Hiyo ya Dar.. I hope itaisha kimya kimya maana ikilipuka JF mmekwisha... inaonekana mnapata nyeti nyingi kutoka serikalini hata mambo yasiyoandikwa au waandishi hawajui. eg Kwamba Kikwete alienda Ujerumani kunywa chai na kurudi kumuwahi Bush.

Mzee Mwenzangu,
Wewe ninakuaminia kwa dataz, na ninataka kuamini hizi picha ni za kweli kutoka huko Kiteto, na kwamba chanzo cha hawa wananchi kupigwa ni kiu yao ya demokrasia kwa kusaidia chama chochote cha upinzani kushindana na CCM, na kwamba wamepigwa kwa shinikizo la CCM, basi Tanzania tutakuwa tumefika mbali sana na ccm wanahitaji kutoa maelezo mazito on this ishu,
Bado ninatafuta ukweli zaidi kabla ya kuzisukuma mbele hizi picha.
Msekwa has been mentioned to get deeply involved . Umesikia katika kuhojiwa kasema anamlinda Msekwa na wametoka Dar . Sasa tunasemaje ?
Nathibitisha kuwa picha hizi ni za Kiteto. Kutoka kushoto, Msafiri Mtemelwa- Afisa Mwandamizi- Kampeni na Uchaguzi; Daudi Baraka; Joseph Fuime-Mwenyekiti wa Mkoa wa Ruvuma na Danda Juju Martin- Afisa Mwandamizi- Sera na Utafiti. I reserve my comments for now regarding this matter.
Tume ya uchaguzi nayo imeanza kuleta longo longo; Msimamizi wa uchaguzi ametoa barua inayoeleza kwamba lazima mawakala wa vyama watoke ndani ya kata ambazo wanasimamia kama mawakala. Mimi nilikuwa mgombea 2005, suala hili halipo kwenye sheria- nijuavyo mimi wakala anaweza kutoka sehemu yoyote ili mradi ni mtanzania. Mawakala wangu Ubungo wengine niliwatoa IFM, UDSM nk. Hapa CCM inataka CHADEMA isipate fursa ya kutoa mawakala nje ya Kiteto ambao hawawezi kuwahonga wala kuwatisha. Wanataka mawakala watoke wawe ni wananchi wa kawaida wa Kiteto ili wapate fursa ya kucheza michezo michafu dhidi yao. Hiki ni kipimo cha pili kwa Tume, kipimo cha kwanza kilikuwa pingamizi dhidi ya Kimesera. Sasa Tume Taifa inapaswa kuingilia kati na kumkemea Msimamizi wa uchaguzi ambaye kwa bahati mbaya kwa mujibu wa mfumo wetu wa Tume ya uchaguzi usio huru ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Kiteto ambaye ni mtumishi wa serikali na wengi wao ni makada wa chama tawala! Tunakutana na Tume hapa Dar es salaam kesho, natumai watatanguliza mbele sheria, haki na nia ya kujenga taswira kwa umma kwamba ni chombo huru kinachofanya kazi bila kupokea maelekezo toka CCM.
Huko Kiteto, tumewabana sana- wasipopata mwanya wa kutokea KITAELEWEKA. Hakuna Kulala...
JJ
Habari za kawaida
Posted Date::2/18/2008
Viongozi sita Chadema wajeruhiwa vurugu za uchaguzi
Na Mussa Juma,Kiteto
VIONGOZI sita waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka makao makuu ya chama hicho, wamejeruhiwa vibaya mmoja akiwa mahututi baada ya kupigwa na kuchomwa visu na kundi la vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa CCM na Polisi katika vurugu za uchaguzi Jimbo la Kiteto ambalo lipo wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Benedict Lusulutya (CCM) kufariki dunia hivi karibuni.
Licha ya kupigwa viongozi hao pia walimwagiwa kemikali machoni ambayo bado haijafahamika na kusababisha kutoona kwa zaidi ya nusu saa na mmoja wao hadi jana macho yalikuwa yake hayaoni.
Vurugu hizo zilitokea katika kata ya Kijungu wilayani hapa juzi majira ya saa 12 jioni , baada ya kundi la vijana hao maarufu kama Green Guard kutoka jijini Dar es Salaam, kuvamia viongozi hao wa Chadema wakiwa katika ofisi yao ya kata ya Kijungu kwa tuhuma za kuwapigia kelele wakiwa katika eneo lao la mkutano.
Waliopigwa ambao hadi jana asubuhi hali zao zilikuwa mbaya na wengine kulazwa katika hospitali ya wilaya hiyo ni Hamadi Mussa Yusuph Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Juju Danda, Afisa mwandamizi kurugenzi ya bunge na halmashauri kuu Taifa.
Wengine ni Joseph Freme(43) Mwenyekiti wa Ruvuma Chadema na mjumbe wa kamati kuu,Msafiri Mtemelwa, Kaimu Mkurugenzi wa kampeni na Uchaguzi,Selemani Mohamed mjumbe wa uchaguzi Kiteto.
Katika sakata hilo, dereva wa gari la makao makuu Daudi Baraka ndiye alijeruhiwa vibaya kwa kuchomwa visu na kupigwa vibaya ambaye hadi jana hali yake ilikuwa mahututi akiwa anaongezewa maji na kushonwa nyuzi kadhaa.
Freme alisema licha ya kupigwa viongozi hao, pia walikamatwa na kupigwa na polisi wa kituo kidogo cha Kijungu ambao awali walikuwa pamoja na viongozi wa CCM, Katibu Mkuu Yusuph Makamba na Makamu Mwenyekiti Pius Mswkwa.
"Sisi hatukupigwa sana na green guard pale ofisini lakini tulipofikishwa kituo kidogo cha polisi kijungu ndipo tulipigwa sana japo kuwa tayari mwenzetu alikuwa amechomwa kisu ubavuni," alisema Freme ambaye alikuwa hajaweza kutembea hadi jana.
Hata hivyo alisema mara baada ya kuona wakipigwa ovyo, alipiga simu kwa IGP na baadaye aliambiwa awasiliane na mkuu wa polisi mkoa wa Manyara ambaye baadaye ndiye alituma polisi kuja katika kituo hicho kutoka makao makuu ya wilaya hiyo umbali wa takriban kilometa 70.
Viongozi hao, waliashiwa na polisi majira ya saa tano usiku baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa,Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mbunge wa viti maalum Grace Kiwelu.
Viongozi hao mara baada ya kuandikisha maelezo yao kwa� mkuu wa polisi wa wilaya ya Kiteto,Archi Killo waliachiwa kwa dhamana na kupewa hati ya matibabu PF 3 na walitakiwa jana asubuhi kuripoti polisi.
Akizungumzia mgogoro huo, Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kijungu, Ibrahim Mdugo alisema vurugu hizo zilianza majira ya saa 12 jioni baada ya kundi la vijana hao wa CCM kuanza kulalamikia kelele kutoka kwa viongozi hao wa Chadema waliokuwa wakisimamia kwaya yao iliyokuwa inafanya mazoezi.
Mdugo alisema awali viongozi hao wa Chadema walikuwa na gari lao wakitangaza watu kujitokeza kupiga kura Februari 24 bila ya woga wakitumia vipaza sauti ambavyo CCM waliokuwa katika mkutano ulikuwa unahutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa,Pius Msekwa walikuwa wanalalamikia.
Nathibitisha kuwa picha hizi ni za Kiteto. Kutoka kushoto, Msafiri Mtemelwa- Afisa Mwandamizi- Kampeni na Uchaguzi; Daudi Baraka; Joseph Fuime-Mwenyekiti wa Mkoa wa Ruvuma na Danda Juju Martin- Afisa Mwandamizi- Sera na Utafiti. I reserve my comments for now regarding this matter.
JJ
Nyongeza tu: Danda Juju Martin ni Afisa Mwandamizi(Idara ya Sera na Utafiti) katika Kurugenzi ya Bunge na Halmashauri.
JJ
Viongozi sita Chadema wajeruhiwa vurugu za uchaguzi
Na Mussa Juma,Kiteto
VIONGOZI sita waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka makao makuu ya chama hicho, wamejeruhiwa vibaya mmoja akiwa mahututi baada ya kupigwa na kuchomwa visu na kundi la vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa CCM na Polisi katika vurugu za uchaguzi Jimbo la Kiteto ambalo lipo wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Benedict Lusulutya (CCM) kufariki dunia hivi karibuni.
Licha ya kupigwa viongozi hao pia walimwagiwa kemikali machoni ambayo bado haijafahamika na kusababisha kutoona kwa zaidi ya nusu saa na mmoja wao hadi jana macho yalikuwa yake hayaoni.
Vurugu hizo zilitokea katika kata ya Kijungu wilayani hapa juzi majira ya saa 12 jioni , baada ya kundi la vijana hao maarufu kama Green Guard kutoka jijini Dar es Salaam, kuvamia viongozi hao wa Chadema wakiwa katika ofisi yao ya kata ya Kijungu kwa tuhuma za kuwapigia kelele wakiwa katika eneo lao la mkutano.
Waliopigwa ambao hadi jana asubuhi hali zao zilikuwa mbaya na wengine kulazwa katika hospitali ya wilaya hiyo ni Hamadi Mussa Yusuph Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Juju Danda, Afisa mwandamizi kurugenzi ya bunge na halmashauri kuu Taifa.
Wengine ni Joseph Freme(43) Mwenyekiti wa Ruvuma Chadema na mjumbe wa kamati kuu,Msafiri Mtemelwa, Kaimu Mkurugenzi wa kampeni na Uchaguzi,Selemani Mohamed mjumbe wa uchaguzi Kiteto.
Katika sakata hilo, dereva wa gari la makao makuu Daudi Baraka ndiye alijeruhiwa vibaya kwa kuchomwa visu na kupigwa vibaya ambaye hadi jana hali yake ilikuwa mahututi akiwa anaongezewa maji na kushonwa nyuzi kadhaa.
Freme alisema licha ya kupigwa viongozi hao, pia walikamatwa na kupigwa na polisi wa kituo kidogo cha Kijungu ambao awali walikuwa pamoja na viongozi wa CCM, Katibu Mkuu Yusuph Makamba na Makamu Mwenyekiti Pius Mswkwa.
"Sisi hatukupigwa sana na green guard pale ofisini lakini tulipofikishwa kituo kidogo cha polisi kijungu ndipo tulipigwa sana japo kuwa tayari mwenzetu alikuwa amechomwa kisu ubavuni," alisema Freme ambaye alikuwa hajaweza kutembea hadi jana.
Hata hivyo alisema mara baada ya kuona wakipigwa ovyo, alipiga simu kwa IGP na baadaye aliambiwa awasiliane na mkuu wa polisi mkoa wa Manyara ambaye baadaye ndiye alituma polisi kuja katika kituo hicho kutoka makao makuu ya wilaya hiyo umbali wa takriban kilometa 70.
Viongozi hao, waliashiwa na polisi majira ya saa tano usiku baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa,Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mbunge wa viti maalum Grace Kiwelu.
Viongozi hao mara baada ya kuandikisha maelezo yao kwa� mkuu wa polisi wa wilaya ya Kiteto,Archi Killo waliachiwa kwa dhamana na kupewa hati ya matibabu PF 3 na walitakiwa jana asubuhi kuripoti polisi.
Akizungumzia mgogoro huo, Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kijungu, Ibrahim Mdugo alisema vurugu hizo zilianza majira ya saa 12 jioni baada ya kundi la vijana hao wa CCM kuanza kulalamikia kelele kutoka kwa viongozi hao wa Chadema waliokuwa wakisimamia kwaya yao iliyokuwa inafanya mazoezi.
Mdugo alisema awali viongozi hao wa Chadema walikuwa na gari lao wakitangaza watu kujitokeza kupiga kura Februari 24 bila ya woga wakitumia vipaza sauti ambavyo CCM waliokuwa katika mkutano ulikuwa unahutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa,Pius Msekwa walikuwa wanalalamikia.
Mnyika poleni sana na haya masaibu yote mkuu,
Watanzania wanawaombea mfanikiwe!
Vilio vya watoto wachanga wenye njaa!
Vilio vya mama wajawazito wasio na dawa!
Maombi ya wapenda haki na amani yako nanyi!
JF na wapenda haki na amani wanawapongeza!
Kazi mbele mkuu mpaka kieleweke ila inatisha!
Sauti ya Mwafrika wa Kike, sauti iliyo nyikani.
Mwangwi wake utasikika Kiteto.
Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu.
Jasho jingi, machozi kidogo, damu kiduchu.
Yote ni kafara katika demokrasia changa.
Itolewayo ardhini kunyoshea mabadiliko.
Ushindi ni lazima.
Ipo siku itakuwa kweli.
Watu wachache wanaweza kuteseka wakati mchache.
Ili watu wote wafurahi wakati wote.
Utawala wa watu hutokana na watu.
Ndiyo maana ya demokrasia yenyewe.
Maendeleo ni kwenda mbele.
Haki hujitokeza uovu unapoonekana hadharani ukitahayari.
Ps: Tuelekea katika kipindi kigumu tarehe 24, kipindi cha kupiga kura na kulinda kura. Popote ulipo, unaweza kufanikisha ulinzi wa kura katika vituo takribani 220 vitavyotumika kupiga na kuhesabia kura. Kwa kuwezesha wakala mmoja kuwepo siku nzima bila wasi wasi, usiku na mchana. Bila hofu ya kupata chakula wala maji. Shime, wakati ni huu!
Mzee Mwenzangu,
Wewe ninakuaminia kwa dataz, na ninataka kuamini hizi picha ni za kweli kutoka huko Kiteto, na kwamba chanzo cha hawa wananchi kupigwa ni kiu yao ya demokrasia kwa kusaidia chama chochote cha upinzani kushindana na CCM, na kwamba wamepigwa kwa shinikizo la CCM, basi Tanzania tutakuwa tumefika mbali sana na ccm wanahitaji kutoa maelezo mazito on this ishu,
Bado ninatafuta ukweli zaidi kabla ya kuzisukuma mbele hizi picha.
Huyo ni kiongozi wa Chadema Bw. Baraka Daudi baada ya kupewa mkong'oto kwenye Kituo cha Polisi huko Kiteto.
Hawa ni viongozi wengine wa Chadema wakiwa kituo cha Polisi baada ya kupigwa wakiwa mikononi mwa Polisi./CENTER]
Ni nani anayeleta mambo kama ya Kenya? Najaribu kumtafuta RPC na OCD wake, this is unacceptable!!!
.......................
Licha ya kupigwa viongozi hao pia walimwagiwa kemikali machoni ambayo bado haijafahamika na kusababisha kutoona kwa zaidi ya nusu saa na mmoja wao hadi jana macho yalikuwa yake hayaoni.......