CCM hawawezi kulaani kitendo hiki, na hawawezi kulaani Polisi au wale waliohusika. Watakachojaribu kufanya ni kukielezea na kuwaruka hao vijana!
Unajua kutafuta sifa ni kubaya sana. Hawa green cards (pun intended) si ndio huku wanaitwa "rent a cop"? Sasa kwa vil wanavirungu, magwanda ya kijani na nyeusi na mikanda mipana na migumu ya kimgambo mgambo wanafikiri wamekuwa Polisi? Sasa kwa vile ni walinzi wa "Bwana Mkubwa" basi wanadhani wanaweza kuingia popote huku wakipeperusha virungu vyao wakidai mbingu ziiname?
Sitarajii hata kidogo kwa Makamba au Msekwa kutoa kauli yoyote ile ya kulaani zaidi ya kuwakana vijana hao. Hivi sasa wamekuwa wakijaribu kulizima jambo hili kimya kimya lakini ndio likatufikia na sasa kimeungua... Nadhani hii picha moja ichapwe kwenye ukurasa wa mbele wa magazeti kama walivyofanya ile ya Kubenea...
Bado hatujasahau yalyotokea Kenya, yanaibuka hapa hapa kwetu mbele ya macho yetu.
Kuwaruka hao vijana haitoshi. Hapa CCM wanatakiwa waonyeshe moyo wa kuyakataa haya. Njia yoyote ya kutaka kujikosha na tukio kama hili haisaidii kabisa. Hakuna sababu, hata kama ni kwa kuchokozwa inayoweza kukubalika hawa watu wafanyiwe haya. Hii ni kujichukulia sheria mkononi na kutoa adhabu.
Unajua kutafuta sifa ni kubaya sana. Hawa green cards (pun intended) si ndio huku wanaitwa "rent a cop"? Sasa kwa vil wanavirungu, magwanda ya kijani na nyeusi na mikanda mipana na migumu ya kimgambo mgambo wanafikiri wamekuwa Polisi? Sasa kwa vile ni walinzi wa "Bwana Mkubwa" basi wanadhani wanaweza kuingia popote huku wakipeperusha virungu vyao wakidai mbingu ziiname?
Sitarajii hata kidogo kwa Makamba au Msekwa kutoa kauli yoyote ile ya kulaani zaidi ya kuwakana vijana hao. Hivi sasa wamekuwa wakijaribu kulizima jambo hili kimya kimya lakini ndio likatufikia na sasa kimeungua... Nadhani hii picha moja ichapwe kwenye ukurasa wa mbele wa magazeti kama walivyofanya ile ya Kubenea...
Poleni ndugu zetu mliopata kashkashi huko Kiteto...
Nguvu za Polisi dhidi ya wananchi waso na hatia zikemewe...Polisi Jueni kuwa Nguvu mlizonazo si za milele..Yupo wapi Mahita? Yupo wapi Zomba? jueni mkiwa na mioyo ya Kuwapiga raia wenzewenu mjue kuwa ipo siku Haki itasimama nanyi mtafikishwa ktk Vyombo vya Sheria.
Kama mnafanya Haya kwa matashi yenu..please yaacheni..lkn kama mnatumwa basi chukueni Mfano wa Muhammad Ali mpiga makonde mmarekani aliekataa kutii Amri ya kwenda kupigana Vietnam kwa kuwa hapakuwa na Haki yoyote ya kupigana.Nanyi kataaeni AMRI zote za kuwapiga ndugu zenu...Siasa si chuki
KAMA NI KWELI KATIBA INALINDA HUU UOZO WA WATANZANIA DHIDI YA WATANZANIA BASI NI LAZIMA TUIBADILISHE..SASA HIVI NA SI ANYOTHER TIME...MAANDAMANO YAANZE..YA KUIBADILISHA NCHI YETU TOP BOTTOM!WANANCHI WASIPOAMKA SASA WATAKUWA WATUMWA AGAIN KWENYE ARDHI YAO WENYEWE!KWANI UTUMWA SI LAZIMA AWE MZUNGU AMA MUARABU!kMA HUNA UHURU KIASI HICHO SASA SI UTUMWA?NASEMA KATIBA IBADILISHWE!MSAFIRI MTEMELWA NAYE SI ANA UZOEFU WA MUDA TU!ANAELEWA UNYAMA WA POLISI LONG TIME!HAKUNA HATA WANASHERIA WA KUWASHTAKI HAO POLISI PAMOJA NA BOSI WAO?MASHTAKA YAFUNGULIWE KAMA NI GHARAMA WANA JF TUTACHANGA!HATUA SAHIHI ZA KINIDHAMU ZICHUKULIWE DHIDI YA HAO WA KINA ZOMBE!WANYAMA NA WAKATILI!MAFISADI WASIKUWA NA HURUMA KWA BINADAMU WENZAO KISA NI UTOFAUTI WA NAMNA YA KUILETEA MAENDELEO NCHI YETU!AAKH HII INATIA HASIRA!Wana JF
Lazima tukumbuke kuwa katiba yetu ni ile tuliyopewa na mkoloni, na kikatiba/kisheria polisi wanapewa haki na kulindwa kisheria kutokana na vitendo vyao vya kupiga watu. Polisi wetu wana uwezo mkubwa wa kutumia nguvu kuliko kutumia akili, kama ilivyokuwa polisi wa kikoloni, kwa hiyo hapa tukiwalaumu sana polisi, ambao wanatumwa tunaweza kuwa tunawaonea. Tunaweza kuwalaumu kwa kutotumia busara zao kuangalia lipi wanatakiwa kufanya wanapotumwa kufanya kazi zao.
Kupiga ni unyama na ni ushenzi, lakini lazima tuwe tunaelekeza mapambano kwa wanaowatuma polisi hao.
Nakumbuka kuna kipindi mkuu mmoja wa polisi alikuwa anatuma polisi kufanya kazi kwenye maeneo kama hayo kwaa masharti kuwa, hakuna kuua wala kuumiza mtanzania, bila sababu ya msingi. Kama waandishi wa habari wakipata nafasi ni vizuri kuwauliza wakuu wa polisi ni kwanini wamefanya hivyo. Na tupiganie utaratibu wa watanzania kuwa na ulinzi kutokana na unyama na ukandamizaji kutoka kwa vyombo vyetu vya dola!
Katika kuendeleza ufahamu kwa watanzania, na kujenga msingi imara ili kuleta changes juu ya katiba. Ni lazima kwanza kuifahamu katiba ambayo inaleta maumivu kwa wananchi wote....
http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf