Ulichoandika ni uongo mtupu. Nadhani huijui siasa za USA kwa kina.
Trump hawezi kuimaliza vita ya Ukraine kwa sababu hakuianzisha yeye, vita ya Ukraine itakwisha siku Putin akishindwa vita au akiitwaa ukraine yoyote. Trump anasimama wapi katika hilo?
Kuhusu uzalishaji viwandani, Biden amekuwa ni rais bora kuliko wengi katika hilo, rekodi ambayo Trump hakuwahi hata kuiwaza.
Suala la LGBT kwa marekani linalindwa na sheria za kupinga upaguzi wa rangi na wahamiaji, hakuna namna Trump anaweza kukabiliana nalo bila kuipasua USA vipande vipande. Na makundi yenye mlengo wa kuunga mkono hayo ndio makubwa zaidi na yaliyobeba wapiga kura wengi wazuri kwa zaidi ya 70%. Trump apingane nayo halafu apigiwe kura na nani?
Kuhusu vita, anza kujiuliza mtazamo wa Trump kuhusu mashariki ya kati (ambapo kitisho cha vita ya dunia ni kikubwa zaidi), Trump anaunga mkono msimamo wa Israel kuendeleza vita na Kamala Harris anataka zaidi mazungumzo ya amani kusitisha vita. Na kanuni rahisi ya kihistoria huwa, Republican ni wapenda vita zaidi huku Democratic ni wapenda mazungumzo zaidi kwenye mizozo.
Mwisho kabisa ukitaka kujua ni kwanini Kamala Harris huenda atashinda urais kirahisi sana nenda kaangalie ni kwanini 2008 Democratic walimpitisha Obama kugombea urais na mwisho wamerekani wengi wakampigia kura na kushinda uchaguzi. Uchaguzi huu ni kama marudio ya mwaka 2008.