Uchaguzi Malawi 2020: Hongereni wana wa Malawi, hakika nyie mnaongoza taifa huru

Uchaguzi Malawi 2020: Hongereni wana wa Malawi, hakika nyie mnaongoza taifa huru

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
11,936
Reaction score
15,196
Mutharika kaaanguka.

Haki imetamalaki Wananchi wameamua kumtoa kuhani madarakani. Sio mapolisi wala wana wa usalama walioingilia mchakato. Hatukusikia IGP wa huko wakiingilia mchakato na kuviita vyama vya upinzani vikiitwa vyama vya hovyohovyo kama anavyoita hapa kwetu bwana SIMON SIRRO.

Hii imetukumbusha kwamba wana wa nchi ndiyo waamuzi wakuu. Nawapongeza wana wa Malawi hakika nyie ni weledi
Hongereni na ujumbe umetufikia kwamba hata watawala wanaweza kuwekwa kando.

MAENDELEO SIO BARABARA TU. MAENDELEO YA KWELI HUANZA NA WATU.

Asanteni
 
Upo sawa lakini ebu fikiria kama angekuwa amejikita kutumia nguvu ya dola na kutengeneza vibaraka wakumsifu unadhani wananchi wangekuwa na namna ya kumtoa?
Hiyo dola yenyewe haimtaki...achilia mbali WANANCHI
 
Kikubwa wamalawi wamekataa ubeberu kama sisi Watanzania tunavyomuunga mkono Rais Magufuli kupinga ubeberu na kutetea Watanzania
ukatae ubeberu wakati hata taulo za kike unasaidiwa na wao. ulisika kwenye bajeti yenu hewa wakiitwa mabeberu kwamba ati Tanzania itapokea msaada wa EUPO kadhaa toka kwa mabeberu au hujui maana ya beberu wewe.

Akikusaidia mfadhili akikuuliza ujinga wa kupiga risasi wabunge unamwita beberu hovyo kabisa kama raisi aliyechaguliwa kiraia kuvaa magwanda ya jeshi ili kuwatisha waliomchagua
 
Hongera kwa MCP. Tanzania tunayo mengi yakujifunza toka kwa wenzetu Malawi.
 
Tume Imesema Nini
Unaweza Kukuta Jecha Yupo Njiani Akabadili Matokeo
 
Kwahiyo ili nchi iwe huru ni lazima upinzani uchaguliwe. Wananchi wakiamua chama Tawala kiendelee kushika madaraka kwa kuridhishwa na utendaji wake inakua siyo haki.
 
hata mapolisi wakikimbia na masanduku ya kura nayo ni halali kama kinondoni kwa mtuliya
Ukishindwa hoja, uungwana ni kukaa kimya au kukubali lakini siyo kuongea Uongo ili kuipa nguvu hoja yako. Hapo ukiambiwa uthibitishe jinsi polisi walivyokimbia na hayo masanduku ya kura utaanza kujambajamba.
 
Back
Top Bottom