Uchaguzi kwenye taasisi una kanuni na taratibu zake, Ni jambo nyeti. Huweza sambaratisha tasisi. Jee alichofanya Lissu ni sahihi?

Uchaguzi kwenye taasisi una kanuni na taratibu zake, Ni jambo nyeti. Huweza sambaratisha tasisi. Jee alichofanya Lissu ni sahihi?

Hahaha Lisu huyu hawezi kuivusha CHADEMA, analia lia sana.

Alipewa TLS ikamshinda, hakufanya chochote, leo anaitaka CHADEMA bila Mbowe mtaja kusema humu humu kwamba anahujumiwa na Mbowe, lakini ukweli ni kwamba CHADEMA Lisu anaweza kelele tu lakini hawezi na hana uwezo kuendesha chadema.

CHADEMA siyo shule kwamba yeyote anaweza kuwa mwalimu mkuu, CHADEMA ni Tanzania, huwezo huo LISU hana jamani.
Nani kakwambia chama ni mtu mmoja? Kwamba hamna kamati kuu? Hamna baraza kuu? Hakuna bodi ya wadhamini? Duh kwa mindset hii unadhani siku Mbowe akifariki ghafla huoni utatokea mtifuano mkubwa sana wa nani kumrithi? Ni bora tu amuachie mwenyekiti mwingine huku akifanya mentorship taratibu hadi awe level zake asisubiri chama kipasuke kama yaliyomkuta Lipumba na Mbatia
 
Ukipewa wewe unaweza kutekeleza,ulichoandika hapa?
Mimi si mwanasiasa na wala sijasema kwamba nina lengo hilo.

Ndiyo maana sijawahi kugombea hata ubalozi wa mtaa.

Umefanya logical fallacies za "logical non sequitur" na "whataboutism".

Tunamuongelea Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA na mapungufu yake.

Mimi hata kama nina mapungufu mengi, hilo halina tatizo, kwa sababu siongozi chama cha siasa cha kitaifa hivyo mapungufu yangu hayana impact katika uongozi wa chama cha siasa.

Huelewi wapi hapo?
 
Kumchoka kunaoneshwa kwenye sanduku la kura. Ukikionesha kwa mtindo aliofanya Lissu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kwa chama na mwenyekiti wake. It is insubordination to Mr Freeman Mbowe. Hili halikubaliki, hatua kali za kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Tundu Lissu.

Bw. Kiranga, jaribu kutofautisha Nyerere wa kabla ya uhuru na yule Nyerere wa baada ya uhuru.

Nyerere wa kabla ya uhuru aliacha kazi yake ya umma kama mwalimu wa sekondari huko Pugu, na kwenda kujiunga na chama cha siasa cha TAA ambacho baadaye kiliitwa TANU na yeye akawa mwenyekiti wake. Lengo la TANU lilikuwa ni kuung'oa utawala wa Muingereza ili Tanganyika ipate uhuru. Aliacha mshahara wake mzuri wa ualimu. Kazi ya uenyekiti wa TANU haukuwa na mshahara wo wote. Ilikuwa ni kazi ya kujitolea. Kazi hiyo ilitegemea michango ya matajiri wa wakati huo hususani akina Sykes na baba yake na Freeman Aikel Mbowe ambao walikuwa wanaharakati wa mbio hizo za kuleta uhuru. Hivyo katika mbio hizo huwezi ukaweka muda wa ukomo wa uongozi wala mambo ya kung'atuka.

Nyerere wa baada ya uhuru alichaguliwa kwenye utumishi wa umma kwenye ngazi ya uraisi wa nchi na amiri jeshi mkuu. Pia aliendelea kuchaguliwa na chama chake cha TANU kilichoitwa baadaye CCM kama mwenyekiti wake. Katiba na sheria za nchi na zile za TANU hazikuwa na kipengele cha ukomo wa kugombea nafasi hizo. Baada ya kushika nafasi hizo kwa miaka takribani 25 mfululizo, busara yake ikamuongoza kung'atuka na kuweka utaratibu wa kikatiba wa ukomo wa miaka 10 kwenye vyeo hivyo serikalini na kwenye chama chake cha CCM.

Lengo kuu la vyama vya siasa vya upinzani kama CHADEMA ni kuung'oa madarakari utawala wa CCM, kama ilivyokuwa lengo kuu la TANU kabla ya uhuru ie kuung'oa utawala wa Muingereza. Mbio au harakati zote za vyama vya upinzani ni hilo. Uongozi wake ni wa kujitolea. Uendeshaji wake unategemea michango ya wanachama wake. Utumishi wao hauna mishahara, tofauti na wengi wanavyofikiria. Inashangaza hadi watu wanararuana na wakati mwingine kuuana kugombea vyeo kwenye vyama hivyo? Jee sababu ni kwenda kudokoa au kuiba hiyo michango ya wanachama ya kuendeshea chama chao? Freeman Aikel Mbowe alizaliwa siku ya uhuru wa Tanganyika. Baba yake alikuwa kati ya wanaharakati waliochangia kwa hali na mali kumng'oa Muingereza. Hivyo uanaharakati huo wa Mbowe ni wa kuzaliwa na kulelewa nao.

Kipindi cha kampeni ni kipindi hatari sana. Ni kipindi cha kubomoana. Busara na taratibu zinawatakq wagombea wabomoane kwa staha. Ndiyo maana kwa kuzingatia athari zake, kipindi hicho hupangiwa siku au wiki chache tu kabla ya uchaguzi wenyewe. Ratiba lazima izingatiwe. Huwezi ukaanza kufanya kampeni kabla ya filimbi ya kuanza kampeni aka kubomoana haijapulizwa. Tundu Lissu kaanza kabla ya filimbi haijapulizwa. Tarehe ya uchaguzi wala bado haijapangwa. Inawezekana ikawa hata mwezi wa nne mwakani. Sasa ataendelea kubomoa kwa miezi yote hiyo kabla ya uchaguzi? Hadi siku ya uchaguzi si atakuwa amebomoa kila kitu?

NEC hupokea majina kutoka kwa vyama vya siasa, jina moja kwa kila chama kilicho na usajili kamili. Tundu Lissu hakupeleka jina lake mwenyewe huko NEC. Angalifanya hivyo halingalipokelewa. NEC haina ya kukata majina yaliyowakilishwa na vyama hali vya siasa.

Kwa upande wa vyama vya siasa kasome katiba, kanuni na taratibu za kila chama ambazo huwa zimepitiwa na kukubaliwa na msajili wa vyama vya siasa kwa niaba ya serikali. Hizi zisipofuatwa msajili ana mamlaka ya kuwaadhibu wahusika.

Kwa upande wa uchanguzi wa serikali kasome katiba ya nchi, sheria na kanuni za uchaguzi

Sasa kwani kuna mtanzania ambaye halijui hilo? Chadema kwa upande wa Tanzania bara kwa sasa ndiyo chama cha upinzani chenye wanachama na washabiki wengi na kimeenea kote. Na aliyewezesha hili kutokea ni Freeman Mbowe kwa kuwapokea Edward Lowasa na Sumaye kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.

Hivyo mitifuano ye yote kwenye vyama hivi viwili (CCM na CHADEMA) vinaweza kuleta athari kwa mtanzania yeyote, mwanachama na asiye mwanachama hususani kutekana na kuuana kwa sababu za kisiasa. Na kwa kiasi kikubwa vyama hivi vinaendeshwakwa pesa ya kodi zetu kupitia ruzuku ya serikali.

Huko tunakoelekea Tundu Lissu anaweza kuiua CHADEMA na kuiacha Tanzania bara kuelea kwenye utawala wa chama kimoja, kitu ambacho hakipendezi.

Nimesoma sijaona vipengele ulivyoainisha
 
Katiba yao haina time limit wala mambo ya kung'atuka. Take from me atakayeng'atushwa ni Tundu Lissu mwanaharakati na kibaraka wa mabeberu
Ccm imejaa mapumbavu ndio maana haiwez kushinda bila polis.
 
Kama lengo kuu la chama cha siasa cha upinzani ni kuung'oa utawala madarakani kama unavyosema, Mbowe anatakiwa kujiuzulu uenyekiti kwa sababu ameshindwa kutimiza lengo hilo over and over again.
Unadhani kuung'oa utawala wa ccm ni jambo jepesi linaloweza kupatikana kwa muda huo mfupi wa miaka 20 ya Mbowe?

Kwa taarifa yako ni jambo ngumu sana kuliko lile la kuung'oa utawala wa Muingereza. CCM itakujaga kujing'oa yenyewe itakaposhindwa kutekeleza maendeleo ya watanzania au pale itakapojibomoa yenyewe kama ilivyotaka kutokea kwenye enzi ya Lowasa 2015. Walishajifunza.

Uzuri au ubaya wa vyama vya upinzani, wanaisaidia sana ccm iendelee kutawala vizuri. Kwani inapotokea ccm imekosea au imevurunda, mara moja vyama vya upinzani huipigia kelele, kuikosoa na kupendekeza kipi bora ifanye. Hivyo nayo hujirekebisha mara moja na kuendelea kupendwa na wapiga kura. Ningalikuwa mimi ni chama cha upinzani ningalikaa kimya ccm inapokosea na kuvurunda. Ningalifurahi kimoyo moyo na wakati mwingine kuipongeza na kuitaka iendelee na makosa inayofanya. Ningaliweka rekodi ya makosa yake ili wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu unaofuata nikawaoneshe wapiga kura na kuwashawishi wasiipigie kura ccm. Sasa wao wanaisahihisha mapema ccm na wakati wa kampeni ukifika wanakuwa hawana hoja ya kuingoa madarakani kwani inakuwa ilishajisahihisha na kuwa safi mbele ya wapiga kura. Hivyo ccm inawapenda sana vyama vya upinzani kwa michango yao ya kuisafisha ili iendelee kutawala.
 
Kuna uwezekano Mbowe mwenyewe amempa baraka Lissu ya kutangaza nia.

Hilo la Lissu kuonekana kama anakosoa chama na uongozi wa sasa ni muhimu sana. Hata JPM na CCM kwa ujumla walifanya hivyo 2015.

Hapa majuzi tu Kamala Haris alifanya kosa kama hilo la kuogopa kumkosoa bosi wake kwenye uchaguzi wa Marekani, aliulizwa ni kitu gani atafanya cha tofauti na Joe Biden, akasema hakuna atakachofanya cha tofauti. Alisema hivyo kwa kutotaka kumkosoa bosi wake. Kosa kubwa.

Lazima uoneshe tofauti yako na waliopo sasa ili kuwapa sababu watu ya kukuchagua. Kama hauna cha tofauti utakachokifanya kwanini watu wakupigie kura? Si afadhali waendelee na huyohuyo aliyepo?
Hoja imeenda shule, safi mkuu
 
Mbowe anavyozidi kuongea ndiyo anavyozidi kudhihirisha kuwa ana elimu ndogo.

Ule.msemo wa "Kaa kimya ili watu wasijue ujinga wako" unamhusu sana Mbowe.

Hili jambo la ujinga wa Mbowe lilikuwa linafichika kirahisi wakati anaisema serikali na CCM, kwani hapo huhitaji elimu kubwa kuisema CCM. Huhitaji mambo mengi ya nuance. Hata mjinga anaweza kusema tu "Katiba mpyaa, tume huruu, peopleees, power" akaonekana ana akili.

Lakini, ukija kwenye issue kama kutetea kukaa kwenye uenyekiti muda mrefu kwenye nchi ambayo Nyerere kashaweka somo na standard, mpaka tumejifunza neno "kung'atuka", Mbowe ameshindwa kujenga hoja za kimantiki kwa nini yeye abaki. Kasema, kawafokea watu, halafu baada ya kusema kwa mihemuko kaja Lissu kapanga maneno vizuri, kwa hoja, kabla.Lissu hajatangaza kugombea uenyekiti mimi nikasema hapa mbona Mbowe kaongea pumba halafu Lissu ndiye kaongea vizuri?
Nani kasema Mbowe anangombea? Yeye hajatamka bado tungoje
 
Unadhani kuung'oa utawala wa ccm ni jambo jepesi linaloweza kupatikana kwa muda huo mfupi wa miaka 20 ya Mbowe?

Kwa taarifa yako ni jambo ngumu sana kuliko lile la kuung'oa utawala wa Muingereza. CCM itakujaga kujing'oa yenyewe itakaposhindwa kutekeleza maendeleo ya watanzania au pale itakapojibomoa yenyewe kama ilivyotaka kutokea kwenye enzi ya Lowasa 2015. Walishajifunza.

Uzuri au ubaya wa vyama vya upinzani, wanaisaidia sana ccm iendelee kutawala vizuri. Kwani inapotokea ccm imekosea au imevurunda, mara moja vyama vya upinzani huipigia kelele, kuikosoa na kupendekeza kipi bora ifanye. Hivyo nayo hujirekebisha mara moja na kuendelea kupendwa na wapiga kura. Ningalikuwa mimi ni chama cha upinzani ningalikaa kimya ccm inapokosea na kuvurunda. Ningalifurahi kimoyo moyo na wakati mwingine kuipongeza na kuitaka iendelee na makosa inayofanya. Ningaliweka rekodi ya makosa yake ili wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu unaofuata nikawaoneshe wapiga kura na kuwashawishi wasiipigie kura ccm. Sasa wao wanaisahihisha mapema ccm na wakati wa kampeni ukifika wanakuwa hawana hoja ya kuingoa madarakani kwani inakuwa ilishajisahihisha na kuwa safi mbele ya wapiga kura. Hivyo ccm inawapenda sana vyama vya upinzani kwa michango yao ya kuisafisha ili iendelee kutawala.
Kama kuung'oa utawala wa CCM si jambo jepesi ni jambo gumu sana, that is even more reason mtu mmoja asing'ang'anie kuwa mwenyekiti kwa muda mrefu.

Kwa sababu hiyo ni kazi ngumu, kazi ya kupokezana si ya kuongozwa na mtu mmoja tu.
 
Chadema haiongozwi na mtu mmoja. Kuna Kamati Kuu, Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na Baraza la Wadhamini. Mkutano Mkuu ndiyo huchagua Mwenyekiti wa Chama kwa kupiga kura za siri kila baada ya miaka 5. Haya yote ni kwa mjibu wa Katiba ya chama iliyopitiwa na kukubaliwa na Msajili wa vyama vya siasa kwa niaba ya serikali.

Utaratibu wa kubadilisha au kurekebisha katiba ili kuzuia mtu mmoja kukaa muda mrefu uko wazi. Tundu Lissu au mwanachama mwingine mwenye wazo kama hilo annapaswa kuwasilisha wazo hilo kwenye ngazi husika: kamati kuu, baraza kuu na hatimaye kwenye mkutano mkuu ambao ndiyo wenye maamuzi. Kama mchakato huo waliweza kwa wabunge waliowaita covid 19, kwa nini wazo hili zuri walishindwa kufanya hivyo badala yake wanakuja kupuyanga huku vichochoroni mbele ya waandishi wa habari? Nidhamu ya wapi hii kama siyo uhuni mtupu? Kutofuata utaratibu ni uhuni by definition.
 
CHADEMA haitakiwi kuongozwa na mtu mmoja ndiyo maana sasa ni wakati mwenyekiti ang'atuke.

Kuna mizozo kibao kuwa Mbowe ana scandals, mfano, anatumia akaunti binafsi kwa shughuli za chama.

Kiongozi mmoja akikaa muda mrefu kwenyw cheo anajijengea himaya ya kifalme, hiki si kitu kizuri.

Huelewi wapi?
 
Atang'atuliwa na mkutano mkuu wa chama unaowakilisha wanachama wote wa chadema nchini. Hawezi kung'atuliwa na vichochoroni na Tundu Lissu. Kwa taarifa tu ni kwamba ni kwamba ni jambo ngumu zaidi kumung'oa Mbowe kuliko kuing'oa ccm. Wasubiri tu hadi atakapoamua mwenyewe kwa hiari yake. Ni mtoto wa mjini, atawaangamiza wahuni wote wanaotaka kumchezea.
 
Huwezi tu mtu ukakurupuka kutoka huko ulikotokea, tena wakati wo wote na kujitangaza mwenyewe kuwa wewe ni mtia nia au mgombea wa kiti fulani kwenye chama chako.
Upo sahihi sana mkuu ktk hili. Lkn kwani Lisu alojitangaza kuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti ama kasema ameondoa kusudio la kugombea umakamu mwenyekiti na sasa kapeleka kusudio la kugombea uenyekiti??

Vikao vya chama bado vinayo nafasi ya kukataa ama kukubali maombi ya Lisu, lkn waje na sababu kuntu.

Wasimuogope wala wasimuonee Lisu.
 
Wasubiri tu hadi atakapoamua mwenyewe kwa hiari yake.
Kwa mantiki hii chadema ni mali binafsi ya Mbowe na siyo chama cha demokrasia.

Demokrasia maana yake ni wote wanashiriki kuamua, maamuzi ya wengi ndiyo yanayopewa nafasi.

Sasa kwann Mbowe asiheshimu maoni ya wengi wanaomtaka kukaa pembeni? Kwa kuwa kukaa kwake muda mrefu kwenye nafasi ya uenyekiti kunakiletea doa chama. Anaonekana ni Nkurunzinza ndani ya chadema.
 
Kahodhi madaraka kwa vipi wakati kila miaka mitano vikao halali vya chama vilikuwa vinamchagua kuwa mgombea wa kiti hicho na mkutano mkuu halali wa chama kupmpigia kura ya siri na kushinda. Tundu Lissu ni mmoja wa waliokuwa wanampigia kura hizo za ushindi. Hakuna aliyelalamika kuwa alikuwa anaiba kura wala kulikuwa na kura feki na kadhalika.
Basi isiwe nongwa kama kuna mwanachama mwingine (mfano Lisu) anapotangaza kugombea nafasi hiyo. Shida nn?
 
Atang'atuliwa na mkutano mkuu wa chama unaowakilisha wanachama wote wa chadema nchini. Hawezi kung'atuliwa na vichochoroni na Tundu Lissu. Kwa taarifa tu ni kwamba ni kwamba ni jambo ngumu zaidi kumung'oa Mbowe kuliko kuing'oa ccm. Wasubiri tu hadi atakapoamua mwenyewe kwa hiari yake. Ni mtoto wa mjini, atawaangamiza wahuni wote wanaotaka kumchezea.
Hujaelewa naongea nini.

Mbowe alitakiwa kung'atuka mwenyewe kabla ya kung'atuliwa na mkutano wowote.

Nyerere hakung'atuliwa na mkutano wowote. Mikutano yote ilikuwa inamwambia "Mwalimu bado tunakuhitaji".

Akang'atuka mwenyewe.
 
Nani kakwambia chama ni mtu mmoja? Kwamba hamna kamati kuu? Hamna baraza kuu? Hakuna bodi ya wadhamini? Duh kwa mindset hii unadhani siku Mbowe akifariki ghafla huoni utatokea mtifuano mkubwa sana wa nani kumrithi? Ni bora tu amuachie mwenyekiti mwingine huku akifanya mentorship taratibu hadi awe level zake asisubiri chama kipasuke kama yaliyomkuta Lipumba na Mbatia
Hahaha kwa nini AMUACHIE wakati Lisu kasema anatangaza nia KUGOMBEA? Na kama anagombea ,agombee na Mbowe au hiyo siyo Demokrasia pia? Naona mnataka apite bila kupingwa au awe mgombea pekee?
 
AMUACHIE wakati Lisu kasema anatangaza nia KUGOMBEA
Wapi nimesema Mbowe amuachie Lissu uenyekiti?
Na kama anagombea ,agombee na Mbowe au hiyo siyo Demokrasia pia?
Mbona hata kwenye Urais alichukua fomu ila baada ya kuona upepo wa Lissu akaghairi kurudisha fomu maana anajua asingepata hata kura 1. Kwahiyo Lissu hajawahi muogopa Mbowe in fact Mbowe anaogopa open election maana anaweza kushinda ila kwa kura chache possibly 52% sasa itampunguzia credibility na infallible status aliyokua amejiwekea na hawezi kubali hilo.
Naona mnataka apite bila kupingwa au awe mgombea pekee?
Hapana tunataka demokrasia agombee ila sasa asitumie incumbency kuharibu uchaguzi atavuruga chama. Akishindwa akubali matokeo na akishinda basi aweze kujenga umoja maana mpasuko utakua obvious.
 
Back
Top Bottom