Kumchoka kunaoneshwa kwenye sanduku la kura. Ukikionesha kwa mtindo aliofanya Lissu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kwa chama na mwenyekiti wake. It is insubordination to Mr Freeman Mbowe. Hili halikubaliki, hatua kali za kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Tundu Lissu.
Bw. Kiranga, jaribu kutofautisha Nyerere wa kabla ya uhuru na yule Nyerere wa baada ya uhuru.
Nyerere wa kabla ya uhuru aliacha kazi yake ya umma kama mwalimu wa sekondari huko Pugu, na kwenda kujiunga na chama cha siasa cha TAA ambacho baadaye kiliitwa TANU na yeye akawa mwenyekiti wake. Lengo la TANU lilikuwa ni kuung'oa utawala wa Muingereza ili Tanganyika ipate uhuru. Aliacha mshahara wake mzuri wa ualimu. Kazi ya uenyekiti wa TANU haukuwa na mshahara wo wote. Ilikuwa ni kazi ya kujitolea. Kazi hiyo ilitegemea michango ya matajiri wa wakati huo hususani akina Sykes na baba yake na Freeman Aikel Mbowe ambao walikuwa wanaharakati wa mbio hizo za kuleta uhuru. Hivyo katika mbio hizo huwezi ukaweka muda wa ukomo wa uongozi wala mambo ya kung'atuka.
Nyerere wa baada ya uhuru alichaguliwa kwenye utumishi wa umma kwenye ngazi ya uraisi wa nchi na amiri jeshi mkuu. Pia aliendelea kuchaguliwa na chama chake cha TANU kilichoitwa baadaye CCM kama mwenyekiti wake. Katiba na sheria za nchi na zile za TANU hazikuwa na kipengele cha ukomo wa kugombea nafasi hizo. Baada ya kushika nafasi hizo kwa miaka takribani 25 mfululizo, busara yake ikamuongoza kung'atuka na kuweka utaratibu wa kikatiba wa ukomo wa miaka 10 kwenye vyeo hivyo serikalini na kwenye chama chake cha CCM.
Lengo kuu la vyama vya siasa vya upinzani kama CHADEMA ni kuung'oa madarakari utawala wa CCM, kama ilivyokuwa lengo kuu la TANU kabla ya uhuru ie kuung'oa utawala wa Muingereza. Mbio au harakati zote za vyama vya upinzani ni hilo. Uongozi wake ni wa kujitolea. Uendeshaji wake unategemea michango ya wanachama wake. Utumishi wao hauna mishahara, tofauti na wengi wanavyofikiria. Inashangaza hadi watu wanararuana na wakati mwingine kuuana kugombea vyeo kwenye vyama hivyo? Jee sababu ni kwenda kudokoa au kuiba hiyo michango ya wanachama ya kuendeshea chama chao? Freeman Aikel Mbowe alizaliwa siku ya uhuru wa Tanganyika. Baba yake alikuwa kati ya wanaharakati waliochangia kwa hali na mali kumng'oa Muingereza. Hivyo uanaharakati huo wa Mbowe ni wa kuzaliwa na kulelewa nao.
Kipindi cha kampeni ni kipindi hatari sana. Ni kipindi cha kubomoana. Busara na taratibu zinawatakq wagombea wabomoane kwa staha. Ndiyo maana kwa kuzingatia athari zake, kipindi hicho hupangiwa siku au wiki chache tu kabla ya uchaguzi wenyewe. Ratiba lazima izingatiwe. Huwezi ukaanza kufanya kampeni kabla ya filimbi ya kuanza kampeni aka kubomoana haijapulizwa. Tundu Lissu kaanza kabla ya filimbi haijapulizwa. Tarehe ya uchaguzi wala bado haijapangwa. Inawezekana ikawa hata mwezi wa nne mwakani. Sasa ataendelea kubomoa kwa miezi yote hiyo kabla ya uchaguzi? Hadi siku ya uchaguzi si atakuwa amebomoa kila kitu?
NEC hupokea majina kutoka kwa vyama vya siasa, jina moja kwa kila chama kilicho na usajili kamili. Tundu Lissu hakupeleka jina lake mwenyewe huko NEC. Angalifanya hivyo halingalipokelewa. NEC haina ya kukata majina yaliyowakilishwa na vyama hali vya siasa.
Kwa upande wa vyama vya siasa kasome katiba, kanuni na taratibu za kila chama ambazo huwa zimepitiwa na kukubaliwa na msajili wa vyama vya siasa kwa niaba ya serikali. Hizi zisipofuatwa msajili ana mamlaka ya kuwaadhibu wahusika.
Kwa upande wa uchanguzi wa serikali kasome katiba ya nchi, sheria na kanuni za uchaguzi
Sasa kwani kuna mtanzania ambaye halijui hilo? Chadema kwa upande wa Tanzania bara kwa sasa ndiyo chama cha upinzani chenye wanachama na washabiki wengi na kimeenea kote. Na aliyewezesha hili kutokea ni Freeman Mbowe kwa kuwapokea Edward Lowasa na Sumaye kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.
Hivyo mitifuano ye yote kwenye vyama hivi viwili (CCM na CHADEMA) vinaweza kuleta athari kwa mtanzania yeyote, mwanachama na asiye mwanachama hususani kutekana na kuuana kwa sababu za kisiasa. Na kwa kiasi kikubwa vyama hivi vinaendeshwakwa pesa ya kodi zetu kupitia ruzuku ya serikali.
Huko tunakoelekea Tundu Lissu anaweza kuiua CHADEMA na kuiacha Tanzania bara kuelea kwenye utawala wa chama kimoja, kitu ambacho hakipendezi.