Uchaguzi kwenye taasisi una kanuni na taratibu zake, Ni jambo nyeti. Huweza sambaratisha tasisi. Jee alichofanya Lissu ni sahihi?

Nani kakwambia chama ni mtu mmoja? Kwamba hamna kamati kuu? Hamna baraza kuu? Hakuna bodi ya wadhamini? Duh kwa mindset hii unadhani siku Mbowe akifariki ghafla huoni utatokea mtifuano mkubwa sana wa nani kumrithi? Ni bora tu amuachie mwenyekiti mwingine huku akifanya mentorship taratibu hadi awe level zake asisubiri chama kipasuke kama yaliyomkuta Lipumba na Mbatia
 
Ukipewa wewe unaweza kutekeleza,ulichoandika hapa?
Mimi si mwanasiasa na wala sijasema kwamba nina lengo hilo.

Ndiyo maana sijawahi kugombea hata ubalozi wa mtaa.

Umefanya logical fallacies za "logical non sequitur" na "whataboutism".

Tunamuongelea Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA na mapungufu yake.

Mimi hata kama nina mapungufu mengi, hilo halina tatizo, kwa sababu siongozi chama cha siasa cha kitaifa hivyo mapungufu yangu hayana impact katika uongozi wa chama cha siasa.

Huelewi wapi hapo?
 

Nimesoma sijaona vipengele ulivyoainisha
 
Katiba yao haina time limit wala mambo ya kung'atuka. Take from me atakayeng'atushwa ni Tundu Lissu mwanaharakati na kibaraka wa mabeberu
Ccm imejaa mapumbavu ndio maana haiwez kushinda bila polis.
 
Kama lengo kuu la chama cha siasa cha upinzani ni kuung'oa utawala madarakani kama unavyosema, Mbowe anatakiwa kujiuzulu uenyekiti kwa sababu ameshindwa kutimiza lengo hilo over and over again.
Unadhani kuung'oa utawala wa ccm ni jambo jepesi linaloweza kupatikana kwa muda huo mfupi wa miaka 20 ya Mbowe?

Kwa taarifa yako ni jambo ngumu sana kuliko lile la kuung'oa utawala wa Muingereza. CCM itakujaga kujing'oa yenyewe itakaposhindwa kutekeleza maendeleo ya watanzania au pale itakapojibomoa yenyewe kama ilivyotaka kutokea kwenye enzi ya Lowasa 2015. Walishajifunza.

Uzuri au ubaya wa vyama vya upinzani, wanaisaidia sana ccm iendelee kutawala vizuri. Kwani inapotokea ccm imekosea au imevurunda, mara moja vyama vya upinzani huipigia kelele, kuikosoa na kupendekeza kipi bora ifanye. Hivyo nayo hujirekebisha mara moja na kuendelea kupendwa na wapiga kura. Ningalikuwa mimi ni chama cha upinzani ningalikaa kimya ccm inapokosea na kuvurunda. Ningalifurahi kimoyo moyo na wakati mwingine kuipongeza na kuitaka iendelee na makosa inayofanya. Ningaliweka rekodi ya makosa yake ili wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu unaofuata nikawaoneshe wapiga kura na kuwashawishi wasiipigie kura ccm. Sasa wao wanaisahihisha mapema ccm na wakati wa kampeni ukifika wanakuwa hawana hoja ya kuingoa madarakani kwani inakuwa ilishajisahihisha na kuwa safi mbele ya wapiga kura. Hivyo ccm inawapenda sana vyama vya upinzani kwa michango yao ya kuisafisha ili iendelee kutawala.
 
Hoja imeenda shule, safi mkuu
 
Nani kasema Mbowe anangombea? Yeye hajatamka bado tungoje
 
Kama kuung'oa utawala wa CCM si jambo jepesi ni jambo gumu sana, that is even more reason mtu mmoja asing'ang'anie kuwa mwenyekiti kwa muda mrefu.

Kwa sababu hiyo ni kazi ngumu, kazi ya kupokezana si ya kuongozwa na mtu mmoja tu.
 
Kama kuung'oa utawala wa CCM si jambo jepesi ni jambo gumu sana, that is even more reason mtu mmoja asing'ang'anie kuwa mwenyekiti kwa muda mrefu.

Kwa sababu hiyo ni kazi ngumu, kazi ya kupokezana si ya kuongozwa na mtu mmoja tu.
Chadema haiongozwi na mtu mmoja. Kuna Kamati Kuu, Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na Baraza la Wadhamini. Mkutano Mkuu ndiyo huchagua Mwenyekiti wa Chama kwa kupiga kura za siri kila baada ya miaka 5. Haya yote ni kwa mjibu wa Katiba ya chama iliyopitiwa na kukubaliwa na Msajili wa vyama vya siasa kwa niaba ya serikali.

Utaratibu wa kubadilisha au kurekebisha katiba ili kuzuia mtu mmoja kukaa muda mrefu uko wazi. Tundu Lissu au mwanachama mwingine mwenye wazo kama hilo annapaswa kuwasilisha wazo hilo kwenye ngazi husika: kamati kuu, baraza kuu na hatimaye kwenye mkutano mkuu ambao ndiyo wenye maamuzi. Kama mchakato huo waliweza kwa wabunge waliowaita covid 19, kwa nini wazo hili zuri walishindwa kufanya hivyo badala yake wanakuja kupuyanga huku vichochoroni mbele ya waandishi wa habari? Nidhamu ya wapi hii kama siyo uhuni mtupu? Kutofuata utaratibu ni uhuni by definition.
 
CHADEMA haitakiwi kuongozwa na mtu mmoja ndiyo maana sasa ni wakati mwenyekiti ang'atuke.

Kuna mizozo kibao kuwa Mbowe ana scandals, mfano, anatumia akaunti binafsi kwa shughuli za chama.

Kiongozi mmoja akikaa muda mrefu kwenyw cheo anajijengea himaya ya kifalme, hiki si kitu kizuri.

Huelewi wapi?
 
Atang'atuliwa na mkutano mkuu wa chama unaowakilisha wanachama wote wa chadema nchini. Hawezi kung'atuliwa na vichochoroni na Tundu Lissu. Kwa taarifa tu ni kwamba ni kwamba ni jambo ngumu zaidi kumung'oa Mbowe kuliko kuing'oa ccm. Wasubiri tu hadi atakapoamua mwenyewe kwa hiari yake. Ni mtoto wa mjini, atawaangamiza wahuni wote wanaotaka kumchezea.
 
Huwezi tu mtu ukakurupuka kutoka huko ulikotokea, tena wakati wo wote na kujitangaza mwenyewe kuwa wewe ni mtia nia au mgombea wa kiti fulani kwenye chama chako.
Upo sahihi sana mkuu ktk hili. Lkn kwani Lisu alojitangaza kuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti ama kasema ameondoa kusudio la kugombea umakamu mwenyekiti na sasa kapeleka kusudio la kugombea uenyekiti??

Vikao vya chama bado vinayo nafasi ya kukataa ama kukubali maombi ya Lisu, lkn waje na sababu kuntu.

Wasimuogope wala wasimuonee Lisu.
 
Wasubiri tu hadi atakapoamua mwenyewe kwa hiari yake.
Kwa mantiki hii chadema ni mali binafsi ya Mbowe na siyo chama cha demokrasia.

Demokrasia maana yake ni wote wanashiriki kuamua, maamuzi ya wengi ndiyo yanayopewa nafasi.

Sasa kwann Mbowe asiheshimu maoni ya wengi wanaomtaka kukaa pembeni? Kwa kuwa kukaa kwake muda mrefu kwenye nafasi ya uenyekiti kunakiletea doa chama. Anaonekana ni Nkurunzinza ndani ya chadema.
 
Basi isiwe nongwa kama kuna mwanachama mwingine (mfano Lisu) anapotangaza kugombea nafasi hiyo. Shida nn?
 
Hujaelewa naongea nini.

Mbowe alitakiwa kung'atuka mwenyewe kabla ya kung'atuliwa na mkutano wowote.

Nyerere hakung'atuliwa na mkutano wowote. Mikutano yote ilikuwa inamwambia "Mwalimu bado tunakuhitaji".

Akang'atuka mwenyewe.
 
Hahaha kwa nini AMUACHIE wakati Lisu kasema anatangaza nia KUGOMBEA? Na kama anagombea ,agombee na Mbowe au hiyo siyo Demokrasia pia? Naona mnataka apite bila kupingwa au awe mgombea pekee?
 
AMUACHIE wakati Lisu kasema anatangaza nia KUGOMBEA
Wapi nimesema Mbowe amuachie Lissu uenyekiti?
Na kama anagombea ,agombee na Mbowe au hiyo siyo Demokrasia pia?
Mbona hata kwenye Urais alichukua fomu ila baada ya kuona upepo wa Lissu akaghairi kurudisha fomu maana anajua asingepata hata kura 1. Kwahiyo Lissu hajawahi muogopa Mbowe in fact Mbowe anaogopa open election maana anaweza kushinda ila kwa kura chache possibly 52% sasa itampunguzia credibility na infallible status aliyokua amejiwekea na hawezi kubali hilo.
Naona mnataka apite bila kupingwa au awe mgombea pekee?
Hapana tunataka demokrasia agombee ila sasa asitumie incumbency kuharibu uchaguzi atavuruga chama. Akishindwa akubali matokeo na akishinda basi aweze kujenga umoja maana mpasuko utakua obvious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…