Uchaguzi mkuu ujao kufanyika mwaka 2026?

Uchaguzi mkuu ujao kufanyika mwaka 2026?

Hapana, Mama anamalizia urais wa JPM kwanza hiyo July 2025 halafu November 2025 ndio anaanza awamu yake, ila kwa vile kwa awamu ya pili ya JPM, Mama Mama nimehudumu miaka 4, hivyo hii inahesabika ni awamu yake ya kwanza na 2025 anamalizia ya pili.
P
Kikatiba ana haki ya kutawala kwa miaka 10. Akienda kama unavyosema itabaki kama miezi sita kutimia miaka kumi. Atakuwa na haki kugombea tena mwaka 2030 amalizie miezi yake sita? Hapa ni kwa sababu imebaki miezi michache. Tufanye magufuli angekufa mwaka huu. Mama angemaliza mitatu ya JPM. Kisha angeweza gombea 2025 na kufanya mitano. Jumla miaka 8. Kisheria anakuwa na hakli ya kuwa rais kwa miaka miwili tena. Anaweza gombea kuimalizia?
 
Kikatiba ana haki ya kutawala kwa miaka 10.
japo nikweli kikatiba urais ni awamu mbili za miaka mitano mitano, hii awamu ya kwanza ya Mama ni kumalizia awamu ya pili ya JPM ambayo kwake inahesabika ndio awamu yake ya kwanza ambayo inaisha August 30 2025 na kuanza awamu yake ya pili November 2025
Akienda kama unavyosema itabaki kama miezi sita kutimia miaka kumi. Atakuwa na haki kugombea tena mwaka 2030 amalizie miezi yake sita?
Hapana, 2025 - 2030 ndio awamu yake ya pili na ya mwisho.
Hapa ni kwa sababu imebaki miezi michache. Tufanye magufuli angekufa mwaka huu. Mama angemaliza mitatu ya JPM. Kisha angeweza gombea 2025 na kufanya mitano. Jumla miaka 8. Kisheria anakuwa na hakli ya kuwa rais kwa miaka miwili tena. Anaweza gombea kuimalizia?
Hapana, JPM angechomoka mwaka huu, Mama angemalizia miaka miwili ya JPM hadi 2025, halafu angekuwa na a full terms zake zote mbili from 2025 to 2035 hivyo angetawala for 12 years!
P
 
Chawa tumejipanga
Mambo ya katiba hayahitaji UCHAWA!.
akitaka awamu zaid tutasema 'katiba inasema Rais 'atachaguliwa' kwa awamu mbili ' …ikifika 2025 ndio atakuwa anachaguliwa kwa awamu ya kwanza…sasa hivi anamalizia kiporo cha Mpendwa wetu John Magufuli
Hapana, hiki kiporo cha JPM ndio awamu yake ya kwanza, hivyo hiyo ya pili ni mwisho.
watakaopinga hili tutashirikiana na wabia wetu wa maridhiano kutoka vyama Rafiki kupambana nao kwa jina la 'wahafidhina wasiopenda umoja na mshikamano'
Hii ni katiba ya nchi na sio ilani za vyama.
P
 
Maana huyu Rais wa sasa miaka yake mitano ya uongozi inatimia mwezi wa tatu mwaka 2026? Ina maana uchaguzi wetu wa urais unaofuata utafanyika mwaka huo?

Rais akifia madarakani miaka mitatu kabla ya muda wake , Makamu wa Rais atachukua nafasi ya urais na atachukuliwa kuwa ameanza awamu yake ya miaka mitano.
 
KImsingi Samia ni rais wa awamu ya 5. Hiyo kusema ni awamu ya sita walifoji tu ili kujitenga na makandokando ya Magufuli. Kikatiba alichukuwa alipoishia Magufuli na atamalizia pale amabapo alitakiwa kumalizia. Hata kama Magufuli angefariki 2024 mwezi wa 3 na yeye akapokea, bado 2025 ingekuwa uchaguzi.
Hakuna kitu kinaitwa awamu kwenye katiba
 
KImsingi Samia ni rais wa awamu ya 5. Hiyo kusema ni awamu ya sita walifoji tu ili kujitenga na makandokando ya Magufuli. Kikatiba alichukuwa alipoishia Magufuli na atamalizia pale amabapo alitakiwa kumalizia. Hata kama Magufuli angefariki 2024 mwezi wa 3 na yeye akapokea, bado 2025 ingekuwa uchaguzi.

Sio kweli. Ni awamu ya sita. Rais akifa kabla ya Mika mitatu anayemfuata atachukuliwa ameanza kipindi Cha miaka mitano, Yani awamu yake ya kwanza na atabakiwa na miaka mitano pekee ya kichaguliwa Tena.
 
Samia anamalizia ,awamu yake itaanza 2026 Hadi 2036 🔥🔥🔥

Hapana , kikatiba hii ni awamu mpya, maana Rais akifa ndani ya minne au mitatu kabla ya muda wake, Rais anayekuja atachukuliwa ameanza awamu ya miaka mitano na atabakia na awamu moja tu. Ndio maana hii ni awamu ya sita.
 
Chukua hii scenario. Tufanye JPM angekufa baada ya kutawala miaka miwili. Maana yake samia angemalizia mitatu na akigombea anapata mitano. Jumla 8. Lakini katiba inamruhusu kutawala miaka 10. Je anaweza kugombea tena na kutawala kwa miaka miwili?

Kwa hali iliyopo, ataweza kugombea na kutawala kwa miezi kama sita ambayo itapungua kwenye miaka kumi ya haki yake?

Hapana. Katiba inatambua miaka mitano, minne na mitatu Kama awamu moja. Ukifa ndani ya miaka miwili atakaye ridhi hatakuwa na awamu, atakuwa Rais wa mpito.
 
Chawa tumejipanga

akitaka awamu zaid tutasema 'katiba inasema Rais 'atachaguliwa' kwa awamu mbili ' …ikifika 2025 ndio atakuwa anachaguliwa kwa awamu ya kwanza…sasa hivi anamalizia kiporo cha Mpendwa wetu John Magufuli


watakaopinga hili tutashirikiana na wabia wetu wa maridhiano kutoka vyama Rafiki kupambana nao kwa jina la 'wahafidhina wasiopenda umoja na mshikamano'

Labda katiba ya China. Katiba ya Tanzania mwisho miaka mitatu. Sasa Magufuli kafa bado miaka minne na ushee. Hi ni awamu nyingine kikatiba na amebakiza awamu moja. Tusome katiba yetu.
 
The President term of office is 5 years. Kama tafsiri ni awamu basi Mkapa, Mwinyi, Kikwete walitawala awamu mbili mbili.
 
Maana huyu Rais wa sasa miaka yake mitano ya uongozi inatimia mwezi wa tatu mwaka 2026? Ina maana uchaguzi wetu wa urais unaofuata utafanyika mwaka huo?
Katiba yetu inajibu hoja yako Ibara 37 (5) inasema : 'Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufarariki dunia,kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mawili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais ,basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki. ' Kusema kuwa Samia ni Rais wa awamu ya sita ni huo ni upotoshaji na hatuwezi kuendelea kutembea kwenye upotoshaji huo Katiba ndiyo itakayofuatwa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Nimejaribu kupitia hoja za wadau naona wote wameshampitisha Mama kuendelea... Hii inamaanisha hakuna mtu anaamini ipo siku CCM itakosa kiti cha Urais? Kwa nini watu wana matokeo kabla ya muda? Enewei, Ramadhan Kareem.
 
Back
Top Bottom