Pre GE2025 Uchaguzi ni mchakato, kama kujiandikisha, kuteuliwa, na kuapishwa kumekuwa na "madudu" sahau kuwa kesho kuna haki yoyote itatendeka kwa wapinzani

Pre GE2025 Uchaguzi ni mchakato, kama kujiandikisha, kuteuliwa, na kuapishwa kumekuwa na "madudu" sahau kuwa kesho kuna haki yoyote itatendeka kwa wapinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
27 November 2024
Tunduma, Tanzania

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Tunduma kamanda Boniface William Mwakabanje anazungumza


View: https://m.youtube.com/watch?v=jdUUVD-y6rg
Akiongea na waandishi wa habari kuhusu mchakato mzima wa uchafuzi katika uchaguzi TAMISEMI 2024 jinsi serikali ilivyoshiriki kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduma na Hakimu wa Wilaya zoezi zima kuapishwa kilichotokea mawakala wa CHADEMA walipofika vituo vya uchaguzi wasimamizi wasaidizi waliwazuia mawakala wa wagombea wa CHADEMA kuwa wamekosa sifa, vigezo hivyo kuzuiwa ...
 
Kigoma, Tanzania

ZITTO KABWE ATOA TAMKO BAADA YA MATOKEO YA UCHAFUZI WA UCHAGUZI WA TAMISEMI 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=E9dUDfGy_o4


Hakika hasira walionyesha wananchi wa Kigoma kwa kujitokeza kwa wingi kuonesha kuwa wingi wao haukuonekana katika uchafuzi wa uchaguzi wa TAMISEMI 2024, ni ishara ya kuwa "Hamkani Si Shwari " tena katika taifa la Tanzania.

Labda jambo kubwa litendwe na wenye mamlaka kuzima hasira za wananchi hawa, kwa viongozi wa serikali kufanya maamuzi yatakayoleta matumaini, baada ya wananchi kuonesha waziwazi katika mkutano huu mkubwa wa Kigoma leo tarehe 29 November 2024 kuwa wamechukizwa mno na uchafuzi wa uchaguzi wa tarehe 27 November 2024 TAMISEMI.
 
29 November 2024

Tamko la Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo kufuatia matokeo ya kura za Uchafuzi wa Uchaguzi TAMISEMI 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=EwG06kUG5Nw

Haya yamesemwa leo na Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo Magomeni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa TAMISEMI uliyofanyika Novemba 27, 2024.Pamoja na hayo Kiongozi huyu amewasisitiza wafuasi wapenzi na wanachama wasitoe ushirikiano kwa viongozi wa Chama cha mapinduzi waliyotangazwa washindi bila uhalali.
 
Hahaha ni wapumbavu kukubali kufanya mazungumzo na mwizi. Wangekaa mbali wamwache ajisahau wamlie timingi wammalize. KUFANYA mazungumzo na mwizi, ni ujinga labda nawe uwe mwizi.
 
Tumeona ukiukwaji mkubwa katika kujiandikisha, kuenguliwa wapinzani, /kuteuliwa. kuwekewa mapingamizi ya uongo na kweli, kuapishwa wamekataliwa, sasa UPINZANI mnadhani kesho ndiyo CCM watatenda haki?
Ni baada ya Kushindwa kujiandaa ndio malalamiko yanakuja.

Chama la kipuuzi na kijinga ambalo walikataa hata kutoa maoni kwenye muundo wa Tume na kanuni Mpya wanalalamika nini na wanamlalalikia nani hasa?
 
30 November 2024
Momba, Songwe
Tanzania

CHADEMA MOMBA - HUU SI UCHAGUZI, NI UCHAFUZI TAMISEMI 2024 !


View: https://m.youtube.com/watch?v=wK8_M-9cm_w
Wanachadema kutoka Momba wamepinga matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Viongozi hao wanadai kuwa uchaguzi huo hakuendeshwa kwa haki na usawa bali ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.
 
Tumeona ukiukwaji mkubwa katika kujiandikisha, kuenguliwa wapinzani, /kuteuliwa. kuwekewa mapingamizi ya uongo na kweli, kuapishwa wamekataliwa, sasa UPINZANI mnadhani kesho ndiyo CCM watatenda haki?
Nakubaliana na wewe
 
RAIS FELIPE NYUSI AKUTANA NA WALIOKUWA WAGOMBEA WA URAIS 9 OKTOBA 2024, KUTATUA MTAFARUKU NA MAANDAMANO YANAYOTISHI TAIFA

29 November 2024
Kigoma, Tanzania

Uchafuzi wa Uchaguzi wa TAMISEMI 2024 Tanzania, Sisi Ndiyo Washindi 27 November 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=QjZJlb7WqxU

Katika uchaguzi ukiomalizika wa mitaa, vijiji na vitongoji 2024 ndiyo washindi, waje uwanja wa Kawawa uliopo hapa Kigoma mjini washerehekee kama sisi ACT Wazalendo tuliofika hapa kwa wingi.

Kama chama tunawapongeza kwa ushindi huu mkubwa ingawa kuna waliotajwa kuwa ni washindi, wale watakalia ofisi lakini siyo kuongoza maana hawana watu sisi ACT Wazalendo tuna watu hawa waliojitokeza leo uwanja wa Kawawa.

Hivyo ushindi wa bandia walizotumia hazina uhalali hivyo tuwasusie hawa waliotangazwa washing kwa njia za kijambazi kwa kufanya unyanganyi wa ushindi mchana kweupe nyote mnaona ... ya 2019 na 2020 yamejirudia 2024 ..
1732974024703.jpeg
 
Back
Top Bottom