Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Ukiitazama na kuisikiliza hii video ya unabii huu toka kwa Mwl. Steven Jacob, toka Arusha, inafikirisha na kutafakarisha kiasi chake. Tazama na sikiliza👇🏻👇🏻👇
Kwa ufupi sana kwa wale wasio na vifurushi:
1. Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa sasa wa JMT) amekataliwa na Mungu - Jehovah, hatakiwi kugombea kiti cha Urais mwaka 2025. Si chaguo la Mungu - Jehova kuiongoza Tanzania mwaka 2025 - 2030..
2. Pamoja na kuwa ameshakataliwa, kitakachokuwa ni ajabu ni kuwa yeye na watu wake watalazimisha agombee. Na kwa mujibu wa unabii huu, ni kuwa atapitishwa kwa hila, atagombea lakini habari njema kwa wanamageuzi wote ni kuwa HATASHINDA UCHAGUZI HUO..!
3. Wakati huohuo ndani ya CCM yupo mtu ambaye Mungu keshamweka kuwa ndiye agombee na awe Rais ajaye wa Tanzania na jina lake katajwa kwa uwazi kabisa kuwa ni Bishop Josephat Gwajima. Ila wenzake ndani ya CCM watamkataa na hawatampa nafasi hiyo..
4. Kwa mujibu wa unabii huu, CHADEMA hawana mtu ambaye ana kibali cha Mungu - Yehova kugombea kiti cha u - Rais mwaka 2025 aliye ndani ya chama chao..
5. Na kwa kuwa Mungu tayari ameshampaka mafuta ya u - Rais wa nchi hii ndugu Josephat Gwajima, na kwa CCM watakuwa wamemkataa, basi Mungu atatengeneza mazingira ya kumtoa CCM na mara moja Freeman Mbowe au CHADEMA watampa nafasi ya ugombea u - Rais na CHADEMA kupitia kwa Ndugu Josephat Gwajima, watashinda na kuitawala nchi kwa mara ya kwanza..
6. Kwa Mama Samia Suluhu Hassan na CCM , unabii unasema, systematically Mungu ataachilia aibu iliyo kuu kwake na CCM itachinjwa kidogo kidogo mpaka ife kabisa..
============================================
1. Pamoja na kuwa sisi wakristo Biblia - Neno la Mungu linatuonya kuwa;
".....msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa kila namna.."
Lakini wakati huohuo Biblia hiyo hiyo inatuhadharisha kuwa ni lazima kila unabii (kila roho isemayo yatoka kwa Mungu) ipimwe katika vigezo vya Neno la Mungu (Biblia) kama ilivyoandikwa;
"...Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.."
Ukipimwa na ukaenda sambamba na Neno la Mungu, huo unabii au hiyo roho iliyoleta neno hilo itakuwa inatoka kwa Mungu na kwa hiyo hapaswi mtu kuubeza (kuutweza au kuudharau)..
2. Unabii wa huyu ndugu ni mzito sana. Unahusu hatima ya nchi na taifa letu na watu wa nchi hii kwa ujumla. Natoa wito kwa wajuzi wa maandiko (Neno la Mungu) waje hapa na kutoa uchambuzi usio - base katika hisia na maarifa ya kibinadamu bali ule unaozingatia Neno la Mungu (Biblia...)
3. Je, wewe unasemaje? Toa maoni yako...

MAONI YANGU
1. Pamoja na kuwa sisi wakristo Biblia - Neno la Mungu linatuonya kuwa;
1 Wathesalonike 5:20-22 SUV
".....msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa kila namna.."
Lakini wakati huohuo Biblia hiyo hiyo inatuhadharisha kuwa ni lazima kila unabii (kila roho isemayo yatoka kwa Mungu) ipimwe katika vigezo vya Neno la Mungu (Biblia) kama ilivyoandikwa;
1 Yohana 4:1-2 SUV