Uchaguzi Mkuu TFF - 27 Oktoba 2013: Jamal Malinzi Rais Mpya wa TFF!

Uchaguzi Mkuu TFF - 27 Oktoba 2013: Jamal Malinzi Rais Mpya wa TFF!

MPIRA WA TANZANIA Quishney,
watamkumbuka TENGA x100
mchakato mzima kweli wanashindwa kumtafuta mchezaji mwenye Uzoefu, akasaidiwa na Katibu Mkuu aliyesomea menejiment, Hii ipo sana kwa wenzetu ,Germany, Spain, Cameroun, Nigeria nk
Sasa mtu anatoka Mahakamani au kwenye Boxing na wala huko hakucheza leo mnamtwisha Mpira tena wa Vilabu vikubwa mashindano ya Afrika na Dunia,
Bora kushangilia Man U, Liverpool, Man City nk

Punguza povu dogo, hebu tukumbushe sisi mambumbumbu, Rais wa FIFA Sepp Blatter alichezaga timu gani ya UEFA?

Au ungetueleza Pele ni Rais wa shirikisho lipi la mpira? Au Wabrazil hamnazo?

Halafu utamu wenyewe Nyamlani hana hata ubavu wa kukimbilia mahakamani kwenda kupiga porojo kwa mahakimu wenzake ili apinge matokeo maana hii nyundo ya FIFA ya kukataza mambo ya mpira kwenfa mahakamani sasa watauona utamu wake kama walivyokuwa wanamtesa Michael Wambura.

Sikushangai kwa akili ukwaju kama zako siku ukipendekeza Rick Abdalah awe kocha wa Stars kwa umahili wa kupiga domo kwenye tv.
 
Unapokuwa na watu wawili wanaogombea nafasi moja ni dhairi mmoja atashinda. Nadhani sasa ni wakati wa kuachana na malumbano na kumuunga mkono Malinzi kama amepatikana kwa njia za kidemokrasia. Wapenda soka wote tumpe ushirikiano ili soka yetu osonge mbele. Tumeshuhudia Tenga akijenga misingi imara ya kukuza soka sasa basi Malinzi na timu yake waachane na mambo ya Usimba na Uyanga wawe kitu kimoja kwa manufaa ya bsoka yetu.
 
Hongera sana JM. Wahafidhina wameshindwa na ukweli.

Sasa tunataka kuona maendeleo ya soka letu na sio blah blah tena.

Prove them team Tenga that they were wrong in fighting against you.
 
Change WE CAN, Jana Rais Mpya alianza kwa kuvunja kamati zote..... yaani sasa kamati zitaundwa upya, Pili ametoa msamaha kwa wafungwa wote isipokuwa wale tuu wenye makosa ya rushwa na kupanga matokeo
CHANGE @ TFF is on the Corner
TUST WE CAN

Kumbe. Ndo maana nimepita tff nikakuta pako kimya!.
1382976577021.jpg
Mia
 
Mpira wa Tanzania umekufa.
Natilia sana mashaka upeo na malengo (vision na mission) yako kwa jinsi unavyochangia baadhi ya mambo. Ni lini mpira wa Tz ulikuwa hai mpaka uogope kuwa unakufa sasa!?
Sasa nakuwa na mashaka kuwa huenda na wewe ukawa kama wale wanaoshinda mitaa ya Msimbazi/Jangwani na tuvikombe twa kahawa huku jioni wakisubiri 'mfadhili' kuwaachia elfu tano ya kula. Na hawa ndio waanzilishi wakubwa wa fitina katika mpira wa nchi hii maana ukiwaambia mambo ya electronic tickets au klabu kuajiri makatibu na pesa kupitia kwenye accounts mnaleta hata mapanga. Ni wazi haya ndio pia unayaogopa maana ndizo sera za awali kabisa ambazo Jamal Malinzi anasimamia, labda mmkwamishe.
Kwa hiyo sema kitakachokufa sio mpira bali zile 'kamati za ufundi', 'mabaraza ya wazee na vijana' na vikundi vinavyopiga kelele pale Karume, Msimbazi, Jangwani ambavyo naanza kuamini kuwa nawe ni mmoja wapo.
 
Na yeye asilete za kuleta.
Tunachotaka atufikishe mbali kimpira.
 
Ukitaka kumuuwa nyoka kata kichwa tu.
Nyamlani na Tenga wake out hatuna haja na matokeo zaidi. Snake is already dead.
Mpira ndio umekufa hivyo
ungemuuliza Matumula kwenye Boxing walifanyweje
Sitashangaa wengine nikutafuta Ulaji tu maana Mpira mmeugeuza Siasa.
FAT walishampitisha Raia wa Nchi jirani kuongoza Soka letu,
sitashangaa leo yeyote mwenye Uchu wa pesa kuongoza soka au Siasa
Brazil hawawezi kufanya shughuli zozote za Mpira bila ya kumualika Pele.
Tunaiombea Safari njema TFF yetu macho
 
Mpira ndio umekufa hivyo
ungemuuliza Matumula kwenye Boxing walifanyweje
Sitashangaa wengine nikutafuta Ulaji tu maana Mpira mmeugeuza Siasa.
FAT walishampitisha Raia wa Nchi jirani kuongoza Soka letu,
sitashangaa leo yeyote mwenye Uchu wa pesa kuongoza soka au Siasa
Brazil hawawezi kufanya shughuli zozote za Mpira bila ya kumualika Pele.
Tunaiombea Safari njema TFF yetu macho
Unaboa............
 
Eti oooh Nyamlani ndio mgombea pekee wa Urais TFF! Kiko wapi sasa?

FIFA oyeeeee! Sasa hata Michael Wambura atakuwa na haki ya kugombea TFF.
na hao ndio utasikia mara 'mtu wa system lazima apite' ...'huwezi kushindana na serikali' na mengineyo. Kushindwa kwa hayo majaribio ni wazi nchi sasa inaelekea kwenye mabadiliko na ni onyo kwa wahafidhina wote popote walipo kuwa umma unaweza kuamua jambo na likawa!

 
Sasa ni wakati wa kutuomba radhi sisi ambao hatukumkubali tangia mwanzo
Nilishaomba radhi siku nyingi kaka..Na nilijuta kwa nini nilimpigia kampeni..Hata yeye nilimwambia humu..

Nawaomba sana radhi wanamichezo wenzangu humu JF kwa kumpigia kampeni Jamal Emil Malinzi. Mnisamehe kwa hilo.

Wengi tulitarajia mabadiliko kutoka kwa Malinzi..Alikuja hunu kuomba kura na ushirikiano, tulimpigia debe sana humu baadae akapotea...

Nitakuwa msitari wa mbele kupiga kampeni kuhakikisha kwamba Malinzi na genge lake hawarudi.
 
Back
Top Bottom