Uchaguzi mkuu kiti cha Rais 2025 (video): Unabii waweka wazi kuwa ni Samia S. Hassan (CCM) vs Bishop Josephat Gwajima (CHADEMA)...

Unabii wake ni feki huo...................haitokuwa hivyo....................
 
Mkuu

Nabii ni nyingi Hadi zinachanganya!!

Kuna wengine wanadiriki kusema Kuna vifo vya wakubwa Sasa tushike lipi!!?

Kuhusu mama ni kweli hats duru zinaonyesha ushindi wake sio wa.kura Bali wa Dola kama Dola haitagawanyika wakati was uchaguzi!!
 
Kwanini huungi mkono?

Unadhani nani atapinga au kuzuia jambo ambalo limeamuliwa tayari na Mungu mwenyewe?
Kama una kumbukumbu za kutosha utakumbuka kuhusu unabii wa nabii TB Joshua alipotangaza hadharani kuhusu Edward Lowassa kwamba huyo ndiye rais wa 5 Tanzania, na Mungu ndiye aliyemfunulia hayo.

Hivi umewahi kujiuliza kwa nini Edward Lowassa hakutimiza huo unabii? Mie naamini kuwa nabii TB Joshua alifunuliwa na mungu yule yule aliyemfunulia huyo nabii wa Arusha. Kinachonipa shida ni hiki.. Mungu alimuondoa duniani nabii TB Joshua, baadae akamuondoa na Edward Lowassa.

Mpaka leo Sijajua mwenye shida ni nani kati ya hawa watatu..
1. Mungu aliyemfunulia TB Joshua

2. TB Joshua aliyefunuliwa na huyo Mungu.

3. Edward Lowassa aliyetabiriwa kuwa ndiye rais wa awamu ya tano Tanzania.

Kumbuka TB Joshua na Edward Lowassa sasa.

Hebu nitatulie hiyo shida Ila nipate kuamini pia kuhusu Gwaji boy ndiye rais aliyetabiriwa
 
Inafikirisha Sana , kiukweli .
Mungu ni mwema hawezi kuwa upande wa siasa za uongo za Sisiemu na chadema.
 
Ni ujinga kiasi gani hata wakimpokea? Tambua Gwajima ni CCM then aende kugombea kule sio rahisi ,ishu ya Lowasa bado inawagawa wao kwa wao mpaka leo.

Kama kweli ni Mpango wa Mungu ,yule shekhe yahya yupo correct 💯 kwa sababu alitabiri mpaka kifo cha Magufuli mda mrefu sana ....Uhalisia ni kwamba Mama samia ni chaguo la Mungu.
 
Hii kitu nimeileta mimi hapa jukwaani..

Nilikuwa napita mitandaoni ni kuikuta huko. Nikawa very interested kuishea kwenye jukwaa kuu la mijadala ya kisiasa - JF..

Sijauamini na sijui kama nitauamini unabii huu. Bado nauchambua na kuupima kwenye mizani ya KWELI na HAKIKA...

Lakini ukweli ni kuwa, kuna maswali mengi ya kujiuliza na kuyajibu...

===============================================

KWA UPANDE MWINGINE: kwa wapenda mabadiliko na wanaoomba usiku na mchana CCM ianguke na kupotea ktk nchi hii, unabii huu kwao ni kama habari njema fulani hivi, unavutia na kuhamasisha kwelikweli na unagusa matamanio yao lakini ndani yake uko mtego hatari..

Ndo kusema kwamba, mtu hasa CHADEMA wanapaswa kuwa makini sana. CCM wako so desperate kubaki madarakani kwa njia yoyote. Wako kazini kuhakikisha CHADEMA inavurugika na viongozi wakuu hususani Freeman Mbowe na Tundu Lissu wanaparurana na kuvurugana..

Wako tayari kujigeuza malaika wa nuru aliyebeba matumaini lakini ndani ya moyo wake ni mbwamwitu na shetani hatari. Kwa sasa CCM inatumia mbinu na mkakati wa "mpige mchungaji, kondoo watawanyike..

Watu wasipumbazwe na CCM. CHADEMA kuweni makini na CCM...

Hebu kila mtu amfuatilie na kumsikiliza kwa makini huyu nabii. Kuna maeneo anasema "hili sitalisena kwa sababu..." au "hapa naomba nisiseme kwa sababu...."

Unabii halisi na wa kweli unaotoka kwa Mungu huwa very precisely clear and straight.

Nabii anapo deliver message toka kwa Bwana Yesu Kristo kamwe hatumii maneno "nadhani", "nafikiri" au "hapa nisiseme".

Ukiona mtu anayejiita nabii na ktk kutoa ujumbe wake anatumia maneno hayo☝🏻☝🏻, basi tambua moja kwa moja kuwa hicho anachosema ni chake na hata yeye hana uhakika nacho, ni mwongo huyo...

CCM wanaigopa CHADEMA vibaya sana. CCM wanamwogopa Tundu Lissu vibaya sana. Wasingependa kumuona anasimama na candidate wao yeyote mwaka kesho 2025..

Watakuja na kila political tactical theories kuhakikisha CHADEMA wanabugi na kujiingiza ktk mgogoro dakika za mwisho. CCM wako tayari kujidhalilisha na kumdhalilisha yeyote akiwemo mwenyekiti wao Rais Samia Suluhu Hassan ili mradi wabaki...

Hebu mtazameni na kumsikiliza tena na tena huyu nabii. Anatoka kwa Mungu kweli huyu?
 
Hao wanapigwa pesa mda mwingine wapo sawa kabisa ila kuna siasa wanaingiza hapo.

Kwanza tujue nguvu za Mungu zipo hatukatai ,maana hata kuwepo pale Mama samia ni nguvu nje wa uwezo wala hata yeye japo ya kuwa makamo ila hakuwa na nguvu enzi hizo ,alikuwa kama geresha kuleta usawa wa kijinsia na ishu ya muungano.

Kila jambo lina mda wake ,lolote linaweza kutokea ila hawa watabiri wengi wanatumika kisiasa .
 
Salaam, Shalom!!

Unabii unasema;

Hadi wakati huu tunavyoongea, aliye na kibali Toka Mbinguni kukalia KITI kikubwa Yuko chama tawala, mtu huyo Jina lake linaanza na herufi "J", na ni MMOJA wa watu Kutoka ukoo wa Lawi.

Nami nikaona jengo refu lililojengwa lenye Kona na mikunjo mingi, na juu ya jengo Hilo,kuna siafu na sisimizi wengi ambao KAZI Yao ni kuzuia washindani watakaopita juu ya jengo Hilo katika kinyanganyiro hicho.

Kisha nikaona kiongozi mmoja mkuu wa chama Cha upinzani ameshikilia barua ya kaki, pia nikaona , chama tawala kimeshika bahasha ya khaki na kilikuwa kinedhamiria kumpa "J" barua hiyo Kwa ajili ya shindano Hilo.

Ikaonekana kuwa, chama Cha kikuu Cha upinzani, pamoja na kushika barua Ile, hakikuwa na mtu wa kwenda kushiriki ushindani Ule.

Ghafula, akatokea mtu mmoja, aliyepita Kwa Kasi na kusafisha njia Ili shindano Hilo lianze Rasmi,

Kisha akatokea Binti apataye umri wa takribani miaka 18 hivi, Binti huyo alikuja Kwa Kasi ya ajabu na kupora bahasha Ile Kutoka chama tawala Kisha akaanza kwenda Kwa Kasi juu ya jengo Hilo.

"J" akaonekana mwenye mawazo akiangalia bila kujua nini Cha kufanya, Kisha nikaona ,kiongozi wa Upinzani akimpa bahasha "J" Ili kwenda kushindana na Binti yule.

UJUMBE:

Mungu anakiambia chama kikuu Cha upinzani kumpokea "J" maana atarudi nyumbani. "J" ndiye aliye na kibali Cha kuongoza na kushinda shindano lijalo, Maana Mungu ameamua huyo ndiye awe kiongozi ajaye.

Mungu amesema, atawapiga upofu chama tawala wasiweze kuandaa theory iliyo Bora ya kumsaidia aliyenyakua bahasha Ile iliyopasa apewe "J". Binti yule, siku ya kwanza atakayoshika mike kuanza shindano lile hatopata HOJA Imara kulingana na mshindani wake " J".

Mungu ameapa kupitia mtumishi wake kuwa, yeyote atakayejaribu kupindisha kusudi la Mungu kumzuia "J" atakutana na mkono wa Mungu, na itathibitika, nani mwenye nguvu na mamlaka, kati ya Mungu na wanadamu.

.............Mwisho wa Unabii..........

Source: Huduma ya Kristo, U-Tube channel, video ya tarehe 16 April , 2024.

Ameeen.
 
😂😂😂 Shekhe yahya alisema baada ya kuongoza mwanamke ,kwa mara ya kwanza chama cha upinzani kitashinda
 
Kila jambo lina mda wake ,lolote linaweza kutokea ila hawa watabiri wengi wanatumika kisiasa .
".. Ole wake mtu (nabii) asemaye kwamba Mungu amesema nami ilhali sijasema naye".

Hiyo ni kauli (onyo) kutoka kwa Mungu mwenyewe.

Walikuwepo na wataendelea kuwepo hao manabii wanaotumia kisiasa Ila mwisho wao huwa ni mmbaya kabisa.
 

1. Naweza kukubaliana na wewe kwa moja, kuwa, huu unabii umekosa vigezo vya unabii wa kweli toka kwa Mungu...

2. Nakubaliana na wewe kuwa, CHADEMA watashangaza ulimwengu tena kama wanaweza kufanya kosa la 2015..

3. Lakini sikubaliani na wewe 100% kuwa Samia Suluhu Hassan ni chaguo la Mungu..

Huyu mwisho wake ni sasa. Hawezi kwenda 2025. Akilazimisha kugombea, HATASHINDA KAMWE...

CCM ikiweka mtu mwingine (mwanaume) na awe Mtanganyika, inaweza kujikongoja na kushinda tena japo itakuwa kwa binde kwelikweli...
 
Labda CHADEMA tuwe tumerogwa! Gwajima?
 
Ume text-narrate vizuri sana..

Lakini huyu nabii hajaficha jina kwa herufi "J"

Amemtaja kwa uwazi kabisa kuwa ni Josephat Gwajima...
 
Ninaposema chaguo la Mungu ni wakati wa sasa ,baada ya miaka 5 ni ishu nyingine anaweza asiwepo...Yote sawa.

Kwa wakati uliopo ilipangwa ndio maana hata kifo cha Magufuli hakikutarajiwa ni mpango wa Mungu ambao upo nje ya uwezo wetu.


Lolote linaweza kutokea ,humu ndani kuna jamaa aliandika utabiri wa Mwanamke haswa Samia kushika usukani ,hatuwezi kudharau hatujui lolote .
 
Ninaposema chaguo la Mungu ni wakati wa sasa ,baada ya miaka 5 ni ishu nyingine anaweza asiwepo...Yote sawa.

Kwa wakati uliopo ilipangwa ndio maana hata kifo cha Magufuli hakikutarajiwa ni mpango wa Mungu ambao upo nje ya uwezo wetu.


Lolote linaweza kutokea ,humu ndani kuna jamaa aliandika utabiri wa Mwanamke haswa Samia kushika usukani ,hatuwezi kudharau hatujui lolote .
 
Tunaomba CV yake.
Asijekuwa mwanamfumo maana mara chache Mungu amejihusisha na mambo vyama vingi.
Manabii washakaji wa Trump walifanya sana haya wakati wa uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…