Marehemu Magufuli alipofariki hakuacha Urais nyuma.
Pascal unaniangusha. Wewe mwanasheria kabisa unasema Rais Samia anamalizia Urais wa Magufuli! Hujawahi kusoma katiba?
Nenda kwenye katiba, ukaangalie ukomo wa Urais. Katiba inatamka wazi kuwa Rais aliyepo madarakani, Urais wake utakoma endapo atafariki, atajiuzulu, atakuwa amefutuwa uwanachama wa chama chake kilichomwingiza madarakani, ataugua kwa kiwango kitakachothibitika kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake, au Bunge likipiga kura ya kutokuwa na imani na Rais, na kisha kufanyika uchaguzi ambao utawarudisha theluthi mbili ya wabunge waliokuwepo.
Urais wake unapokoma, iwe kwa kifo, maradhi, kujiuzulu, kupigiwa kura ya kutokuwa na imani, n.k; Urais wake unakuwa umeishia pale. Hakuna anachokuwa amekiacha kwenye Urais. Katiba inaeleza tu nini kitatokea baada ya yeye aliyekuwa Rais, Urais wake kukoma. Inasema kuwa hakutakuwa na uchaguzi, badala yake aliyekuwa makamu wa Rais atakuwa Rais kumalizia kile kipindi kilichobakia kama yule aliyekoma kuwa Rais angeendelea kuwa Rais. Kwa hiyo Makamu wa Rais anamalizia kipindi kilichobakia mpaka kufikia kipindi cha uchaguzi kinachofuata. Hamalizii Urais wa mtangulizi wake, maana yule Urais wake umekoma. Anamalizia kipindi kilichobakia kufikia uchaguzi unaofuata. Na akimalizia kipindi hicho, huyo Rais atakuwa na haki ya kugombea tena kwa kipindi kimoja tu.