuchukua nafasi ya Dkt. Fredrick Shoo

Nawashangaa sana hawa maaskofu wa KKKT kumchagua huyu kipenyo,mwaka 2018 KKKT ilitoa waraka wa jinsi mambo ya awamu ya tano yalivyokuwa ndiyo siyo na ikaamriwa usomwe kwenye makanisa yote ya KKKT lakini huyu kipenyo akazuia usisomwe kwenye Dayosisi ya Mashariki na Pwani aliyokuwa anaiongoza. Mtu ambaye alikwenda kinyume na maaskofu wenzake inakuwaje leo wamwani kuwaongoza? Ataiheshimu kweli Katiba ya KKKT? Naliona Kanisa hili likienda kupasuka. Au Jecha alifufuka akasimamia huo uchaguzi wao?
 
From the best of my knowledge

Maaskofu wa katoliki wanateuliwa na papa baada ya mchakato mrefu.

Pia, hawana hicho cheo cha Askofu mkuu. Badala yake kila askofu ana mamlaka kamili kwenye jimbo lake. Anawaongoza maparoko, mapadri na watawa wengine ndani ya jimbo lake tu. Ni kama wabunge.

Kuhusu uchaguzi, upo wakati wa kuchagua viongozi wa Baraza lao la maaskofu (TEC). Lakini viongozi hao wa TEC hawana ukuu juu ya maaskofu wengine. Ni kama viongozi wa kamati za bunge.

Pia kuna baadhi ya maaskofu wana cheo cha ukadinali, mfano Pengo na Rugambwa. Hawa wanawajibika Vatican na sio viongozi wa maaskofu wengine. Ni kama mawaziri miongoni mwa wabunge.

Siyo kweli, cheo cha Askofu Mkuu kipo ila ni kwa jimbo kuu anbalo ndani yake yanakuwepo majimbo mengine yenye maaskofu. Kwa kufupi Askofu Mkuu wa Jimbo la Katoliki kunakuwa na maaskofu wa majimbo ndani ya jimbo kuu, yaani yeye anakuwa ni dingi sawa na kuongoza kanda!
 
Hiki ni kifo cha KKKT labda Mungu aingilie kulinusuru Kanisa hili. Shame upon us watu wa KKKT
 
Back
Top Bottom