Uchaguzi Mdogo Mbarali: Bahati Ndingo ashinda Kiti cha Ubunge

Uchaguzi Mdogo Mbarali: Bahati Ndingo ashinda Kiti cha Ubunge

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466
#CCM BABA LAO,

Matokeo ya uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya yametangazwa,

Mgombea ubunge kupitia CCM Bi. Bahati Ndingo ameibuka mshindi kwa kura elfu 44,334 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha ACT Wazalendo Bw. Dickson Kilufi, aliyepata kura 10,014.

#UCHAGUZI SIO UADUI HONGERA SANA ACT- WAZALENDO TUKUTANE 2024 & 2025 "MKISUSA SISI TWALA"

IMG-20230920-WA0006.jpg

=========

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali, Bw. Missana Kwangura amemtangaza Bi. Bahati Ndingo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 44,334 kati ya kura 56,095 halali zilizopigwa kwenye vituo 490 vya kupigia kura.

Bi. Ndingo amewashinda wagombea wengine 12 ambao walikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika jana tarehe 19 Septemba, 2023.

Kwenye uchaguzi huo ushindani mkubwa ulionekana ukiwa baina ya Bi. Ndingo na Bw. Modestus Kilufi aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, aliyepata kura 10,014.
 
Mwisho
 
Kwani huo nao ulikuwa ni uchaguzi, au muendelezo tu wa yale maigizo yetu ya miaka nenda ya bongo muvi!!

Bila yaKatiba mpya ya wananchi, na Tume Huru ya uchaguzi, kamwe hakutokuja kutokea uchaguzi huru na haki nchini.
 
Binafsi huwa ninawashangaa sana wale wote wanaoshiriki kwenye hilo zoezi.

Binafsi niliapa sitokuja tena kupiga kura chini ya Katiba hii ya ccm ya mwaka 1977, na pia Tume ya Taifa ya uchaguzi inayoteuliwa na Mwenyekiti wa ccm!

Nakumbuka mara ya mwisho kupiga kura ilikuwa ni 2015!
 
Back
Top Bottom